Nahama Aliexpress naenda Ebay

Nahama Aliexpress naenda Ebay

Pole sana mdau. kama wadau wengine walivyokushauri cha muhimu zingatia haya
  1. Soma reviews za watu walionunua vitu kwa huyo seller uone wana mrate vipi, kama ana reviews chache akili kichwani (ingawa anaweza kuwa ndo ameanza karibuni, ila the rule of thumb ni kwamba reviews chache stay away)
  2. Make sure wakati una search kitu unataka nunua kushoto kwako chagua suppliers ambao ni verified na wanatoa trade assurance hawa ikitokea cha kutokea aidha watakuletea mzigo mwingine ama hela itarudishwa wewe utachagua (nimejaribu kuweka screen shot hapa naona imegoma)
  3. wakati una search bidhaa unayotaka hakikisha pale palipoandikwa sort by unachagua order maana yake ni kwamba watakuletea kwanza suppliers ambao wameuza hiyo bidhaa unayotaka kwa wingi sana ukilinganisha na wengine -yaani bidhaa zao zina ubora/hawana longo longo ndo maana wameweza kuuza kwa wingi ukilinganisha na wengine
  4. kama ni supplier mpya kabisa ni vizuri ukaomba akutumie sample ya bidhaa unayotaka kabla hujaweka hela kununua mzigo mkubwa
  5. ukipata ishu kama hiyo report kwa alibaba/aliexpress mapema waweze mblock huyo seller asiwaumize wengine
binafasi nanunua na kuuza alibaba miaka mingi tu sijapata shida kabisa.pole sana
 
Mkuu kwa mfano nikitaka Computer used kupitia Amazon unaweza kumupa shipping fee Yao na tax deposit na itachukua muda gani kufika TANZANIA?
Kwa experience yangu machine used Tanzania ni rahisi kuliko masoko ya nje, huwa maofisi ulaya/marekani wakibadili computer zinakuja kubwagwa huku. Niliwahi nunua Fujitsu moja gen ya 4 ina touch screen na stylus kwa 320,000 discountkubwa ukiniambia nikwambie mahala bei rahisi zaidi online sina pa kukuonesha.

Ila kama unataka machine kali ya gaming ama computer latest Amazon na masoko mengine ya marekani kama Newegg, bestbuy etc utapata bei nzuri.
 
Tatizo hamazoni hawakubali kuandika bei tofauti na uliyonunua kwenye proforma invoices zao kwahiyo ukikutana na kodi unatwangwa kwelikweli
Unafanya tu utafiti, soko la marekani si sawa na la China, mfano unakuta simu kama oneplus 8 mwaka jana ilikuwa inauzwa hadi dola 600, kwenye sale inashuka hadi $250, ukiinunua simu pamoja na usafiri na kodi hadi hapa haifiki dola 400 hivyo unapata kifaa kipya cha uhakika umelipa kodi na bado bei rahisi.

Cheza na website kama slickdeals vizia vitu vikishuka bei nunua wala hutahangaika na hayo mambo mengine.
 
Kwa experience yangu machine used Tanzania ni rahisi kuliko masoko ya nje, huwa maofisi ulaya/marekani wakibadili computer zinakuja kubwagwa huku. Niliwahi nunua Fujitsu moja gen ya 4 ina touch screen na stylus kwa 320,000 discountkubwa ukiniambia nikwambie mahala bei rahisi zaidi online sina pa kukuonesha.

Ila kama unataka machine kali ya gaming ama computer latest Amazon na masoko mengine ya marekani kama Newegg, bestbuy etc utapata bei nzuri.
Kuna watu wanahitaji PC used ila sijui wapi pa kuwa naziagiza mkuu. Kama unafaham sehemu niambie hata PM
 
Nikawaida yangu kuagiza bidhaa mtandaoni na nimeisha pokea order zaidi ya tatu ndani ya muda sahihi Ila hii order ya mwisho ndo ilikuwa matata nimeagiza mzigo wangu LCD Display ya iPhone 6 plus muda umefika nimepokea mzigo wangu kuja kuangalia nakutana na LCD ambayo inaonekana ni used alafu zile lock zake za pembeni zimekatwa Tena zimekatwa kifujo fujo mbaya zaidi kitu chenyewe hakifanyi kazi kiufupi ni dead.

