Habari zenu jamani,
mimi ni mgeni kidogo humu, sina muda sana. Nilikuwa napitia tu maongezi
na comment za watu na nikavutiwa kujiunga, anyway turudi kwenye point
ilionileta hapa.
Nlikua nina mpenzi wangu ambaye alikua workmate wa kaka yangu, akatokea
kunipenda na mimi nikampenda tukaanza mahusiano hapo.
Kiukweli nilimpenda sana na nikahisi ndie atakaekuja kuwa mume wangu coz
alikua na sifa zote nilizozihitaji. Tulianza mapenzi vizuri sana mpaka
nikawa nahisi duniani tumebaki wawili tu mimi na yeye.
Lakini kuna siku alinipa mashaka kidogo. Ikumbukwe kuwa mimi bado nakaa
kwetu na nilikua ndo nimemaliza chuo nasubiri majibu nianze na utaratibu
wa kutafuta kazi. Kwa jinsi nilivyokuwa nampenda nililazimika kusema
uongo nyumbani na kwenda kulala kwake, na hata siku nyingine kutoroka
kabisa ili tu niwe na yeye.
Basi bwana, siku hiyo nilienda kwake nikalala huko, sasa asubuhi
mapenzi yakazidi akasema haendi kazini anataka tushinde wote ilkuwa siku
ya jumatatu. Baadae kama saa tatu akapigiwa simu aende ofisini, ikabidi
aende, kufika akapewa barua ya kusimamishwa kazi akarudi akawa upset
sana.
Basi nikajaribu kumpoza pale akatulia kidogo sasa baadae akawa ameweka
simu kwenye chaji, na mimi nimeweka ya kwangu huku naitumia pale pale,
ikawa simu yake ikiita ananiambia nimpe anapokea.
Ikapigwa simu ya mdada ikiwa imeseviwa na picha yake nikampa hakupokea,
akaimute, akapiga tena kama mara 5 hivi nikwamwambia mbona hutaki
kupokea akanijibu 'aah! msumbufu huyu' akapiga tena akapokea akamwambia
nitakupigia badae.
Basi bwana, mimi nikaendelea na zangu, kwakuwa huwa sipendi kugusa simu
ya mpenzi wangu nikamuacha na sikumuuliza.
Siku nyingine tukiwa tunaangalia TV mchana nikapitiwa usingizi kwenye
kochi, nikalala, simu yangu niliiacha pembeni kidogo na yeye alikua
karibu yangu, basi akachukua simu yangu na kuanza kusearch. Sasa kwa
sababu simu yangu kila ukiitouch inatoa mlio fulani hivi, nikastuka
lakini hakujua kama nipo macho coz nilikua nimegeukia upande mwingine,
akaikagua sana siku hiyo na mimi nikamuacha coz nlikua najiamini.
Basi alivyomaliza baadae nikajifanya nimeamka, kushika simu yangu
nakuta vitu viko shagalabagala, si unajua mtu chako bana, akitumia
mwingine unajua tuu, nikamuuliza umeshika simu yangu akataa huku akiwa
amebadilika usoni.
Baadae akaniuliza kuna watu nilikuwa nachat nao kama friends akajua ni
mabwana zangu, nikamtoa wasi wasi na kuwapigia kabisa akaamini.
Sasa baada ya hapo nikahisi kuna kitu kinaendelea, kuna siku usiku
tunataka kulala namba ile ile ilipopigwa siku ile mara nyingi ikapigwa
tena, hakupokea. Nikaona anamtumia message asubuhi yake wakati yupo
bafuni nikachukua simu yake na kuangalia nikakuta message zaa ajabu,
nikaja kumuuliza akaniambia yule ni rafiki yake tu wamezoeana sana.
Niliumia sana coz huwa sipendi kudanganywa, yakapita hayo akaomba
msamaha yakaisha.
Sasa visa vikawa haviishi mara nimpigie asipokee, mara aanze kunambia
kama simtaki nimwambie kisa sijampigia wala kumtext wakat na yeye kakaa
kimya, kuna kipindi tukaa siku 3 bila mawasiliano yoyote yale, nkaanza
kuchoka sasa.
Lakini siku hyo ndo nilichoka zaidi, alikua amesafiri kwenda kwao kwa
ajili ya arobaini ya babu yake, akarudi, akataka niende siku ambayo
anarudi nikamwambia haiwezekani nitakuja kesho.
Basi kesho nikaenda nikakuta mafuta ya mwanamke hizi lotion za
kujichubua na yametumika limebaki kama nusu kopo, nikamuuliza akaniambia
ni ya mdogo wake wakati wanarudi akayasahau kwenye begi lake wakati
huyo begi lipo sebuleni amelitupa na kuniambia hajalifungua amefika na
kuliweka hapo na kulala, na mimi nilienda asubuhi mida ya saa 3 na
wakati nafika ndo aliamka kunifungulia geti (shangaeni maajabu hayo)
basi nikakaa kimya tu. Nikawa nafanya usafi wa kupanga nguo kabatini
nikakuta nguo zimefichwa kwenye mfuko za kike, nikamuuliza za nani
akasema za dada ake mmoja hivi aliziacha wakati anahama, nikamwambia
mbona siku zote napanga nguo humu sijawahi kuziona na mimi huwa
nikipanga nguo natoa kabati zima linakua tupu kabisaa naanza kuwekaa
upyaaa.
Akakosa cha kunijibu ndipo nikachukua simu yake baadae kuangalia kwenye
picha nakuta picha za utupu za mwanamke na zimetumwa jana yake, na
mwanamke mwenyewe ndo yule wa awali aliyekua hapokei simu zake.
Kumuuliza ananiambia kuna rafiki yake alimtumia kitamboo akasema
aangalie watoto wa chuo wanavyofanya uchafu wa kupiga picha za uchi,
nikamuuliza una uhakika unachokisema ni kweli akajibu ndiooo,
nikamuonyesha tarehe siku mwezi na saa iliyotumwa akawa anajing'ata hana
cha kujibu mara akawa mkali anataka tugombane, mimi niIichukua vitu
vyangu nikaondoka nyumbani nikamwambia 'its over' akajibu 'poaa maisha
mema' tukaachana.
Ikumbukwe penzi hili halina hata miezi miwili, lakini imepita mwezi sasa
hatuna mawasiliano, na nahisi bado nampenda, kuna siku nimemtumia
message hakunijibu, lakini bado nampendaa nawishi
ivi bint miezi miwili utalalaje kwa mwanaume?