Nafikiria kufanya maamuzi magumu

Nafikiria kufanya maamuzi magumu

kama wananichukia na wanichukie ila wanaume wa kihaya wana gubu,wivu,ubinafsi mfumo dume uliotukuka hata kitchen party hawawaruhusu wake zao kwenda

hahahaaa....mie simo.
 
Kuwa na subira maanaaa yanaweza yakakupata matatizoo huko. Baraka za wazazi ni muhimu.
 
Ni kheri uwasikilize wazazi, wengi waliokaidi wazazi wamefikwa na makubwa na mengine mabaya sana. Angalia tu familia isije kuchukua maamuzi ya kukutenga.
 
mzinguaji huyu hana point... dushe imemchanganya.....
 
No way kuna muda maamuzi magumu yanahitajika, imeandikwa tuheshimu wazazi lakini isiwe fimbo basi...mi pia nshafanya maamuzi magumu na naona hali inakua shwari taratiibu!!!
 
kama wananichukia na wanichukie ila wanaume wa kihaya wana gubu,wivu,ubinafsi mfumo dume uliotukuka hata kitchen party hawawaruhusu wake zao kwenda

Acha mbwembwe dogo, waende kwenye kitchen party kwani wao ni wazaramo???
 
biblia inasema, mwanamke atawaacha wazazi wake na kuambatana na mumewe, lakini kuna utaratibu wake, wewe naona unalazimisha, hivyo itasomeka mwanamke atawakimbia wazazi wake na kuambatana na mzinzi mwenzake.
 
Waheshimu baba na mama yako upate baraka na miaka mingi duniani
 
Wazazi wetu ndio wa kwanza kuliona jua kabla yetu kwa hiyo wanayafahamu mambo mengi ya ulimwengu kuliko sisi likiwamo hilo la mapenzi kwani katika kipindi cha maisha yao hadi kufikia hapo walipo, walishapitia mambo mengi ya misukosuko ya ulimwengu na walishapata taabu nyingi sana za ulimwengu na ndio maana leo hii tunafaidi busara zao na kwa kutumia uzoefu wao kwenye ulimwengu huu wanatuelekeza njia za kuishi ili maisha yetu yawe na ustawi bora...tusichokijua ni kuwa wazee wetu nao hapo mwanzo walikuwa vijana kama sisi na waliwahi kuwa katika mahusiano kama sisi na wakaumizwa na mapenzi kama sisi....kwa hiyo katika mambo tunayoyafanya leo hakuna jipya kwao ni kama tunayarudia tu yale waliokuwa wakiyafanya wao......na kwa udhoefu walionao kwenye ulimwengu wamegeuka kuwa walimu wazuri kwetu kama tukiamua kufuata mafunzo yao kwa umakini...kwa uzoefu walionao wanaweza kutambua tabia ya mtu hata kwa kumuangalia tu.....na ndio maana wazee wetu walikuwa wakiwachagulia wake vijana wao wa kiume na ndoa zikadumu mpaka leo hii tunashuhudia babu na bibi zetu wakizeeka pamoja kwani wanajua tabia njema ndio silaha na wala sio uzuri wa sura wala umbo...nina uhakika kuwa hao wazazi wako hawawezi wakakupeleka wewe sehemu mbaya kwa sababu wanakupenda na ndio maana wakakulea hadi kufikia hapo ulipo....wazazi wako watakuwa wameona kuna kitu ambacho si kizuri kwa huyo mpenzi wako...lakini wanaogopa kukwambia kwa kuwa huwezi kuwaelewea kwani wewe hapo ulipo unaongozwa na hisia kuliko uhalisia wa jambo lenyewe.....nakushauri kaa chini ongea na wazazi wako kwa hekima na utapata muafaka wa jambo lako kwani imeandikwa kuwa tuwaheshimu baba na mama zetu ili tupate kuishi miaka mingi hapa duniani......TAFAKARI CHUKUA HATUA.........

wewe ni mmoja kati ya watu wachache wenye UELEWA humu jamiiforums.
Naamini huu ndo ushauri mzuri aliopaswa kupewa.
GOOD THINK.
 
habari za hapa,

mimi ni binti age 26yrs nafanya kazi ktk kampuni fulani hapa Dar, nina mchumba wangu tulipanga kuoana tangu mwaka jana nilipopeleka taarifa home wazazi wakawa wagumu kwa sababu nyingi sana ambazo kimsingi sijaona kama zina umuhimu sana. mambo yakawa magumu na hatimaye tukakubaliana mimi na mchumba wangu tusubiri hadi mwaka huu.
Sasa mwaka ndo huu umefika bado naona mambo c shwari sana. sasa tumepanga na huyu mtarajiwa kama watagoma nihamie kwake tu, sio siri hapa nina hali mbaya sana kimawazo,.

badae kidogo nitawaeleza kuhusu hili suala langu vizuri ili mnipe ushauri. ila sio siri nina waza kufanya maamuzi magumu sana yani mimi nihamie tu kwa mwanaume na hali nimewashemu wazazi, ila leo wao wananifanyia hivi.

pole ya mimi. soon nitwaeleza mwanzo mwisho.

Waafrika tuna oa au kuolewa kwaajili ya familia zetu! Kamwe kama wazazi hawato kubali hutoishi kwa amani na hata huyu Mchumba wako hatokubali kukaa na mtu ambaye hana baraka za wazazi!

Mapenzi yenu hayana maana yeyote kama yatakosa baraka za wazazi hakika!

Tafuta maelewano na wazazi wako huna uwezo wa kushindana nao na kama unataka kushindana nao hakika unapoteza muda na utashindwa kabisa!
 
No way kuna muda maamuzi magumu yanahitajika, imeandikwa tuheshimu wazazi lakini isiwe fimbo basi...mi pia nshafanya maamuzi magumu na naona hali inakua shwari taratiibu!!!

Ni sawa tena hongera kwa ujasiri ila maamuzi yako si sheria lakini maandiko ktk kitabu kikuu ni sheria.
 
Back
Top Bottom