Nafikiri nahitaji kuwa na watu wapya

Nafikiri nahitaji kuwa na watu wapya

Aisee mkuu ni kweli kukosa hela kubaya sana

Ukipata shida ndo utaelewa ubaya wa umaskini
Kwa kweli tutafute hela, hela ina raha yake
Hela ina heshma yake

Nawazia watu wasio na kipato kabisa namna wana survival nakosa majibu

Kusaidiana kumekuwa nadra sana
Wale wasiokuwa na kitu hawapati changamoto kama yule ambae alipata fedha halafu zikamuisha, huyo ana kazi ya ziada.
 
Kuna dogo nilikuwa namkuta ghetto yuko na wenzie wanajazanà hapo zaidi ya watano.

Siku kanifata kapungukiwa na kama 70000 ya kodi. Nikamuuliza ina maana wenzio wote huwa na kukutaga nao ghetto hakuna hata mmoja wa kukuazima hiyo hela. Akasema hawana.

Nikamwambia piga chini kampani za design hiyo, so hata mnavyokaa huwa mnajadili nini si mnaongezeana ufaukara tu hapo.
 
Wewe umewahi msaidia Nani hata laki mbili?....huwezi tafuta watu wapya wa kukusaidia Kama wewe humsaidii mtu...usikute mama yako katoa pesa vicoba na wewe akikwambia twende vicoba unaona ishu za wazeee...


Ushauri wangu jiunge vicoba ..au Sacco's au fanya biashara zenye network ya watu wengi wenye Sacco's....ili usiwe MTU WA kutoa lawama Kwa wasiohusika
 
Wewe ndio umeshindwa kuwatumia watu wako hao kwa manufaa badala ya kukopa ungeanzisha kabiashara ili wakuungushe ni rahisi mtu akanunua simu ya laki tano kwako kuliko akukopeshe
 
Hao watu mia nane wote kwenye phone book wa kazi gani.
Kuna watu mnaweza kwa kweli.
Ndio ile una manamba mengi hata mengine hayanaga maana kujaza tu phone book.
Halafu mara nyingi ukiwa na tatizo anza na wale ambao umewahi kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine kuliko kuanza kumtafuta mtu hujawasiliana nae muda,hujawahi mpa msaada wowote halafu akusaidie ni ngumu.Angalau yule aliyepo karibu au umemuweka karibu anaweza kukusaidia.
Halafu sio mara zote ukiwa na shida utasaidika wakati mwingine hata wale waliopo karibu au umewahi kuwasaidia wanashindwa kukusaidia mana nao wanakosa kama ulivyokosa wewe.
Japo Kuna wale hata uwasaidie vipi ila wewe yakikufika unapambana na hali yako yeye hanaga kila siku na shida ni za kwake.
Mimi nimejiwekea kuna watu wachache tunasaidiana katika shida na hao nikipata tatizo wakikwama basi.
 
Tatizo siku hizi ukimkopesha hasa sisi wabongo hatulipi ndio tatizo linaanzia hapa ukimkopesha mbongo hesabia tu umeipoteza hela na ukimdai hela uliyomkopesha inakua ugomvi.
Nb;Hata niwekewe bastola shingoni simkopeshi mbongo
 
Aaah aaah
 

Attachments

  • 255717606434_status_c6cff573148f4abcb8643f0ed60ca1f0.jpg
    255717606434_status_c6cff573148f4abcb8643f0ed60ca1f0.jpg
    58.5 KB · Views: 13
Tatizo siku hizi ukimkopesha hasa sisi wabongo hatulipi ndio tatizo linaanzia hapa ukimkopesha mbongo hesabia tu umeipoteza hela na ukimdai hela uliyomkopesha inakua ugomvi.
Nb;Hata niwekewe bastola shingoni simkopeshi mbongo
Huu ndio ukweli mchungu. Wabongo sio waaminifu kabisaaa.
 
Kati ya unaoita watu wako 800+ wenye uwezo wa kuwa na milioni ni WATANO tu, itoshe tu kusema wewe ni mtu wa chini sana….. na hao watano sio marafiki zako na wala sio hadhi yako bali umesevu namba zao tu.
yaan umepita mule mule kwenye mshono.[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Huwez kuwa na contact 800+ alaf 5 of them ndo wenye uwezo dah si bora mm nina watu 49 na sina ninaemtarajia zaidi ya ushauri hamasa na kupeana ideas kipi kifanyike wapi bas na hapo bado wale wasio kua na muda na mm nafuta namba zao mfano mtu unamcheki leo ili muweze shauriana jambo anakujibu kesho au kesho kutwa ndo mambo siyatak hayo
 
Back
Top Bottom