Nime OPEN DISPUTE nikaelezea kila kitu baadae AliExpress wananiambia nirudishe bidhaa ili nirudishiwe pesa zangu na ninavyojua ningumu Posta yetu kutuma vitu nje hasa vitu Kama hivi.

SASA ALIEXPRESS NAVUNJA NAO MKATABA
Mimi niacha zamani sana. Niliagiza Bluetooth speaker wakaniletea used
 
Karibu sana, Ebay ni uhakika hata kitu usipokipenda unakirudisha tu within specified time.
 
Kuna watu wanahitaji PC used ila sijui wapi pa kuwa naziagiza mkuu. Kama unafaham sehemu niambie hata PM
Watu wengi hasa wasomali wanazinunua kwa Bulk zikitolewa kwenye Makampuni.

Ila hata ebay unazipata mfano angalia hii list

Hapo ni laptop 6 za 6th gen kwa $810 inamaana kama laptop 1 kwa $135, hazina hdd hazina os. Zikija huku wanazipolish zinaingia dukani refurbished.

6th gen i5 huku ni Around laki 6.
 
Nikawaida yangu kuagiza bidhaa mtandaoni na nimeisha pokea order zaidi ya tatu ndani ya muda sahihi Ila hii order ya mwisho ndo ilikuwa matata nimeagiza mzigo wangu LCD Display ya iPhone 6 plus muda umefika nimepokea mzigo wangu kuja kuangalia nakutana na LCD ambayo inaonekana ni used alafu zile lock zake za pembeni zimekatwa Tena zimekatwa kifujo fujo mbaya zaidi kitu chenyewe hakifanyi kazi kiufupi ni dead.

Nime OPEN DISPUTE nikaelezea kila kitu baadae AliExpress wananiambia nirudishe bidhaa ili nirudishiwe pesa zangu na ninavyojua ningumu Posta yetu kutuma vitu nje hasa vitu Kama hivi.

SASA ALIEXPRESS NAVUNJA NAO MKATABA
Possibly wewe mwenyewe ndio tatizo , inawezekana hukusoma vizuri maelezo. Hili tatizo lipo kwa watz wengi. Wepesi kuhukumu na kulaumu wengine Kwa makosa yao wenyewe.
 
Miaka hii nadhani hakuna shida, manake tangu nimeanza sijawahi kuona tatizo...labda mzigo utachelewa kidogo lakini unafika.
Mshukuru sana MUNGU, Mi juzi juzi tu hapa, walinipiga 130K, nlinunua bidhaa ikaja mbovu, kurudisha kimoja, kila nkiwauliza wana nambia swala langu linashughulikiwa tena hadi wanakua wakari, ipo siku yako we endelea tu.
 
Nikawaida yangu kuagiza bidhaa mtandaoni na nimeisha pokea order zaidi ya tatu ndani ya muda sahihi Ila hii order ya mwisho ndo ilikuwa matata nimeagiza mzigo wangu LCD Display ya iPhone 6 plus muda umefika nimepokea mzigo wangu kuja kuangalia nakutana na LCD ambayo inaonekana ni used alafu zile lock zake za pembeni zimekatwa Tena zimekatwa kifujo fujo mbaya zaidi kitu chenyewe hakifanyi kazi kiufupi ni dead.

Nime OPEN DISPUTE nikaelezea kila kitu baadae AliExpress wananiambia nirudishe bidhaa ili nirudishiwe pesa zangu na ninavyojua ningumu Posta yetu kutuma vitu nje hasa vitu Kama hivi.

SASA ALIEXPRESS NAVUNJA NAO MKATABA
Niliagiza mzgo wangu free shipping toka mwezi wa tisa hadi sasa
 
Back
Top Bottom