Nafikiria Kuwashitaki PPF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafikiria Kuwashitaki PPF

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mtoboasiri, Apr 20, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  Mimi ni mwananchama wa PPF, ninafikiria (na naamini nitaungwa mkono na wanachama wenzangu kwa hili) kuwapeleka mahakamani ili nihamishe michango yangu mahali pengine. Ni wanyonyaji wakubwa, wakati wanalipana mafao ya mamilioni kwa kufanyakazi miaka mitatu, bosi wangu alieanza kuchangia miaka ya 70 (alipata Masters na ACCA 1972 na akastaafu 2008) amelipwa chini ya Milioni 20 na pension yake ya mwezi ni 80,000).

  Naomba msaada tafadhali wandugu tuondoe uonevu huu.
   
 2. M

  Mshika Moja Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malipo ya mafao yanategemea na mshahara wa mwanachama anayestaafu, hivyo ukienda PPF watakuonesha wanavyokokotoa mafao hadi kupata salio lako, baada ya kukata kodi of course.

  Hata hivyo, labda kupitia SSRA (Social Security Regulatory Authority) watasaidia ku-harmonise pension benefits nk; kama utakumbuka SSRA imeanza kazi na juzi juzi tu Mkuu wa Kaya amezindua Bodi ya SSRA na sasa wameanza regulatory role yao, pengine itasaidia kutoa comfort kwa wanachama kwani Pension Entities wako na pesa nyingi sana. Moja ya promise ya SSRS ni kuwa wananchi/wanachama watakuw ahuru kujiunga na Mfuko wowote wa hifadhi ya jamii bila vikwazo wala mikwara yoyote.

  Nakushauri nenda kawaone PPF (Members Srvices) utasaidiwa kabla kujaenda mahakamani, unaweza kukwama au kupoteza muda.
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  tatizo lipo kwetu wenyewe tena hasa watumishi wa umma na hasa serikali tunaoshangilia mishahara midogo na marupurupu mengi, hasara zake ni kukosa wekezo sahihi na kuishi maisha yasio sahihi

  fikiria
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Walioko kwenye hiyo authority wengi ndio hao hao walikuwa PPF sidhani kama kuna jipya ni mvinyo uleule kwenye chupa mpya
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbona unaficha jina sasa kama unataka kushitaki ? come out open
   
 6. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mkuu,umejuaje kuwa hili sio jina langu?
   
Loading...