Kodi yangu ya nyumba imeisha tangia juzi namuona Mama Mwenye Nyumba hata salamu hana ushirikiano mzuri kabisa na mimi

Ernest 255

Member
Oct 7, 2020
42
27
Wakuu kodi yangu ya nyumba imeisha tangia juzi lakini naona Mama mwenye nyumba nikimuamkia hana ushirikiano mzuri kabisa,,, sasa sijaelewa kwa sababu sijamlipa kodi yake.

Kiukweli huwa sijawai pitiliza hata siku moja tangia kukaaa kwake na huwa nikimlipa kodi yake huwa ananipa na elfu kumi ananiambia kanywe soda,, sasa nashindwa kuelewa anashindwa kuniambia au? Maana huwa hatuna mazoea kabisa mimi na yeye zaidi ya salamu tu na kama anajambo la kuniambia huwa anamuagiza mtoto wake.

Na hapa sina hata dalili za kupata hiyo kodi leo wala kesho,, embu nishaurini wakuu nimwambie nitampa nikipata au nimuache hadi nikipata nimpe?
 
Mkataba wenu unasemaje?Kisheria ni baada ya miezi sita,mwambie sina kodi mpaka baada ya miezi miwili hawezi kufanya lolote.
 
Si ajabu aliwapa tarehe ya juzi wanaomdai kuwa atawalipa.
Mimi mwaka jana 2019 nilifukuzwa kama mbwa Arusha kisa nilichelewa kulipa kodi na huyo mama mwenye nyumba tulikuwa tunasali katika jumuiya moja ya wakatoliki aliona aibu kunifukuza yeye akaona bora amtume mumewe.

Tangia hapo ndio nikaamini katika pesa hakuna urafiki wala udini aisee.
 
Sasa hivi hali ya mzunguko wa pesa ni mbaya sana Tanzania.
 
Mimi mwaka jana 2019 nilifukuzwa kama mbwa Arusha kisa nilichelewa kulipa kodi na huyo mama mwenye nyumba tulikuwa tunasali katika jumuiya moja ya wakatoliki aliona aibu kunifukuza yeye akaona bora amtume mumewe.

Tangia hapo ndio nikaamini katika pesa hakuna urafiki wala udini aisee.
Pesa siyo tuu inavunja urafiki bali hata undugu unakufa. Kuna jamaa waliuza nyumba ya urithi wakagawana pesa, sasa mmoja wapo alikuwa hayupo, akamuomba dada yake apokee mgao wake amewekee. Sasa dada naye akapata tamaa akaitumia kwenye biashara pesa haikurudi. Mpaka leo mwaka wa 5 hawaongei, acha kabisa.
 
Daaaah, noma sana mkuu
 
Back
Top Bottom