Nafasi ya kazi (House Manager)

nguzo1

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
349
535
Terups Familly Wanayofuraha kutangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo

1) HOUSE MANAGER ( Nafasi 3)

SIFA ZA MWOMBAJI

-> Awe jinsia ya kike na awe Amesomea MAPISHI au.
Food&Beverage Production Au Hotel Management
na kuhitimu kwenye chuo kinachotambulika kwa.
ngazi ya Cheti au Diploma

-> Awe na Elimu ya Computer Basics

-> Awe na umri kati ya Miaka 18 hadi 21. Awe na urefu Usiopungia Sentimita 170 (5.5ft).

-> Asiwe mnene awe msafi kupitiliza na mwenye
kujipenda awe na afya njema (H.I.V negative)

-> Awe mwaminifu, mkweli mchangamfu na Mwenye hofu ya Mungu na asiwe na mtoto wa kumzaa

-> Awe mvumilivu na awe tayari kufanya kazi kwenye mazingira tofautitofauti na awe mwepesi kujifunza kitu kipya.

MAJUKUMU YA KAZI

-> Kuandaa chakula
-> Usafi wa ndani ya nyumba
-> Mengineyo (kwa kadri yatakavyojitokeza)

KITUO CHA KAZI
>>Kituo cha kazi ni Dar es Salaam ila awe tayari kwa mabadiliko endapo yatatokea

MALIPO / MSHAHARA

-> Malazi na chakula ni bure na kuhusu mshahara Ni Mazungumzo na pia itatengemea na Utendaji wa kazi

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

>> Barua ya Maombi na Wasifu wako (CV) itumwe kwa njia ya E-mail nikota166@gmail.com

*Mwisho wa kutuma maombi Ni Tarehe 30/12/2020 *
 
"Awe negative" kwenye mambo ya upishi anatumia visu,machines na vingine vyenye ncha kali hivyo ni muhimu akawa HIV negative kwa usalama wa familia kwa ujumla.

"Kupika na Mengineyo..." kuna kigezo cha Computer nimweka hapo Computer works ni mojawapo ya mengineyo.

Karibu
Awe negative na majukumu ya kazi ni kupika na mengineyo kadili yatavyojitokeza. Sema unatafuta mke tu kwani shida iko wapi.
 
Nahisi utapeli kwenye hii kazi kwenye hiyo deadline , najiuliza maswali mengi sana nikizingatia aina ya kazi
 
Nahisi utapeli kwenye hii kazi kwenye hiyo deadline , najiuliza maswali mengi sana nikizingatia aina ya kazi
Hatuna Uhitaji wa haraka Kwani hata hivyo baadhi ya miundombinu inatarajiwa kukamilika December 2020.

Wasiwasi ndio akili ila Mara nyingi jaribu kuwa na "mtizamo Chanya" (Positive mind) itakusaidia kufanikisha mipango yako kiurahisi.
 
Kama hamna uhitaji wa haraka kwa Nini mmetangaza sasahivi?
Wakati watu waliosomea hizo fani wapo wengi sana.
Halafu mnategemea huyo mtu aanze kazi lini.
Na mwisho kwa ushauri tu sheria zetu za kazi zinakataza kumbagua mtu kwa HIV status yake ulivyoiweka kwenye tangazo lako Ni kinyume cha sheria
Waajiri wanawapima watumishi watarajiwa ukimwi kiuficho wanaenda kuwapima afya Mambo ya uzito,kuona , homa ya ini na ukimwi majibu mfanyakazi hupewi mwajiri anayachukua na kuyafanyia kazi bila muomba kazi kujua mtu anaambiwa hajafauli usaili bila kuambiwa sababu kumbe Ni HIV positive, kiutaratibu huwezi kumwambia mtu umefeli usaili wa kazi kwa sababu wewe Ni hiv postive angalia usije shtakiwa
 
Terups Familly Wanayofuraha kutangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo

1) HOUSE MANAGER ( Nafasi 3)

SIFA ZA MWOMBAJI

-> Awe jinsia ya kike na awe Amesomea MAPISHI au.
Food&Beverage Production Au Hotel Management
na kuhitimu kwenye chuo kinachotambulika kwa.
ngazi ya Cheti au Diploma

-> Awe na Elimu ya Computer Basics

-> Awe na umri kati ya Miaka 18 hadi 21. Awe na urefu Usiopungia Sentimita 170 (5.5ft).

-> Asiwe mnene awe msafi kupitiliza na mwenye
kujipenda awe na afya njema (H.I.V negative)

-> Awe mwaminifu, mkweli mchangamfu na Mwenye hofu ya Mungu na asiwe na mtoto wa kumzaa

-> Awe mvumilivu na awe tayari kufanya kazi kwenye mazingira tofautitofauti na awe mwepesi kujifunza kitu kipya.

MAJUKUMU YA KAZI

-> Kuandaa chakula
-> Usafi wa ndani ya nyumba
-> Mengineyo (kwa kadri yatakavyojitokeza)

KITUO CHA KAZI
>>Kituo cha kazi ni Dar es Salaam ila awe tayari kwa mabadiliko endapo yatatokea

MALIPO / MSHAHARA

-> Malazi na chakula ni bure na kuhusu mshahara Ni Mazungumzo na pia itatengemea na Utendaji wa kazi

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

>> Barua ya Maombi na Wasifu wako (CV) itumwe kwa njia ya E-mail nikota166@gmail.com

*Mwisho wa kutuma maombi Ni Tarehe 30/12/2020 *
Unataka House girl anayetoka chuo Ooh
 
We jamaa hapana aisee. Awe HIV negative na awe mrefu 170cm. Unatumia kigezo gani kutafuta muhudumu wa nyumbani kwa urefu?

