Nadhani Tundu Lissu anakosea hapa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Tanzania ni nchi masikini sana, tangu tupate Uhuru hatujawahi kuwa na nafuu, hata Rais Magufuli ameikuta hivyohivyo ikiwa na hali mbaya. Sio siri, wote tunafahamu kuwa wakoloni hawakuondoka kipumbavu wakati wanaliachia bara la Africa ikiwemo Tanzania yetu. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia njia mbali kuendelea kupata malighafi, masoko ya bidhaa zao, na nguvukazi. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia mafariki zao ambao sisi tunawaamini sana kama vile viongozi maarufu, watu maarufu, mashirika ya hisani, mashirika na taasisi za kidini, viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati, WB, IMF, WTO na majasusi kufanikisha adhima zao hizo.

Rais Magufuli ameamua kujilipua na kutumia uncommon sense kutatua common problems zinalolikumba bara lote la Africa hasa kusini mwa jangwa la Sahara. Maana huwezi kutumia common sense kutatua common problems yaliyowashinda Marais wenzako waliokutangulia. Hata wazungu walitumia uncommon sense kufika pale walipofika, uncommon sense yao Ndiyo iliyowatuma watutawale, watufanye watumwa, watufanyishe kazi nyingi bila ujira, kuua Marais wetu waliopinga kunyonywa nk.

Tundu Lissu hakupaswa kupinga kila kitu cha Rais Magufuli kwakuwa vitu ambavyofanya kamavile kuondoa wafanyakazi na wanafunzi hewa, kukamata wakwepa kodi, wauza madawa ya kulevya, kuwaondoa viongozi wasiowajibaka, kujenga miundombinu ya kisasa kama barabara, madaraja na reli, elimu bure , kufufua shirika la ndege na reli, nk. hivi vyote vinaonekana hadharani Kwa watanzania na wasiokuwa watanzania.

Tundu Lissu anapaswa ku acknowledge mazuri na ku condemn mabaya, hapo kila mtu angemuelewa. Rais wetu kuna vitu anavifanya kinyume kabisa na matarajio ya wakoloni tusipomsaidia sio Tu atapandwa na hasira lakini tunaweza kuhatarisha uhai wake Kwa ajili yetu sote.
Hata wademocratics wana vitu wanamkosoa Trump lakini kuna vitu hawezi kumkosoa navyo kwakuwa ni kwamanufaa ya Yao wote
 
Hii hoja ya kusema kwamba Rais Magufuli "anatatua matatizo yaliyowashinda marais waliotangulia" ni upuuzi wa karne. kwa nini? Kwanza kumbuka kwamba "kila enzi na kitabu chake". Matatizo aliyokutana nayo Nyerere, ya kujenga taifa kutoka makabila aliyoyagawa mkoloni, kutengeneza dira ya taifa hilo, kuweka misingi ya utaifa, siyo anayokutana nayo leo Magufuli. Kwa kweli magufuli anabomoa misingi ya utaifa. inafikia hatua tunashuhudia mgogoro wa ajabu kabisa, mgogoro feki wa kutengenezwa kati ya CAG na Spika wa bunge.
 
Rubbish, as long as it involves killing people, i.e loss of lives e.g MKIRU, Coco bech, Ben Saanane,killing our beloved ones, eti ni kuleta maendeleo, whaterver "good" he might be doing, if at are there, goes to the trush, down by the trench!
Mimi sijui kuhusu killing maana ushahidi sina nikiambiwa niseme nani amewaua au wapoteza. Ila ninchofahamu tulikuwa maskini tangu tupate Uhuru miaka 50 iliyopita, kama hao wanaopotea ni sehemu ya mkakati wa kupambana na ukoloni mamboleo ili kuondokana na umaskini mbaya it is fine, wazungu wameua watu wangapi wakati wanajenga uchumi wao?
 
Sasa uhuru wa maoni uko wapi, ikiwa tutafundishana jinsi ya kutia maoni na tuyatoeje.
Unayoyaona wewe mazuri, sio lazima kila mtu ayaone hivyo. Maoni na mitizamo yetu tofauti.
 
Leta ushahidi kuwa wazungu wameua? Hapa ushahidi utaujua mkitoka madarakani! wazungu hawapo, leta ushahidi.una uhuru wa kufanya inquries, .... unachelewa nini?
 
Hujui kwa sababu ya low thinking capacity! Basi!
 
Hii hoja ya kusema kwamba Rais Magufuli "anatatua matatizo yaliyowashinda marais waliotangulia" ni upuuzi wa karne. kwa nini? Kwanza kumbuka kwamba "kila enzi na kitabu chake". Matatizo aliyokutana nayo Nyerere, ya kujenga taifa kutoka makabila aliyoyagawa mkoloni, kutengeneza dira ya taifa hilo, kuweka misingi ya utaifa, siyo anayokutana nayo leo Magufuli. Kwa kweli magufuli anabomoa misingi ya utaifa. inafikia hatua tunashuhudia mgogoro wa ajabu kabisa, mgogoro feki wa kutengenezwa kati ya CAG na Spika wa bunge.
 
We jamaa nilianza km kukuelewa ila kumbe hamna kitu yaan kisa wazungu waliua watu so unasupport watu wauliwe karne hii ili mradi watu wasiikosoe serikali dah bado tu na njia ndefu si tunahitaji kabita bora ambayo itakuwa na goals za taifa bila ivo tutaendelea kuwa nchi maskini mpaka yesu arudi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndio maana siasa ni mchezo mbaya.
Tuna wanasiasa wanajitanabahisha kwa umma lakini ni magenge ya wahuni samples za kina Rungwe,zitto,Bashange na Bavichaa !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rubbish, as long as it involves killing people, i.e loss of lives e.g MKIRU, Coco bech, Ben Saanane,killing our beloved ones, eti ni kuleta maendeleo, whaterver "good" he might be doing, if at are there, goes to the trush, down by the trench!

Killing people by whom! Upuuzi mtupu. Mbona wewe au ndugu yako hawajauliwa?

Kupigwa risasi kwa Lissu kwa sababu anazozijua mwenyewe ndiyo iwe jumuisho ya hoja zako?

Kupotezana watu kwa sababu za kibinafsi, ndiyo hitimisho la hoja zako?

Mtabaki kubwatabwata kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari wakati ule ule mkifaidika na maendeleo yanaonekana nchini, chini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Naamini ndani ya mioyo yenu mnaumia, kama hao mabwana zenu huko ulaya, mnaposhuhudia mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini.
 
Sasa uhuru wa maoni uko wapi, ikiwa tutafundishana jinsi ya kutia maoni na tuyatoeje.
Unayoyaona wewe mazuri, sio lazima kila mtu ayaone hivyo. Maoni na mitizamo yetu tofauti.
Watu maskini na wasio na elimu ukiwapa Uhuru mpana wa kutoa maoni hutiki mbali. Kama wachina ambao ni robo ya world's population kama watapewa Uhuru wa kutoa maoni China itasambaratika. Hata Marekani watu, wanasiasa, wanahabari kuna vitu ambayo wanaviacha hivyohivyo. Uingereza pamoja na elimu na Maendeleo Yao hakuna anayehoji uwepo wa ukoo mmoja Tu wa kifalme unaotumia Kodi zao kifahari milele na milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…