Asante sana MkuuMpe uhuru na Muulize kama kuna chochote anachohitaji kutoka kwako ambacho anahisi kitamsaidia endapo kutatokea lolote, Mfano
Jina halisi, Kitambulisho, Namba zako nyingine, Sehemu unayoishi, Sehemu ya Kazi, sehemu ya biashara, picha n.k
Na wewe kama kweli unajiamini huna nia ovu, mpe...,
Ndio unahitaji mteja, ila pia epuka kumharakisha sana,
Asante sana MkuuOnline Business changamoto yake kubwa ni unapoanza kutafuta wateja waaminifu hii ni biashara unayoifanya na watu wasiojulikana,na kwakua wewe (muuzaji) humjui mteja hata mmoja inakupasa uingie ktk risk ambayo si risk kivileee ila n risk
wateja wa online hawaaminiki na ktk makosa watu wengi wa online huyafanya ni kuonyesha wasi wasi kwa mteja, au ile kutomuamini mteja ndio mana utaskia wakimwambia mteja ili tukutumie mzigo "lipia kwanza"
mteja humuamini ila wewe unataka akuamini alipie wakati hakujui (shenzi kabsa),ni kosa la jinai kumuonyesha mteja humuamini au una wasi wasi nae,sasa Utafanyaje ili usipoteze mzigo/bidha yako unayomtumia mteja usie mjua?
Umepata mteja wa Mwanza wewe muuzaji upo Tanga,chakufanya ongea na mteja wako vizuri kabisa,tumianeni picha za bidhaa anayotaka mteja mpk mfikiane muafaka,akisharidhika na kuafiki kapenda bidhaaa A mwambie Kesho utamtumia
Alipo,hapo hakikisha umeshaongea nae kuhusu gharama za usafirishaji mzigo + mzigo wenyewe Mkishakubaliana,wala usionyeshe kutaka hela kwa mteja wako,muonyeshe unamuamini 100% ila moyoni mwako imani nae ipo 0.5%,baada ya kuafikiana
funga mzigo wako tayari kwa kuutuma/safirisha,mpigie picha ya jinsi ulivyoufunga mpk ulivyouchora juu ya box lake,baada ya hapo unapoenda kuutuma mzigo wako sasa (HAPA NDIPO PAMUHIMU) mwambie konda au huyo unaemkabidhi
mzigo asiutoe bila kupewa kias husika unachomdai mteja au kuepusha kupeana hela mkononi Mteja afanye muamala wa mzigo wake kisha wewe muuzaji ukipokea muamala ukathibitisha ndipo unampa go ahead Konda amkabidhi mzigo,Hapo maana yake mteja anakua na amani na wewe unakua na amani.
ila maswala ya kumwambia mteja atume hela ya usafiri kwanza au hela ya bidhaa huo ni uzwazwa,umeamua kufanya online business elewa kuna matapeli lkn pia elewa si wote ni matapeli wapo Real customers ambao wanahitaji caring kubwa sana.
Muhimu msome mteja wako huyu n mteja au tapeli,unaweza tu kumsoma bila hata tatzo na ukijua n tapeli usimuonyeshe umemshtukia kwakua bado huna uhakika nenda nae taratbu TU.
Kama n tapeli atakupa hasara ya wewe kulipia tu usafiri lkn hatoweza kkutapeli mzigo wako kama utaamua kufata nilichokiandika.Muhimu na la kuweka kichwani Muonyeshe mteja unamuamini na usiwe na haraka na Malipo.
kauli mbiu yako iwe Huduma kwanza,Malipo Badae
AsanteProcess yako ndefu sana na utapeliwa mara kibao, we mwambie ofisi yetu hii imesajiliwa kwa jina hili leseni yetu ni hii kama huna lesen tuma kitambulisho cha kupiga kula au nida kama ana mtu mkoan ambao wew upo amtume aje ofisin , laa sivyo alipe kama ikishindikana achana na hiyo biashara itakugalimu na utajutia uamuzi wako wa kutuma huo mzigo
Nikikutumia kitambulisho changu kwa pcha,leseni na kila taarifa kwenye simuProcess yako ndefu sana na utapeliwa mara kibao, we mwambie ofisi yetu hii imesajiliwa kwa jina hili leseni yetu ni hii kama huna lesen tuma kitambulisho cha kupiga kula au nida kama ana mtu mkoan ambao wew upo amtume aje ofisin , laa sivyo alipe kama ikishindikana achana na hiyo biashara itakugalimu na utajutia uamuzi wako wa kutuma huo mzigo
Tanzania mambo bado bado sana kenya hapo kuna watu wana system yao ambayo inasaidia malipo kwa njia zote bank transfer, na mobile wallet, lakini ile pesa inabaki kwenye escrow account mpaka mteja atakapo confirm kuwa kapata mzigo wake au kazi yake. Ni kama vile paypal wanavyoshikilia malipo mpaka client aconfirmKaribuni kwa mjadala nafanya online business lakini nimekuwa nakutana na swala la Uaminifu
Ni kweli dunia Imeharibika kuhusu Uaminifu je mwenzangu ulifanikiwa vipi kuhusu Uaminifu mtu anahofia kukupa kazi
Karibuni
cc. CONTROLA
Nami ndo njiani natumia.Biashara ya online lazima uwe na utaratibu wako
Mfano mm , mteja akiitaji bidhaa yangu na mwambia Kama yupo Dar pesa atatoa akipokea bidhaa yake
Kama nje ya Dar atalipia kwanza pamoja na Gharama za usafiri anatumiwa mzigo wake.
Kama akiwa haamini Basi kama ana mtu anayemfahamu Dar atupe no zake atapelekewa huko ,yeye atamalizana na huyo jamaa yake.
Hii njia imenisaidia sana