Nafasi ya Tanzania katika uchumi wa Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi ya Tanzania katika uchumi wa Dunia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Stuxnet, May 10, 2011.

 1. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wakuu hii imekaaje? Pamoja na hali mbaya ya uchumi inayowakabili watanzania lakini bado kimataifa tuko vizuri kwa vigezo vya IMF. Katika nchi 25 za mwisho inaonekana Tanzania tuko juu ya nchi kama DRC na Uganda ingawaje tunapitwa na jirani zetu wa Kenya pamoja na nchi ya Raisi king'ang'anizi Mugabe. Takwimu hizi ni za 2010 kutoka kwenye chanzo kifuatacho List of countries by GDP (nominal) per capita - Wikipedia, the free encyclopedia

  RankCountryUS$152 Kenya809153 Comoros802154 Chad768155 Tajikistan741156 Burma702157 Mali692158 Benin689159 Haiti673160 Bangladesh638161 Gambia, The617162 Burkina Faso598163 Zimbabwe594164 Timor-Leste588165 Rwanda562166 Nepal562167 Tanzania548168 Afghanistan517169 Guinea-Bissau509170 Uganda501171 Togo459172 Mozambique458173 Guinea448174 Central African Republic436175 Eritrea398176 Madagascar392177 Niger381178 Ethiopia350179 Sierra Leone326180 Malawi322181 Liberia226182 Congo, Democratic Republic of the186183 Burundi180
   
 2. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Mzazi...kuwa namba Kumi kati 25 wa mwisho sio kitu cha kujivunia...kuwa namba 50 kati ya 100 wa kwanza...tungejivuna sio hiki..bado chini sana...acha kujilinganisha na nchi changa tukijivuni tumewapita...tukifanya hivo hatutaenda mbele
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli maendeleo bongo yatachukua muda sana kuja... yaani tunajisifu kuwa kwenye 25 za mwisho!!!
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  potential ya kuwa juu tunayo sana compared na nchi zingine zilizo juu yetu,,,corruption na bad politicking/leadership are key sources of our economic demise
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kila kitu au stage za mafanikio huenda kwa hatua, hauwezi uchumi ukapanda tu at par lazimi upande taratibu na hivyo Tanzania hatua ya kwanza kuchukua ni kuhakisha inapanda katika hio list ya underdeveloped countries, ikitoka hapo tena ipande stage nyingine vivyo hivyo. Kitu cha kuobserve hapa ni Tanzania imekaa katika hio nafasi kwa mda gani, ndio inawezekana katika list inaonekana ahuweni, lakini kama miaka inaenda bado tupo hapo hapo - ndo tatizo ambalo inabidi tulitaakari...
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna observations mbili zingine; Rwanda ambayo waliuana miaka 17 iliyopita kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe wako juu yetu kwa nafasi 2 halafu hawana raslimali aslia Kama sisi. DRC ya Joseph Kabila yenye kila utajiri ni ya pili toka mwisho. Je hii ni laana au ni kukosa viongozi wenye vision ya maendeleo?
   
 7. i411

  i411 JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  hizi takwimu za IMF na Wold bank wote wahunii tuu ndo wanatudidimiza tumebanana nao tokea tumepata uhuru wametupa madeni tuu. Sasa kazi yetu imekuwa kukopa na kulipa madeni tuu
   
 8. i411

  i411 JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  DRC imeandamwa na mavita kwa miaka kazaa kwa vile kunawatu wanafaidika kwa madini bila kulipa maushuru. rwanda ni kanchi kadogo sawa tu na kama kajiji ketu ka arusha uwezi kulinganisha na bongo zima lakini raisi wao yupu makini pia hataki upuuzi anaendesha hiyo nchi kiubavu ubavu anataka maendeleo tuu. Lakini nazani hawa wold bank na IMF wataenda kutega ile mitego yao ili Rwanda waingie kwenye ule mtego wa madeni lasivyo utasikia vita karibuni hapo tena.
   
