Nafasi 2 za kazi-Kama una mdhamini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi 2 za kazi-Kama una mdhamini.

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by rakeyescarl, Apr 2, 2011.

 1. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wadau,
  Tunazo nafasi 2 kwa wa Tz wa kuzaliwa.
  Hamna vyeti vinavyotakiwa ili mradi uwe na nguvu za kutosha na afya ya kutosha.
  1.Kazi ya kwanza ni kuuza Mpesa,kusafirisha mizigo na kupokea mizigo.
  Mshahara 90Elfu,nyumba bure,kitanda bure-hii iko Njombe.
  2.Kutumwa kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 na nusu jioni madukani.
  Mshahara elfu 90,nyumba bure. Hii ni kazi nzuri kwa sababu utakuwa ukipata posho kutoka kwa jamaa unaonunua kwao vitu kila siku si chini 5elfu.
  Tuma ujumbe kwa rakeyescarl@yahoo.ie au hapa.
  Kazi zote hizo lazima uwe na wadhamini 3 wa si chini ya milioni 50 au mwenye nyumba,mfanyakazi wa serikali kama polisi etc,kama unahitaji maelezo ya ziada uliza
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Mshahara elfu 90, nyumba na kitanda ni bure. Inabidi niwe na afya na nguvu hivyo nitahitaji kula vizuri.
  Kwahiyo mlo kwa siku ni 90,000/30= 3000. Kwa siku nitakuwa nakula elf 3. Naasume sitooga wala kufua kwahiyo gharama ya sabuni hakuna pia sitoumwa....
  Wadhamini 3, total ya mali zao ziwe 150million.....!
  Mkuu hapa nawaza tuuu, nimeona niandike ninavyowaza ili baadae niyapitie tena.
   
 3. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nahisi kama umekurupuka hivi mkuu.
  Wadhamini 3 wenye fixed asset zisiyopungua 50 ml @ wamdhamini mtu anaekwenda kulipwa mshahara wa sh.90 elfu per month?Imekaaje hii?eenhee!!! tena mwenye nguvu bila shaka awe na akili timamu weee!! ogopa hii mambo usije tafuta mazingira ya kuibiwa wewe mkuu.

  Nimekusoma katika sura mbili (1) Hujajua mambo ya kuzingatia unapo hitaji mfanyakazi kuanzia hadhi ya office yake hadi mahitaji yake ya msingi afya yake uthamani wa mali yako mwenyewe.
  Just imagine we usimamie zaidi ya sh 50ml then uje ulipwe elfu 90 kwa mwezi?Kama sio majaribu ni nini hii?Ushauri_Tafuta wataalamu wa uchumi uzungumze nao kuhusu kile unachokifikiria naamini watakushauri vizuri tu.

  (2)Yawezekana huna mzunguko mkubwa wakukufanya uwe na uwezo wa kuajiri na kumlipa mfanyakazi kwa kadri ya hali ya uchumi ilivyo ila basi wenge tu- Ushauri _kazakaza kwanza mwenyewe ukishafikia hatua ya kumudu utafanya hivyo acha udunya otherwise kaka dada mtoto wa mamdogo ndio msaada sana katika hili.

  Hitimisho;_Hao wadhamini 3 nao watakua na matatizo ya kufikiri kama kweli wanaamini kijana wao (anasifa stahiki) anaakili timamu na afya yakutosha na wakashindwa kumsaidia wao kama wao.

  Anyway ku edit si inaruhusiwa unaweza kufanya hivyo inawezekana una nia njema tu mkuu.
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Sina kazi lakini hii hapana aisee kha!!!!
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mil 50 kwa mshahara elfu 90 kwa mwezi, TAFUTA FREELANCERS WAKUIBIE. Weka strategies za kueleweka unapo-implement biashara,, TIGO PESA (TP), M-PESA, ZAP hizi zinamzunguko mkubwa na zahitaji mtaji maridhawa, TAFUTA WATAALAM WAKUSHAURI VINGINEVYO UTADONDOKA KIBIASHARA.
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  mmmh hayo masharti na huo mshahara hata haviendani? hata msaidizi wa ndani siku hizi wanalipwa zaidi ya hiyo

  90000/=!!!! are u kiddin me?:faint:
   
 7. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kuna kila dalili mtoa mada hana hana ajira ila ni bepari aliyezowea kusulubu binadamu wenzie wasio na ukwasi. Wapo wengi hawa jamani.
   
 8. e

  eliyap1 Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hujui unalo lifanya mjomba
   
