Nafasi Kazi za Uhamiaji (2014) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi Kazi za Uhamiaji (2014)

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Tmajuto, Feb 14, 2014.

 1. Tmajuto

  Tmajuto JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2014
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kamishna Mkuu wa idara ya Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwenye vyeo vya Koplo na Konstebo wa uhamiaji.

  A: MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI NAFASI 70

  1. SIFAZINAZOHITAJIKA

  Awe na shahada ya kwanza au Stashahada ya juu kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikalikatika fani zifuatazo; Sheria, Uchumi, Biashara,
  Utawala, Uandishi wa habari, Ualimu, Usafirishaji, Rasilimali watu, Sayansi ya kompyuta, Teknolojia ya mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi majengo na Uhandisi Mitambo. Awe na umri usiozidi miaka 35

  2. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA

  (i) Kusimamia doria sehemu za mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.

  (ii) Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa hati ya mashitaka na kuendesha mashitaka.

  (iii) Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya hati za uhamiaji

  (iv) kufanya ukaguzi wa mwanzo wa maombi mbalimbali

  (v) kupokea na kukagua hati za safari, fomu ya kuingia na kutoka nchini.

  (vi) kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za uhamiaji kwa wanaostahili

  (vii) kuagiza ufunguaji wa majalada ya watumiaji

  (viii) kutunza kumbukumbu za ruhusa kwa wanaongia na kutoka nchini

  (ix) kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za uhamiaji na uraia

  (x) Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa

  B. KOPLO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)

  1. SIFA ZINAZOHITAJIKA


  (i) Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu

  (ii) Awe na umri usiozidi miaka 30

  C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)

  1. SIFA ZINAZOHITAJIKA

  (i) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu

  (ii) Awe na umri usiozidi miaka 25

  D. SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI

  (i) Cheti cha ufundi stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya umeme na mitambo.

  (iii) Cheti au Stashahada ya Uhazili (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) katika chuo kinachotambulika na Serikalì.

  (iv) Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statistics) kutoka chuo kinachotambuliwana Serikali.

  (v) Cheti au Stashahadayavyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operation) kutoka katika Chuo kinachotambulika
  na Serikali.

  (vi) Cheti au Stashada katika fani ya uchapaji (Printing)

  (vii) Ujuzi na elimu ya kompyuta na uandishi mzuri utazingatiwa.

  E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA

  (i) Kufungua, kupanga na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma za Uhamiaji.

  (ii) Kuandika Hati mbalĂ­mbaLi za Ubamiaji

  (iii) Kufanya Doria schcme za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwcmo vya
  majini.

  (iv) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini (Deporters). Kufanya ukaguzi kwcnye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara.

  (vi) Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji.

  (vii)Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji.  F: MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATANISHO VIFUATAVYO.

  (i) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masonia kwa mujibu wa sifa zilizotajwa.

  (ii) Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi

  (iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa

  (iv) Picha mbili (passport size)

  (v) Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa.

  G: UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

  Maombi yote yapite posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.

  (i) Maombi ya nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji yatumwe kwa;

  KATIBU MKUU,
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
  S.L.P 9223,
  DAR ES SALAAM

  (ii) Maombi ya nafasi ya Koplo wa uhamiaji na konstebo wa uhamiaji yatumwe kwa;

  KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
  S.L.P 512,
  DAR ES SALAAM

  Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27/02/2014 kwa nafasi zote.
   
 2. Tmajuto

  Tmajuto JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2014
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mie nimewasilisha tu
   
 3. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2014
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,362
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kesho ntaanza mchakato wa ku Apply ! Hivi kwa Koplo anachukua kama ngapi kwa mwezi ?
   
 4. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,899
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  ahsante sana mkuu!!!!!

  naona valentine imeniamkia vyema!

  naanza kuapply kesho!
   
 5. chanakeshava

  chanakeshava New Member

  #5
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 7, 2014
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Lol afashali
   
 6. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2014
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mungu akubariki Dkt Jakaya Kikwete kwa kumwaga Ajira hapa nchini.
   
 7. abbaczo

  abbaczo JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2014
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,448
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hawa nao kama pccb washatuengua wengine hapo kwenye vyeti vya dalasa la saba.
   
 8. abbaczo

  abbaczo JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2014
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,448
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  mkuu una cheti cha dalasa la saba.?
   
 9. d

  dtv Member

  #9
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chet cha darasa la saba sina jamani nifanyeje
   
 10. m

  msnajo JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,326
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata hujajua hatima umeshataka kujua mshahara?! Kazi kwanza, mshahara baadae. Hizi ni kazi za uzalendo na kijitolea mkuu
   
 11. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,899
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  kitoke wapi?

  nina form 4 form 6 na chuo tu!

  ila kuapply ni lazima! hii fursa ikinipita ntajuta!
   
 12. mzungu pori

  mzungu pori JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2014
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cheti cha darasa la saba uhamiaji 2taxamehana
   
 13. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 17,537
  Likes Received: 7,760
  Trophy Points: 280
  mkuu wangu Excel
  kumbe huna kazi? mbona hukunambia?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,899
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  !!!

  niko tu hapa nasikilizia hizo post tuanze kuzihangaikia!
   
 15. Honey Faith

  Honey Faith JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2014
  Joined: Aug 21, 2013
  Messages: 15,860
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hebu msaidie basi apate kazi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 17,537
  Likes Received: 7,760
  Trophy Points: 280
  hatukujuana mapema

  TAKUKURU nimepeleka wawili

  halafu mbona huku return back? ha ha ha mkuu wewe!!
   
 17. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 17,537
  Likes Received: 7,760
  Trophy Points: 280
  sina access na uhamiaji ingekuwa TAKUKURU angekuwa anasubiri kuripoti tuu
   
 18. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,899
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  usijali mkuu tuko pamoja!

  sikureturn back nini lakini?
   
 19. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,899
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  thanks honey faith for your touch...
   
 20. Honey Faith

  Honey Faith JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2014
  Joined: Aug 21, 2013
  Messages: 15,860
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Basi umkumbuke siku mkiitaji tena watu
   
Loading...