Nahamishaje sexual energy kwenda kuwa mafanikio au business delevopment energy?

boss,hiyo ni akili yako ulivyoiseti ila ushauri kama hujaoa fanya haraka kuoa japo siyo solution ya muda,tatizo lako ni akili pili soma vitabu mbalimbali huenda upata idea nzuri za kukuondoshea tatzo na mwisho sali sana,mazoezi na fanya uwekezaji wa akili na rasilimali.
 
Hilo lenyewe lishoga amwone msichana gani sasa? You are not serious. Amekuwa yupo horny all the time. Hushangai?
 
Chukua Kitabu cha Think and Grow rich cha Napoleon Hill, chapter 10. Isome, usipo elewa au ukitaka manufaa zaidi, karibu inbox broo, nikupe ka semina ka Nusu saa kwa njia simu.

Wengine tuna nguvu ktk maneno kuliko maandishi
 
Haupo peke yako bw wewe, mpo wengi!

Kuna kisa niliwahi kukisoma, tena mwalimu kabisa huko Uingereza, yupo jela huko USA kwq sasa.

Alifuata penzi la mtandaoni kumbe alikuwa akiwasiliana na matapeli, kufika uwanja wa ndege, akapokelewa na minjemba ya mtandao wa dawa za kulevya yaliyokuwa yamehuck mawasiliano yake tangia mwanzo wa mawasiliano.

Alipoteremka tu uwanjani, yameshammaki, yakamuuliza utambulisho na kumpatia furushi yakidai yameachiwa yamkabidhi ili aende ampelekee mpenzi wake huyo.

Kumbe misheni yalingeuza 'punda' ili ayavushie nje ya uwanja huo mzigo.

Alipotoka airbport akaishia mikononi mwa vyombo vya dola na asiweze kukutana na mpenzi wake huyo, sii unajua tena mkamatwa na ngozi ndiye...?

Cha kufanya wewe, lazima uwe na mpangilio wa kufanya mambo yako kwa kadiri.

Katika maisha usifanye jambo likakufanya teja, baadaye lazima likuletee tu madhara.

Hayo mambo yanarekebishika tu kwa maamuzi thabiti toka moyoni mwako wewe mwenyewe bila ya ushauri toka kwa mtu.

Midhali umeshagundua kuwa njia ya maisha unayoifuata ni batili, basi ni rahisi kujirekebisha na kufuata misingi sahihi ya maisha.
 
Kitendo cha kuanza kugundua tu kuwa mwenendo wako sio mzuri ni mwanzo mzuri. Ila pili jaribu kumshirikisha rafiki yako wa karibu(rafiki anayekupa makavu live), ambae anaweza kuwa anakushauri unapotaka kufanya maamuzi yasiyo na faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…