habari zenu jamani, mimi ni mgeni kidogo humu, sina mda sana. nilikua napitia tu maongezi na comment za watu na nkavutiwa kujiunga. anyway turudi kwenye point ilionileta hapa.
Nlikua nna mpenzi wangu ambaye alikua workmate wa kaka angu, akatokea kunipenda na mimi nkampenda tukaanza mahusiano hapo. kiukweli nilimpenda sana na nikahisi ndie atakaekuja kuwa mume wangu coz alikua na sifa zote nilizozihitaji. tulianza mapenzi vizuri sana mpaka nkawa nahisi duniani tumebaki wawili tu mimi na yeye. lakini kuna siku alipa mashaka kidogo. ikumbukwe kuwa mimi bado nakaa kwetu na nilikua ndo nimemaliza chuo nasubiri majibu nianze na utaratibu wa kutafuta kazi. kwa jinsi nilivyokua nampenda nililazimika kusema uongo nyumbani na kwenda kulala kwake, na hata siku nyingine kutoroka kabisa ili tu niawe na yeye.
Basi bwana, siku hiyo nilienda kwake nikalala huko, sasa asubuhi mapenz yakazidi akasema haendi kazini anataka tushinde wote ilkua siku ya jumatatu. Badae kama saa tatu akapigiwa simu aende ofisini, ikabidi aende, kufika akapewa barua ya kusimamishwa kazi akarudi akawa upset sana. basi nikajaribu kumpoza pale akatulia kidogo sasa baadae akawa ameeka simu kwenye chaji, na mimi nimeweka ya kwangu huku nai2mia pale pale, ikawa simu yake ikiita ananiambia nimpe anapokea. Ikapigwa simu ya mdada ikiwa imeseviwa ....... na picha yake nkampa hakupokea, akaimute! akapiga tena kama mara 5 hivi nikwamwambia mbona hutaki kupokea akanijibu 'aah! msumbufu huyu' akapiga tena akapokea akamwambia nitakupigia badae. basi bwana, m nkaendelea na zangu, kwakua huwa sipendi kugusa simu ya mpenz wang nkamuacha na sikumuuliza.
Siku nyingine tukiwa tunaangalia tv mchana nkapitiwa usingizi kwenye kochi, nikalala! simu yangu niliiacha pembeni kidogo na yeye alikua karibu yangu, basi akachukua simu yangu na kuanza kusearch, sasa kwa sababu simu yangu kila ukiitouch inatoa mlio flani hivi, nikastuka lakin hakujua kama npo macho coz nilikua nimegeukia upande mwingine, akaikagua sana siku hiyo na mimi nkamuacha coz nlikua najiamini. Basi alvyomaliza badae nkajifanya nmeamka, kushija simu yangu nakuta vitu viko shagalabagala, si unajua mtu chako bana, akitumia mwingine unajua tuu, nkamuulza umeshika simu yangu akataa huku akiwa amebadilika usoni. Badae akaniulza kuna watu nilikua nachat nao kama frends akajua ni mabwana zangu, nkamtoa wasi wasi na kuwapigia kabisa akaamini.
Sasa baada ya hapo nkahisi kuna kitu kinaendelea, kuna siku usiku tunataka kulala namba ile ile iliopgwa siku ile mara nyingi ikapigwa tena, hakupokea... nkaona anamtumia msg... asubuh yake wakati yupo bafuni nkachukua simu yake na kuangalia nikakuta msg zaa ajabu, nikaja kumuuliza akaniambia yule ni rafiki yake tu wamezoeana sana..... niliumia sana coz huwa sipend kudanganywa, yakapita hayo akaomba msamaha yakaisha.
Sasa visa vikawa haviishi mara nimpigie asipokee, mara aanze kunambia kama simtaki nimwambie kisa sijampigia wala kumtext wakat na yeye kakaa kimya, kuna kipindi tukaa siku 3 bila mawasiliano yoyote yale, nkaanza kuchoka sasa.
Lakini siku hyo ndo nilichoka zaidi, alikua amesafiri kwenda kwao kwa ajili ya arobaini ya babu yake, akarudi, akataka niende siku ambayo anarudi nikamwambia haiwezekan ntakuja kesho. Basi kesho nkaenda nkakuta mafuta ya mwanamke hizi lotion za kujichubua na yametumika limebaki kama nusu kopo, nikamuuliza akaniambiambia ni ya mdogo wake wakati wanarudi akayasahau kwenye begi lake wakati huyo begi lipo sebleni amelitupa na kuniambia ajalifungua amefika na kuliweka hapo na kulala, na mimi nilienda asubuhi mida ya saa 3 na wakati nafika ndo aliamka kunifungulia geti (shangaeni maajabu hayo) basi nkakaa kimya tu, nikawa nafanya usafi wa kupanga nguo kabatini nkakuta nguo zimefichwa kwenye mfuko za kike, nikamuuliza za nani akasema za dada ake mmoja hivi aliziacha wakati anahama, nikamwambia mbona siku zote napanga nguo humu sijawahi kuziona na mimi huwa nikipanga nguo natoa kabati zima linakua tupu kabisaa naanza kuwekaa upyaaa.
Akakosa cha kunijibu ndipo nkachukua simu yake baadae kuangalia kwenye picha nakuta picha za utupu za mwanamke na zimetumwa jana yake, na mwanamke mwenyewe ndo yule wa awali aliekua hapokei simu zake. Kumuuliza ananiambia kuna rafiki yake alimtumia kitamboo akasema aangalie watoto wa chuo wanavyofanya uchafu wa kupiga picha za uchi, nkamuuliza una uhakika unachakisema ni kweli akajibu ndiooo, nkamuonyesha tarehe siku mwezi na saa iliyotumwa akawa anajing'ata hana cha kujibu mara akawa mkali anataka tugombane, mi nIkachukua vitu vyangu nikaondoka nyumbani nkamwambia 'its over' akajibu 'poaa maisha mema' tukaachana. Ikumbukwe penzi hili halina hata miezi miwili. lakini imepita mwezi sasa hatuna mawasiliano, na nahisi bado nampenda, kuna siku nmemtumia msg hakunijibu, lakini bado nampendaa nawishi arudi na kuadmit mistake zake..... sijui nyie wenzangu mnaonaje.
naombeni ushauri..... nifanyajeee
ni hayo tu.