Nadhani somo la ujasiriamali na utengenezaji wa bidhaa vitu na mitambo ndio lingetiliwa mkazo toka awali hadi chuo kikuu

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Hivi kuna mtu yu na mawazo kama yangu?

Tunahitaji nchi ya viwanda, kujiajiri na ubunifu na ujasiriamali

Nadhani somo la ujasiriamali na utengenezaji wa bidhaa vitu na mitambo ndio lingetiliwa mkazo toka chekechea hadi chuo kikuu

Somo la ujasiriamali, stadi za maisha, ubunifu kutengeneza bidhaa ndio ilipaswa liwe somo la kutiliwa mkazo.

Kwa namna hii vijana wengi wangekua zaidi ya Veta, tungekuwa na wataalam chungu mzima wabunifu tena waliojiajiri lakini kwangu historia sio kipaumbele maana yalopita yashapita tu hata ufanyeje hayatosaidia chochote

Tunahitaji kuwaza future ya nchi hii ndo maana tunatakiwa tufokasi kwenye masomo ya kimkakati yenye mahusiano na uchumi wa dunia hii uchumi wa viwanda na uzalishaji.
 
Historia ndiyo muhimili; ukishaijua tu, mengine hujipanga yenyewe. Kwa IQ kubwa ya JPM, wengine itawachukua miaka 1000 japo kuelewa kauli yake moja. Kazi mnayo, halafu mlivyo wabishi sasa!???
 
Who is who?
Historia ni nzuri ila haina msaada wowote kwenye maisha ya upambanaji (kijasiriamali)
Hizo ni hashi na vigano tu mzee pambana na maisha hayana kuremba
 
Mimi nachoshangaa kuna masomo ya historia na civics tunahitaji nini kujua zaidi kuhusu Tanzania?? ..wenzetu wanapima nini kinakosekana katika jamii then wanatunga syllabus, sisi tuna upotolo halafu tunaongeza upotolo..........
Civics ni muhimu sana.. hasa kwa utamaduni mchanga.. Wakati wetu kulikuwa na masomo ya Siasa na Uraia.. haya yalilenga kumfunza mtu juu ya mfumo mzima wa uongozi na majukumu yake kikatiba. Ustaarabu wa kitanzania.

Yalipoondolewa kama masomo nilisononeka.. lakini yalisave lengo.. leo unao watu ambao wanafika mpaka bungeni na hawajui wajibu wa mtanzania, namna ya kumpata kiongozi sahihi na hata namna sahihi ya kumuwajibisha kiongozi kisheria.

Aliyeyaondoa alikuwa na nia.. japo inaviashiria vya uovu. Nadhani ni moja kati ya masomo muhimu kurejeshwa tena.. maana huwezi kutegemea kuwa na raia wema wasiojua wema ni nini kwa mujibu wa sheria/katiba.

Kuchangia kwa Mada hii
Hakuna njia rahisi ya kuwafunza watu kubwa wabunifu.. zaidi ya wao kujua walikotoka matatizo yao,. Na namna gani wamehangaika nayo kuyapatia ufumbuzi.

Kisha wajifunze Discipline tofauti tofauti kwa namna njema na yenye ubora. Wapate vitabu, na waelimishwe kwa namna rafiki kwao.. wazijue nadharia nje ndani.. wazizoee, waweze kuzitafsiri katika maisha yao ya kila siku.. waweze kuziona kwenye vitu vinavyowazunguka..

Automatically, utaona uvumbuzi. Nikiwa shule msingi kulikuwa na vitabu vingi vya sayansi.. na vijana tulipenda kushindana kuunda vitu mfano magari na kuunda kengele ya umeme na kuitumia kama honi..

Ulikuwa ukifika kwenye UMITASHUMTA/UMISETA kukuta vumbuzi kubwa kubwa ilikuwa ni kawaida mno.. maana vijana walielewa vyema nadharia na wa kazitafsiri katika maisha yao ya kila siku.

Tuboreshe Elimu, Kwa kuhakikisha the best ndio wanatulindia Taaluma, huko kwenye kodi na Majeshini pelekeni wenye akili za kawaida.. wale exceptional waende wakafundishe.
 
Mimi nachoshangaa kuna masomo ya historia na civics tunahitaji nini kujua zaidi kuhusu Tanzania?? ..wenzetu wanapima nini kinakosekana katika jamii then wanatunga syllabus, sisi tuna upotolo halafu tunaongeza upotolo..........
Umeongea kwa uchungu na hisia kali mno, we are heading somewhere unexpected of. Playing dumb won 't save but worsen the condition even more. Something must be done to update our education system
 
Umeambiwa kipi ambacho hakisomwi kuhusu Tanzania kwenye CIVICS /URAIA, HISTORY, GENERAL STUDIES hadi leo mtu mmoja amke atake liwe somo moja la kiswahili kuhusu historia ya Tanzania? Hakuna alipo beza.

Asante mkuu, huyu mtu hanijui ila ananipiga biti, utam zoom vipi mtu humjui??? Mwambie akupe jina langu halisi hapa?!?
 
Mimi nachoshangaa kuna masomo ya historia na civics tunahitaji nini kujua zaidi kuhusu Tanzania?? ..wenzetu wanapima nini kinakosekana katika jamii then wanatunga syllabus, sisi tuna upotolo halafu tunaongeza upotolo..........
Juzi mpaka nikajiuliza, kwa hali ilivyo sasa history itamsaidia nini muhitimu kujiajiri ama kuajiriwa?
Nini lengo wanafunzi kusoma historia kutoka darasa la kwanza?
Itawasaidia nini huko mbeleni?
 
Mwenye Nchi anataka Somo la Historia ya Tanzania ili kuimarisha Uzalendo!! Baada ya hapo, tunakuwa Donor Country moja kwa moja.
nafikiri ana miss concept ya uzalendo. uzalendo hauletwi kwa kusoma somo flani, uzalendo ni mapenz ya mtu mwenyewe kwa nchi yake.
huwezi lazimisha mtu apende kitu fulani.

uzalendo si kusimama na rais, si kusimama na serikali.. hao wote wanaweza kuwa corrupted.. lakin ni tanzania kama nchi itabaki.
 
Inasikitisha sana watawala hawachukui maoni ya wananchi. Mtaala wa kikoloni ulishafeli zamanii... hovyo kabisaa..
Hivi kuna mtu yu na mawazo kama yangu?

Tunahitaji nchi ya viwanda, kujiajiri na ubunufu na ujasiriamali

Nadhani somo la ujasiriamali na utengenezaji wa bidhaa vitu na mitambo ndo lingetiliwa mkazo toka chekechea hadi chuo kikuu

Somo la ujasiriamali, stadi za maisha, ubunifu kutengeneza bidhaa ndo ilipaswa liwe somo la kutiliwa mkazo.

Kwa namna hii vijana wengi wangekua zaidi ya Veta, tungekua na wataalam chungu mzima wabunifu tena waliojiajiri lakini kwangu historia sio kipaumbele maana yalopita yashapita tu hata ufanyeje hayatosaidia chochote

Tunahitaji kuwaza future yanchi hii ndo maana tunatakiwa tufokasi kwenye masomo ya kimkakati yenye mahusiano na uchumi wa dunia hii uchumi wa viwanda na uzalishaji.
 
Back
Top Bottom