Nadharia kuhusu chanzo na maana ya heshima ya kijeshi ya Mizinga 21

Mods please mna chanzo kizuri cha mapato. Wekeni kiwango cha pesa kwa kila uzi mpya mvune mamiliomi
 
Kuna jambo huwa linanitatiza kuhusiana na heshima ya mizinga 21 inayotolewa kwa kiongozi mkuu wa nchi (Rais) aidha anapokuwa katika shughuli za kitaifa ndani kama vile kuadhimisha siku ya uhuru n.k au wanapokuja viongozi maraisi wa nchi za nje kutembelea Tanzania.

Nataka kujua ni kwa nini wanapigiwa mizinga 21 kuwa ni ishara ya heshima kwa Rais, Je chimbuko lake ni nini?, Kwani nini mizinga 21 tu na isiwe zaidi au pungufu ya 21? Kutompigia mizinga 21 Rais kunamaanisha kuwa heshima kwa raisi husika inashuka?

Naomba wale wataalamu wa mambo ya itifaki na kijeshi wanieleweshe kuhusu jambo hili.

Naomba kuwasilisha.
Sababu tuna mizinga mingi sana na toka 1978 nadhani 80% watanzania walikuwa hawajazaliwa hivyo hakuna vita na mizinga ipo tu haina kazi mwisho inaweza lipuka kama huko Mbagala ikikaa muda mrefu. Nawasilisha mkuu
 
Wote humu watasema ni heshima lakin hawatakwambia ni kwann wanatumia mizinga kama ishara ya heshima
Sio mizinga tu,na bunduki pia hutumika.
Rejea askari wanapokuwa wanazikwa ni common sana tu.

Ila kwa mzinga ni ishara kwamba anayezikwa ni mzito kiasi fulani.
 
Ipo hivi kuna malikia wa Uingereza aliwahi kutekwa kipindi hicho kwahiyo katika kumuokoa ilipigwa mizinga 21 pekee ikatosha au kufanikisha kumtoa katika ngome ya adui so ikawekwa kama ishara ya heshima hata pale wanapokuwa wamekufa.
 
Habari za usiku wakuu,

Tukiwa tunaendelea kuomboleza msiba mzito wa kiongozi wetu mpendwa,Hayati Benjamin William Mkapa aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo.

Naomba kuuliza kuhusu mizinga ambayo viongozi wetu wakubwa huwa wanapigiwa pindi wanapofariki au tukio jingine.

Niliwahi kusikia huwa inapigwa mizinga 21(ishirini na moja),Sasa najiuliza kwanini iwe 21 na isiwa kumi,au 30 au basi idadi yeyote ile?

Kwanini mizinga 21?.Pili ina maanisha kitu gani??.Tatu je haiwezi kuleta madhara kwa binadamu km vile kujeruhi au kuua pindi ikikosewa kupiga?

Nne ukiacha Maraisi,ni viongozi gani wengine wanaostahili kupigiwa mizinga? Au basi ni matukio gani yanayoweza kupelekea mizinga kupigwa?

Naomba kuwasilisha.Wajuzi wa mambo hayo ya Kijeshi njooni mnielimishe.Alamsiki.
Umeshasema kwanini isiwe idadi yoyote, hiyo yoyote ndo hiyo 21. Wakipiga 10 utauliza why not 21
 
Kwaiyo lisu naye anapambana ili siku akifa apigiwe mizinga badala ya manati kutoka bavicha
 
Swali liko hivi
#Kwanini Rais akifa wanapiga mizinga 21?
#Kwanini wapige mizinga wasipige bomb? #Na kwanini iwe 21 na is iwe 3?
#Na ninani alianzisha utaratibu huu?

Jibu tafadhali.
 
Taratibu hii ilianzia mwaka 1776 kule marekani.Marekani ilipata Uhuru wake 1776 sasa wanajeshi siku ya Uhuru wakataka kusherehekea siku hiyo kwa kupiga mizinga.Swami likaja wapige mizinga mingapi kuonyesha furaha yao? Mmoja akashauri kuwa wajumlishe namba zote zilizoko kwenye maana 1776 jibu watakalopata ndio liwe idadi ya mizinga watakayopiga.Ukijumlisha namba zote za 1776 jibu utapata 21.yaaani 1+7+7+6 jibu ni 21.wakapiga mizinga 21.toka hapo Ukawa desturi ya majeshi duniani wakifurahia jambo iwe kupokea kiongozi au sherehe kupiga mizinga 21
Naona logic Mkuu. Hongera kutupatia pa kuanzia
 
Dunia ya wapi uliona wanapiga

Jisomee hapo usipoelewa nayo ukasomewe sawa
IMG_7288.jpg
 
Back
Top Bottom