Unatafuta mengine wewe sio uhudumu
 
Kama hamna uhitaji wa haraka kwa Nini mmetangaza sasahivi?
Wakati watu waliosomea hizo fani wapo wengi sana.
Halafu mnategemea huyo mtu aanze kazi lini.
Na mwisho kwa ushauri tu sheria zetu za kazi zinakataza kumbagua mtu kwa HIV status yake ulivyoiweka kwenye tangazo lako Ni kinyume cha sheria
Waajiri wanawapima watumishi watarajiwa ukimwi kiuficho wanaenda kuwapima afya Mambo ya uzito,kuona , homa ya ini na ukimwi majibu mfanyakazi hupewi mwajiri anayachukua na kuyafanyia kazi bila muomba kazi kujua mtu anaambiwa hajafauli usaili bila kuambiwa sababu kumbe Ni HIV positive, kiutaratibu huwezi kumwambia mtu umefeli usaili wa kazi kwa sababu wewe Ni hiv postive angalia usije shtakiwa
HIV Ni ugonjwa kama magonjwa mengine na pia kuna kazi nyingi tu ambazo kunakuwa na vigezo vya afya mfano kazi zingine hazihitaji watu wasiokuwa na Pressure, Pumu au ulemavu wa mcho au usikivu na mengineyo kwahiyo siyo ubaguzi bali tu ni Nature ya kazi.

"Kuwapima Afya wafanyakazi kwa KIFICHO" Sina uhakika kwa upande wa sheria za kazi but kwa mtizamo wangu naona Kuwapima afya iwe hadharani na majibu ndiyo yanakuwa KIFICHO/ Confidential.

Sioni tatizo la kucha wazi Dirisha la maombi ya kazi kwa miezi miwili ila lengo lilikuwa ni kumpata mtu sahihi na bora zaidi.

Asante kwa ushauri wako nitafuatilia zaidi ili nijue zaidi kuhusu mambo ya afya ya mwajiriwa
 
We jamaa hapana aisee. Awe HIV negative na awe mrefu 170cm. Unatumia kigezo gani kutafuta muhudumu wa nyumbani kwa urefu?

Unatafuta mengine wewe sio uhudumu
Vigezo vimewekwa kwa kufuata mazingira ya kazi ndugu hakuna la ziada.
 
Na asiwe na mtoto wa kumzaa, ww unatafuta mke
Ningeweka Tangazo la kutafuta mke na mojawapo ya vigezo ikawa ni ajue kupika kitaalam ungesema natafuta Housegirl... Anyway ndio binadam tulivyo.
 
"asiwe mnene, awe msafi kupitiliza, hofu ya mungu, HIV negative, urefu cm..." Wewe nguzo1 acha mambo yako hayo bhana, washirikishe ndugu wakusaidie hilo hitaji la msingi kama huwezi kusort mwenyewe!
 
Unataka House girl anayetoka chuo Ooh
Sioni tatizo kama atalipwa vizuri na atatimiza majukumu yake ipasavyo.

Sisi kama watanzania tubadilike jamani huku mtaani tunaishi na wataalam wengi wa kila fani na wengi wao hawana kazi. Kwa uzoefu wangu nimegundua kuna faida nyingi unapotumia wataalam kwenye shuhuli zako kwani unaokoa garama na kuboresha ufanisi wa kazi zako.

Mtaani kuna Madaktari, wanasheria, Enginineers, Archtect, Mechanics,Plumbers, Teachers na wengine wengi tu ambao wengi wao ni Graduates na hawana kazi na wako tayari kujitolea/kutoa ushauri wa bei nafuu na hata kufanya kazi kwa commission kama hutaweza kuwaajiri Its time to use them.

Nchi zingine kama Nigeria,India,China wana cheap labour na wengi wao wamesoma sana. Mfano India kuna huduma bora na nafuu za afya kwa sababu wataalam wako wengi na vifaa tiba pia viko vingi kwaiyo unakuta ni rahisi kwa familia kuwa na daktari wao (wawili au hata watatu) tena specialist.

Labda hebu nipe maoni yako kwanini umeshtuka kusikia Anahitajika house helper mwenye elimu ya chuo? Tena Certificate au diploma in Nutrition/Food & Beverage production Pamoja na computer skills?
 
"asiwe mnene, awe msafi kupitiliza, hofu ya mungu, HIV negative, urefu cm..." Wewe nguzo1 acha mambo yako hayo bhana, washirikishe ndugu wakusaidie hilo hitaji la msingi kama huwezi kusort mwenyewe!
Asante kwa Maoni yako ila tu jua kwamba kwenye familia suala la Maadili ya watoto na afya ya familia kwa ujumla ni swala nyeti sana pia hiyo nafasi tunayowapa Wasaidizi wetu wa ndani ni nafasi nyeti na inahitaji iheshimiwe sana.

Kuna majirani zangu Wapo bize 24/7 muda mwingi watoto wanashinda na Dada wa kazi hadi watoto wanampenda Dada wa kazi kuliko wazazi wao na amewafundisha lugha yao wanaongea vizuri kuliko lugha ya wazazi sasa kama Dada wa kazi hana maadili au mtizamo chanya juu ya malezi ya mtoto mwisho wa siku mtoto anakosa malezi bora.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom