Nafasi ya kazi (House Manager)

hana lolote huyo,..
Naona umeshtuka sana kuona 170 Centimeter minimum height.

Iyo 170Cm ni kwa ajili ya kuchukua ama kuweka glass kwenye hizo kabati za juu (Picha imeambatanishwa) bila kuvunja . Sasa hiyo ni sababu mojawapo tu sioni cha kushangaza hapo.
IMG_20201016_211836_389.jpeg
 
Sioni tatizo kama atalipwa vizuri na atatimiza majukumu yake ipasavyo.

Sisi kama watanzania tubadilike jamani huku mtaani tunaishi na wataalam wengi wa kila fani na wengi wao hawana kazi. Kwa uzoefu wangu nimegundua kuna faida nyingi unapotumia wataalam kwenye shuhuli zako kwani unaokoa garama na kuboresha ufanisi wa kazi zako.

Mtaani kuna Madaktari, wanasheria, Enginineers, Archtect, Mechanics,Plumbers, Teachers na wengine wengi tu ambao wengi wao ni Graduates na hawana kazi na wako tayari kujitolea/kutoa ushauri wa bei nafuu na hata kufanya kazi kwa commission kama hutaweza kuwaajiri Its time to use them.

Nchi zingine kama Nigeria,India,China wana cheap labour na wengi wao wamesoma sana. Mfano India kuna huduma bora na nafuu za afya kwa sababu wataalam wako wengi na vifaa tiba pia viko vingi kwaiyo unakuta ni rahisi kwa familia kuwa na daktari wao (wawili au hata watatu) tena specialist.

Labda hebu nipe maoni yako kwanini umeshtuka kusikia Anahitajika house helper mwenye elimu ya chuo? Tena Certificate au diploma in Nutrition/Food & Beverage production Pamoja na computer skills?
Tulichozoea kwa hizo kazi hapa kwetub hazina malipo makubwa ya mtu kuweza kusogeza maisha yake ipasavyo hubaki kuelelewa na mwajiri wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom