Nahisi ananipenda

Nahisi ananipenda

Habari zenu wakuu;

Kuna jambo linanipa tabu kidogo, kuna sister mgeni kanisani kwetu amekuja kuungana na ma sister wengine kuendeleza utume.

Sasa kila nikikutana naye huwa kama ananipenda hivi, muda mwingine tunaangaliana kwa kuibia ibia halafu kama tunafurahi hivi.

Sijui ni nini hiki ila mimi nimempenda kweli na nauhakika anajua au hata kuhisi hivyo, sijui naanzia wapi. Kila nikimkumbuka natamani Jumapili ifike nikutane naye, nifurahi.

Wajuzi wa haya mambo naombeni uzoefu wenu.
Mkuu nyie ni Wahindi? Kama ndiyo, toeni movie mtauza sana. Anyway zingatia kile kinachokupeleka kanisani
 
Muokoe sister wa watu pengine anahitaji sana mwanaume. Msaidie bhana ye hawezi kukuanza muanze tu usiwaze. Ila jua tu siku ya kukutana tu ndio anaupata ujauzito.
 
Muokoe sister wa watu pengine anahitaji sana mwanaume. Msaidie bhana ye hawezi kukuanza muanze tu usiwaze. Ila jua tu siku ya kukutana tu ndio anaupata ujauzito.
Ahsante mkuu Kwa uzalendo wa kiroho, huu ushauri ni mzuri, niko tayari kumtwaa akipata ujauzito itakuwa poa zaidi tutamalizia hatua zilizo bakia.
 
Anakupenda eehee.......kumbe kaambiwa ulikuwa nakatabia Ka kuchota sadaka na mara nyingi umeonywa bila kuacha.......SASA jiangalie umewekewa mtego ukinasa na kanisani hapo ndio bye bye
 
Weee jamaa mpuuzi kweli,,, Mwanamke kukuangalia tu tayari unajua kakupenda?
 
Duh we noma nikajua unaenda kusali church kumbe unaenda kuangalia warembo kwel Imani ngumu sana tutafika mbinguni tumechoka sana
 
Habari zenu wakuu;

Kuna jambo linanipa tabu kidogo, kuna sister mgeni kanisani kwetu amekuja kuungana na ma sister wengine kuendeleza utume.

Sasa kila nikikutana naye huwa kama ananipenda hivi, muda mwingine tunaangaliana kwa kuibia ibia halafu kama tunafurahi hivi.

Sijui ni nini hiki ila mimi nimempenda kweli na nauhakika anajua au hata kuhisi hivyo, sijui naanzia wapi. Kila nikimkumbuka natamani Jumapili ifike nikutane naye, nifurahi.

Wajuzi wa haya mambo naombeni uzoefu wenu.
Mtongoze muwe wapenzi haukatae usister muoane,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom