Nadharia kuhusu chanzo na maana ya heshima ya kijeshi ya Mizinga 21

Kimsingi kupiga mizinga 21 ina historia toka zamani wakati meli za kijeshi zilipokua zinatembelea nchi za kigeni(zilikua na mizinga 21 ndani ya meli) hivyo mabaharia walilazimika kufyatua mizinga yote katika pwani ya nchi wanayotembelea ili kutoa alama kwamba wanakuja kwa amani. Wakishafyatua wote wanajipanga juu ya meli ili waonekane kwamba hawawezi ku-reload ndo wanaruhusiwa kuingia katika nchi.

Kwahiyo muda ulivyokwenda baadae ikaja kuzoeleka na mapokeo ikawa hata mkuu wa nchi anapotembelea anapigiwa mizinga 21

Askari yeyote anapokufa kwenye mazishi anapigiwa risasi 21?

Mwanajeshi kuanzia cheo cha Brigedia Jenerali anapigiwa mizinga 6 nadhani

Viongozi wakuu wa nchi mizinga 21

Watakuja wajuzi wengine kurekebisha nilipokosea
Asante sana mkuu, umenifungua sasa.
 
Habari za usiku wakuu,

Tukiwa tunaendelea kuomboleza msiba mzito wa kiongozi wetu mpendwa,Hayati Benjamin William Mkapa aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo.

Naomba kuuliza kuhusu mizinga ambayo viongozi wetu wakubwa huwa wanapigiwa pindi wanapofariki au tukio jingine.

Niliwahi kusikia huwa inapigwa mizinga 21(ishirini na moja),Sasa najiuliza kwanini iwe 21 na isiwa kumi,au 30 au basi idadi yeyote ile?

Kwanini mizinga 21?.Pili ina maanisha kitu gani??.Tatu je haiwezi kuleta madhara kwa binadamu km vile kujeruhi au kuua pindi ikikosewa kupiga?.

Nne ukiacha Maraisi,ni viongozi gani wengine wanaostahili kupigiwa mizinga?.Au basi ni matukio gani yanayoweza kupelekea mizinga kupigwa?

Naomba kuwasilisha. Wajuzi wa mambo hayo ya Kijeshi njooni mnielimishe.Alamsiki.
Iliwahi kujadiliwa hapa

Kwa nini Mizinga 21?
 
Ni utaratibu sidhani kama waliuanzisha wao ila ulipewa umaarufu na waingereza, super power wa wakati huo.

Hii ilitokea pale ambapo warship inaingia port ya kigeni.Kabla hiyo warship haijaingia kwenye target za hao wenyeji,basi wenye hicho chombo walikuwa wanafyatua mizinga yote iliyo ndani yake(warship).Nadhani sababu ilikuwa kuashiria kwamba hiyo warship imekuja kwa lengo la amani au tunaweza sema ndo mambo ya salute yenyewe.

By that time haikuwa 21. Ilikuwa ni mizinga 7. Why saba? Sababu namba saba imebeba vitu vyingi katika nyanja za unajimu na kibiblia.Upande wa unajimu kuna haya mambo ya miandamo ya mwezi n.k ila upande wa Biblia kuna hii ishu ya uumbaji (siku 7),sabato(siku ya 7) n.k. Kumbuka pia kipindi hicho hizo warship zilikuwa na projectile moja.So mrusho mmoja ukawa unatoa mzinga mmoja.So hiyo 7 shots ikawa standard.

Baadaye pia zikaja hizi za nchi kavu.Yenyewe zikawa na uwezo zaidi.Ikawa tena sio mrusho mmoja unatoa mzinga mmoja bali mrusho mmoja unatoa mizinga mitatu (more projectiles).

Kwa hiyo idadi ya mirusho ikabaki vilevile ila idadi ya mizinga inayotoka ikaongezeka mara tatu.Kwa nini walichagua no.3? Kuna sababu zake pia. So ikawa 7 × 3 = 21. Hence mizinga 21.

Huu mfumo ulikuwa wa waingereza ila kutokana na yeye kuwa super power kipindi hicho, ulianza kusambaa. Ni kama tu sahivi unavyotumia mfumo wake wa GMT.

At first Marekani hawakukubaliana na huu mfumo ila baadaye waliupitisha.Nadhani unafahamu kitu kikiwa na mkono wa Muingereza na Mmarekani kipindi hicho basi kinakuwa universal.

Kwa hiyo nasi Waswahili tukaiga!

Natumai nimekupa mwanga fulani mtoa mada.
 
Huyo ndugu yako alikuwa Afisa wa jeshi?,Kuhusu madhara nauliza ikitokea ikakosewa kupiga.

Katika risasi/mzinga kunakua na vitu viwili explosive(mlipuko/baruti) na projectile(kile kinachorushwa na mlipuko)

Sasa mizinga ya sherehe inakua haina projectile. Wenyewe wanaita blanks(Musiba alisema blancoo😄😄)

Maana yake nini?? Maana yake ni kwamba inapigwa mzinga/risasi inatoa mlio tu na moshi na moto lakini hakuna kinachorushwa kufwata target yoyote. Hivo haina madhara labda kwa wagonjwa wa moyo tu mshtuko wanaambiwaga wakae chini kabisa kabla(Mizinga baridi inaitwa)
 
Huyo ndugu yako alikuwa Afisa wa jeshi?,Kuhusu madhara nauliza ikitokea ikakosewa kupiga.
Hakuna madhara kwa kuwa ni baruti tu inayoripuliwa pale inakuwa haijaunganishwa war head.
Idadi ya mizinga inategemeana na cheo cha kiongozi anayepewa hiyo gun salute.
Pia wanajeshi kuanzia cheo cha brig gen kuendelea nao hupigiwa mizinga kwa idadi tofauti kwenye mazishi yao kutokana na vyeo vyao.
Ila vyeo vya chini ya hapo mazishi ni kupiga bunduki juu idadi mara3.
 
Hakuna madhara kwa kuwa ni baruti tu inayoripuliwa pale inakuwa haijaunganishwa war head.
Idadi ya mizinga inategemeana na cheo cha kiongozi anayepewa hiyo gun salute.
Pia wanajeshi kuanzia cheo cha brig gen kuendelea nao hupigiwa mizinga kwa idadi tofauti kwenye mazishi yao kutokana na vyeo vyao.
Ila vyeo vya chini ya hapo mazishi ni kupiga bunduki juu idadi mara3.
Yaaap!!!;.nimekupata mkuu.
 
Kwa miaka nenda rudi nimekuwa nikisikia na kushuhudia upigaji wa mizinga 21 kwenye hafla, misiba ya viongozi wa kitaifa.

Hiyo idadi ya 21 inatokana na nini ? Kwanini siyo 5, 10 au 100?
 
Hata ingekuwa 5 bado ungeweza kuuliza kwanini isiwe 21. Nadhani vitu vingine vimewekwa ili maisha yawe meaningful.
 
Back
Top Bottom