 9. M

  Mutu JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  90,000madafu mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 10. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I personally,do appreciate your efforts and good intention(probably)of helping others. But this amount of sallary/allowance or whatever you call it is insurficient depending on many factors one of them being Tshs daily flactuation status. Economic crisis not accounted for,not saying on tax additions or incliment on bus /transpot fair/prices in general. Have you ever had it in your good mind that this pariticular person will have to eat,have some medical care, and saving for future? Does that 90 cover all that?
  Come to this guarantors fact: If they ca have those assets,50 mil. valued, Why wouldn't they(for Gods sake)help this person themselves? Why would they want to just give you a service man?
  What about your security? Nahisi huyu mtu atahusika na makusanyo makubwa thats why thamana ni kubwa! Huoni ni hatari kumpa kazi hiyo mtu ambaye atakuwa na uhitaji wa pesa always kutokana na malipo duni?
  Tuache hizi tabia za kikoloni. Hivi bado kuna watu wanaamini kuwa tuliwakataa wakoloni kwa sababu ni weupe? Tuliwakataa kwa sababu ni wanyonyaji! And there you are unafanya yaleyale. Bad enough hapa unahatatrisha na huo mtaji wako ambao mi sijui ulifanya nini mpaka ukaupata.
  Ushauri
  Tafuta wataalam husika wakueleweshe ni lini mtu alipwe nini ili awe mfanyakazi wa kutegemewa.
  Usifikirie kile tu unachotaka kupata angalia na wanaokuzunguka! Usitegemee amani sana kama utakuwa umeshiba wewe wakati wanaokuzunguka wana njaa kali!
  Thanks
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Fanya mwenyewe ku**mako
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  naona haka kabosi kameyeyuka..
   
 13. m

  mbweta JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kazi kama hyo ya f90 utampata mwana jf kweli. Mda wa kuja jf atapata sa ngap?
   
 14. Dadii

  Dadii Senior Member

  #14
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimepata wazamini......nakuja njombe,,,, nipande gari gani? kiswele?
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  elf 90???? C bora kuendlea kula ugal wa shkamoo! Mashart na Mshahara hata haviendani! Hta km ktnda ni bure, kwn nan kakwmbia sshv 2nalpa ktnda?
   
 16. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Doooh mpaka matusi nimepata,anyway ndio JF wamo wa aina zote. Naomba nijibu kama ifuatavyo.
  1)90,000 Salary-jamani si nimeweka kiwango ambacho kinawezekana kupatikana?Ni bora mtu aibe/aniibie kuliko kum guarantee ambacho sikiwezi.
  Kama ninachopata mimi ni 100,000 kwanini nitoe /niahidi nisichokiweza?
  2)Walionibeza kuwa house girls wanapata 90,000pm ni wapi huko? wapo watu wako tayari kufanya kwa 45,000 na hawazipati hizo kazi.
  3)wadhamini wa 50M ?watu wengi hatujui thamani ya mtu, kwa mfano mtu anayefanya kazi serikalini ,yy kukupa udhamini ni kitambulisho chake tu,kina thamani zaidi ya hy pesa,Elly B naona umenielewa,mimi hapa ilikuwa ni kusaidia ndg zetu,shida ya watanzania wengi ni kujifanya tuko juuuu sisi na ndg zetu wote,hebu jiangalie hata kijijini kwenu au nyumba ya nyumba yako kuna Phd holders wangapi wanawadhulumu hata hy 30K pm ma house girls wao baada ya miaka 2/3 ya kazi?
  4)Dunia hii imekuwa mbaya kidogo ndio maana ni bora kwenda kwenda kwenye interview unajua mshahara wako kuliko kwenda usipojua utaanzia kiasi gani?
  Naomba mnisome vizuri,nimesema sihitaji vyeti wala qualifications za ajabu,maana yangu ni kuwasaidia watu wa hivi na nina imani katika haya maombi tuliyopata ya zaidi ya 60 mpaka sasa tutaweza kufanya kazi na hao 2. Hii ni kazi ya accord lakini huenda hawa watu wakawazidi wengi kwa kipato wanaobeza hapa baada ya miezi michache,Yes 90K ya uhakika lakini in few month wanaweza kuwa mbali.
  Nawashukuru wanaotaka nilipe consultants kwa ushauri,lakini sisi hizi kazi tukizifanya mwisho hawa staff wanaanza za kwao na tuko kwenye huu ulingo miaka 5 wanaotegemea kuwa tutaanguka nina diriki kusema hatuwezi kuanguka kwa sasa tuna uzoefu wa kutosha. AAprt from hiyo 90thou si wanapata na elimu kusudi wafanye ya kwao-nani na ni wapi wanaotoa elimu kama hii bure?
  Kama zipo kazi zinazolipa zaidi kuliko kutukana si bora tusaidiane wa TZ wenzangu,kuna watu wanakula ugali kwa baba huu mwaka wa 5 tuwasaidie wasije kuolewa wasipotaka.
  wa TZ TUSAIDIANE! NAWASHUKURU WOTE Wanaoendelea kutuma maombi na nayapeleka na kwa watu wengine walioniomba kama watakuwepo wa ziada, AHSANTENI!
   
 17. m

  mbenye Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bwanaaaa wewe
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Duuh...mpaka namuhurumia mtoa mada:embarrassed1:!
   
 19. duda

  duda Senior Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hauna ndugu zako kule kijijini kwenu? wapeleke na ukawaajiri, na ikiwezekana walipe hata elfu30, inaudhi sana kumtumikisha mwenzako masaa yote halafu unamlipa elfu90
   
 20. R

  Renegade JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa Upstairs hayuko vizuri. Anajifanya kujua na kudharau watu kwa sababu ya vipesa vyake, Ajira ngapi watu wanaajiriwa ku hande millions bila hata kuwa na Senti tano? Nini maana ya kuwa na Controls, Controls ipo kwa ajili ya kusafe Guard Asets za Biashara. Unapokuwa na mzunguko mkubwa wa pesa na unalipa mishahahara midogo si utaibiwa? Kuwa makini kidogo Acha mawazo ya kuexploit watu.
   
Loading...