Mimi bado naona wazazi wanaona mbali,inawezekana hawana argument sahihi ya kukataa binti asiolewe na huyu kijana lakini wakawa sahihi
Ni dhahiri binti anampenda sana huyu kijana na yupo tayari hata kukosana na familia yake hii ni sacrifice kubwa sana ninamashaka kama ingekuwa ni upande wa huyo kijana angeweza kujitolea hivyo....kutokana na historia fupi ilioandikwa hapa utaona kabisa huyo kijana alishachumbia mabinti wawili wengine kifupi hana msimamo
Tamalisa wakati hamna mawasiliano huyu kijana hakuwa na no. yako?????kwanini wewe ulipomtafuta ndipo akaonyesha nia ya kukutana na wewe???kama kweli alikuwa na nia nawe kwa njia yoyote angekutafuta.
Hii ni view yangu lakini kwa kifupi ndoa inahitaji baraka kutoka kwa wazazi au walezi wanaotuzunguka sishauri ufanye maamuzi ya kulazimisha.
Inawezekana wazazi wako pia wanaonyeshwa mbali,uchumba wako pia ni wa kisiri mimi sijapenda jipange upya kiakili uanze moja kama Mungu alipanga mtaoana tu ila sio kwa hayo maamuzi