 9. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Hii Listi Haswaa sio ngeni, kila miaka mitano au kumi maendeleo ya kila nchi Afrika inatolewa na kuwa compared, haijaanza leo, huwezi kujua tumekuwa katika hiilisti kwa muda gani kwasababu hujafuatalia, suala la kwamba tukifika hatua ya kumi tunajipongeza wakati tuna hatua 1000 zimebaki haileti maana, fika hatua ya 100 jua kuna hatua 900 zimebaki ndo ujipongeze...
  Ni kama mtoto wa Darasa la saba ambaye kati ya watoto wa mwisho wa 25..yeye ndo wakumi...je wazazi wake wampongeze na kumwambia eti..tuangalie yuko kwenye hio listi miaka mingapi?wakati yuko darasa la saba na ana kila kitabu kinachohitajika kwa maendeleo yake...tuangalia mpaka lini na toka lini... Miaka mingapi tumekuwa least developing countries..sasa niambie..tunagalie mpaka lini? Tuipe miaka kumi Mingine? Ili Wazungu walinunue shamba zima la Tanzania?
   
 10. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kumfaidi **** msifie. Ndo wazungu wanavyotufanya. Wakisema hivi basi sisi tunavimba vichwa.
   
 11. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na ww Seniorita kuna ukweli kuwa baada ya uhuru Wa Tanzania hadi mwaka 1967 GNP per capita ya nchi yetu ilikuwa sawa kabisa na ya Malaysia na Indonesia. Kwa kumbukumbu za IMF za mwaka Jana rank ya Malaysia ni 65 wakati ya Indonesia ni 109 na sisi Tanzania ni 167. Nini kifanyike angalao tujinasue hapa tulipokutana kwa nafasi 10 tu yaani tufike namba 157
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Stuxnet I don't believe tuna audacity ya kuita kushindwa au umasikini wa nchi zetu ni laana... Tukifanya hivyo hatutakuja kunyanyuka na tutabweteka.. Katika nchi hizi zinazoendelea matatizo kuja isha itachukua miaka mingi kutokana na ukweli wa hali halisi ulivyo, NDIO raisi anaweza kua na nia nzuri na malengo ya nchi but kwa upana yeye si mtendaji ana delegate tu... Uki observe saana kwa nature ya sisi wananchi/wanajamii tulivyo na sio Tanzania tu hata nchi jirani na maskini wenzetu, unaweza kuta labda aje kiongozi mzuri na dictator for maybe kama 20 years hivi then maybe hatua fulani yaweza pigwa...NAJUA kuwa wengi mtasema nini naongea na kwamba am out of my senses but ukweli unabaki watanzania sio wazalendo hata kidogo... Mfano mdogo uwezi fananisha Mkenya anavyo thamini inchi yake kama Mtanzania anavyothamini inchi yake...Kuongoza na kufanya kazi na watu wasio thamini inchi zao huwezi endelea hata siku moja maana kila mmoja yuko kwa manufaa ya kwake na si ya wanachi... Tanzania hata umuchukue mwananchi mwenye focus ya Tanzania inahitaji nini wanajamii wapate afueni, akipata pesa ya kutosha - anatoka nje ya nchi mara moja moja; s/he is no longer interested na wewe kapuku!!! (sorry off topic kidogo so you know where its coming from)

  Ruanda.... Niseme nini kuhusu Ruanda ambalo wote wenye interest in it hawajui??? Ni kweli ni nchi ndogo yenye raslimali ndogo compared to DRC na Tanzania pia - but that country's president. Kagame yuko focused na anataka ahakikishe inchi yake inanyanyuka Politically na Economically ingawa the former imekua ni shida kidogo kuliwezesha. Anataka hilo na anafanya kwa vitendo si maneno (anajenga mashule, kuangalia miundo mbinu, kusimamia na kuhakikisha wana benefit toka kwa wawekezaji, anafuatilia sana HIV/AIDS na jinsi inavyoathiri nguvu kazi etc ... Ni aibu kusema kweli na sijui viongozi wetu wanalichuliaje an wanajifunza nini kwa Kagame. Shida sasa ni ile mambo ya Democracy, I believe for Ruanda to prosper Kageme should be in it for a long haul; but is it going to be that simple in a nation where the civil wars led to a scar from the 1994 genocide as a result of ukabila... What ever the case at least Ruanda's future looks prosperous compared to others...

