Naenda Kanisani lakini naenda kwa Shekhe kuloga ili mambo yangu yaende sawa

Siyo kwa ubaya ndugu zangu, misumari ni mingi sana, ukiweka japo kabiashara kako sehemu ili kakusaidie wewe na familia yako ikianza tu kuchanua kuna viherere wanajifanya kuizima.

Sasa nikasema dawa na mimi ni kutembea, simlogi mtu ila naweka mambo sawa, nailinda biashara yangu. Kwani kuna ubaya ndugu zangu?
Aisee..
 
Chagua upande, hapo ni sawa na kuoga then unajigaragaza matopeni,
Kama unaona Giza ndio linakufaa sawa ikiwa Nuru ndio Bora kwako sawa
 
Hivi imani ya kristo ni ipi?
Imani ya KRISTO ni yale yote aliyoamini KRISTO na aliyoamini kutoka kwa MUNGU ndio aliyoyafundisha.
Hivyo basi "imani ya KRISTO" ni yale yote aliyoyafundisha KRISTO na aliyoyaishi kwa vitendo. Ndiyo maana kwenye kitabu cha Ufunuo 14:12 utaona kuwa Watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na imani ya KRISTO.

Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema, "watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na mafundisho(imani) ya KRISTO.

YESU KRISTO aliwafundisha wanafunzi wake kile alichokiamini yeye. Na alichokiamini ni yale yote aliyoyasikia kwa BABA (MUNGU). Yohana 8:28-29
 
Acha tu nichelewe nibaki kwa Mungu... Mungu hana mashart...nitalala nitaamka kwa amani...nitaomba muda wote ajibu asijibu sawa tu.
Jiandae kufa masikini dear!
Yani uishi kwa shida na uende motoni... Kwa uzinzi na unafki na uongo mfano tu sijamanisha wewe
 
wanaohudumu huko makanisani nao ni binadamu tu kama huyosheikh au mganga yoyote wa kienyeji.
Kwani hao wanaohidumu kuanzia pastor na wengine, nimeandika hao ndo tunaowategea na kuwaabudu?
Asante kwa kuchangia
 
Mkuu huwezi kufanikiwa bila kujihusisha huko! So big up kwa kujitambua mapema!

Ila usimsahau Sana Mungu!
Yani kufanikiwa kwa uwezo wa Mungu kupo Ila unahitajika effort.

HAKUNA mtu ambae anapenda mafanikio yako!
Kuna mtaalamu katoka mwanza anaenda Oman mwezi ujao Ni hatari Sana..

Pia anauza majini ya kutafuta na kukutengenezea Bahati kwa gharama mdogo tu.

Changamka pambana kwenye ushirikina kujiimalisha mwenyewe na sio kumuumiza mtu.

Mtu akikuroga uvunjike mguuu wewe vunja kiuno

Maisha Ni kutafuta sio kutafutana
Connection tafadhari.
 
Kama wewe ungekuwa ni Mungu ndio umekomenti hii hakika ningeogopa kumbe ni binadamu tu kama mimi, Mungu afikirii kama unavyofikiria wewe, acha niendelee kuweka mambo yangu sawa simlogi mtu lakini, naweka mambo sawa binadamu wabaya sana.
Kitendo cha kuja tu jukwaani ni kuwa haujiamini pamoja na ushirikina wako. Bahati mbaya unatafuta kuungwa mkono, na inapotokea unapingwa unajisikia vibaya. Kiufupi. Umechemka sana katika hilo.
 
Imani ya KRISTO ni yale yote aliyoamini KRISTO na aliyoamini kutoka kwa MUNGU ndio aliyoyafundisha.
Hivyo basi "imani ya KRISTO" ni yale yote aliyoyafundisha KRISTO na aliyoyaishi kwa vitendo. Ndiyo maana kwenye kitabu cha Ufunuo 14:12 utaona kuwa Watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na imani ya KRISTO.

Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema, "watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na mafundisho(imani) ya KRISTO.

YESU KRISTO aliwafundisha wanafunzi wake kile alichokiamini yeye. Na alichokiamini ni yale yote aliyoyasikia kwa BABA (MUNGU). Yohana 8:28-29

1 Yohana : 5 : 4 - Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
1 Yohana : 5 : 5 - Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Hayo maandiko yana uhusiano na imani ya kristo?
 
Hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
INAMAANA MASHEIKH NI WAGANGA.
WALOZI.
WACHAWI????.

Au ndio maana wanapenda ubani Nazi mayai na mafuta tofauti tofauti
 
Siyo kwa ubaya ndugu zangu, misumari ni mingi sana, ukiweka japo kabiashara kako sehemu ili kakusaidie wewe na familia yako ikianza tu kuchanua kuna viherere wanajifanya kuizima.

Sasa nikasema dawa na mimi ni kutembea, simlogi mtu ila naweka mambo sawa, nailinda biashara yangu. Kwani kuna ubaya ndugu zangu?
Hakuna Wala kosa Nini umesema hapa
 
Back
Top Bottom