Mwezi uliopita nilienda kumtembelea bibi yangu huko kilolo ndani ndani, tangia nchi ipate uhuru hadi leo maji ya bomba wanayasikia kwenye redio tu, umeme ndio kabisa anasa. Bibi bado anatumia maji ya mto. Nikamuuliza bibi kura ulimpigia nani kwenye uchaguzi? Akajibu nilichagua CCM. Nikamuuliza kwanini? Akanijibu ukishinda upinzani nchi itaingia kwenye vita. Nilicheka sana, nikampa zawadi ya solar niliyompelekea nikaondoka zangu.
Jibu linalofanana na hilo nililipata huko morogoro, matombo nilipokuwa kwenye shughuli zangu za kikazi. Mama mmoja mkulima wa mpunga aliniambia kuwa upinzani ukishinda nchi itachafuka. Huyu mama bado alikuwa anatumia jembe la mkono na hali ya maisha pale kijijini ni ngumu wafanyabiashara wanakuja kipindi cha mavuno na kubadilisha mitumba kwa mpunga.
Jibu kama hilo tena nililipata mtaani kwangu kwa motto mmoja wa miaka 13 anaeitwa Nzeimana. Jina la huyu motto lilinifanya niwe mdadisi kidogo kujua asili yake maana haya sio majina ya wazawa wa Tanzania. nilimuuliza nzeimana kwa utaalamu bila yeye kujua akaniambia kuwa baba na mama yake walikufa huko Rwanda na yeye kuchukuliwa na mjomba wake ambae ndio anamlea hadi sasa. nikamuuliza nzeimana ukiwa mkubwa utakuwa chama gani ? Akajibu CCM. Nikammuliza kwann? Akajibu mjomba kaniambia CCM ikishindwa wageni wote tutarudishwa kwenye chi zetu.
Jibu kama hilo nilipewa na dada mmoja mwenye asili ya msumbiji lakini anajiita mmakonde.
Baada ya hapo nikajiuliza swali kuwa ni nani anaisambaza nadharia hii ya upinzani ukishinda nchi itaingia kwenye machafuko?
'' EDUCATION IS ABILITY NOT NOTES''