  Na DRC nashindwa niongee nini kuhusu wao maana infor zao kuhusu matatizo, vita vya wenyewe kwa wenyewe, corruption, jinsi gani raslimali zao hawazifaidi wala hawajui zinatumika vipi; waweza publish kitabu.....
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Selwa naona umeninukuu sawa but umenielewa vibaya... Maana yangu ilikua kwamba Tanzania ili iweza fanikiwa ni lazima ishike nafasi ya juu katika hio list ya nchi 25.. hatuwezi tukaanza kuongelea yenyewe TZ kua katika 50 bora kati ya mia na hali the reality ni kua tuko katika hio list mbovu... Hivyo basi mimi kuzungumza hivyo sina maana nafurahia iko nafasi ya kumi NO! sifurahiiii... Na sifurahi kabisa kua iko hata katika hio list. Na kuwekea kipande ambacho naona hukuzingatia wakati una ni nukuu;
  Kitu cha kuobserve hapa ni Tanzania imekaa katika hio nafasi kwa mda gani, ndio inawezekana katika list inaonekana ahuweni, lakini kama miaka inaenda bado tupo hapo hapo - ndo tatizo ambalo inabidi tulitaakari...
  Hivyo basi kama umenielewa saizi utangudua uzungumzayo kuhusu kila siku kuwa hapo nakubaliana nalo na ndo maana kwa perspective yangu niliona kua ni muhimu zaidi tukazingatia hio statement na kazi yetu kubwa ni kufanyinyia kazi au kutoa maoni kwa kuzingatia hapo nilopoweka rangi nyekundu. Selwa, nimekujibu sawa au bado una walakini???
   
 14. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  **** bana..... Msifie tu hata kama amekuwa wa mwisho anaridhika.....haya bana
   
 15. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Haswaa Umenijibu, Hasira za maendeleo duni inanisumbua sana...wajua huku kwetu tunaangalia nchi kwa microscope!
   
 16. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Asha D, Hayati baba Taifa Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji mambo manne; (1) Watu (2) ardhi (3) siasa safi na (4) uongozi bora. Je inawezekana kuna vitu vingine ambavyo Mwalimu alisahau kuvitaja ndiyo vinafanya tusiwe na maendeleo mpaka Leo hii?
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Naamini alitaja vyoote vya muhimu saana, tofauti imekua kua maana yake inabadilika tokana na hali na ulimwengu tuliopo saizi - naamini kuna vipengele kama cha watu kiwe watu wazalendo... au Uongozi bora ni mtihani ukitaka uingie saana mana nayo ni relative term.. Upande wa siasa, Stuxnet katika siasa zote nilizo wahi soma katika vitabu vya historia hakuna siasa safi... Kama tu enzi za utawala wa Roman catholic there hands were stained with blood sembuse utawala wa ki capitalist, communist au kifalme?? Kitu cha muhimu katika mtazamo wangu ni Elimu, watu wakiwa robo tu katika inchi wameelimika twaweza fika mbali, na naomba utofautishe kati ya watu walosoma saana degree kumi kidogo na mtu alosoma hata degree mbili but kaelimika... Kwa Tanzania si wasomi woote wameelimika... Inasikitisha...
   
 18. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,057
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Sasa wewe ulieleta maudhui hii unaisifu Tanzania kwa kupitwa na nchi kama Comoro, Chad, Burkina Fasso, Gambia,Bangladesh, Rwanda nk? Kweli wewe unaijua Tanzania na potential iliyonayo?
  Hapo ungelia rafiki yangu kwani nchi zote hizo nilizozitaja zikijumuishwa hazina rasilimali kama Tanzania, yes, kwa ujumla wao wote. Kweli Tanzania tuna safari ndefu!
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mi mwenyewe nimeshangaa nikafikiri labda tupo 25 bora za mwanzo kumbe za mwisho.
  Resources nyingi kuliko akili. Labda tungenyimwa hizi resources kama nchi zingine tungekuwa na akili za kimaendeleo.
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hapo ume exaggerate saana Sijali, ndio Tanzania ina rasilimali nyingi... But kwamba ni nyingi ukiunganisha Comoro, Chad, Burkina Fasso, Gambia, Bangaladesh.... alafu hapo hapo nakadhalika... Sijali tafadhali naomba fuatilia rasilimali ya hizi inchi ndo ufananishe. Ukitaka kufananisha fananisha tu jirani yetu hapa wa Ruanda uone jinsi Kagame anavyofanya kazi, Hiyo inchi ndogo tena imekumbana na matatizo yalioacha kovu ambalo halitakuja futika katika historia lakini kamshinda nafasi mbili Tanzania the so called inchi ya amani....
   
Loading...