SoC02 Umuhimu wa somo la ujasiriamali katika elimu ya kijana wa kitanzania

Stories of Change - 2022 Competition

KALEKU

Member
Feb 23, 2015
8
6
images (10).jpeg

Upatikanaji wa ajira kwa vijana bado ni jambo linaloisumbua si Tanzania tu bali dunia nzima. Katika kujikwamua na tatizo la upatikanaji wa ajira kila taifa linajitahidi kuchukua hatua za kujikwamua lakini bado matokeo ya mipango ya kujikwamua ni kidogo sana ukilinganisha wanaohitaji kuajiriwa na wanaopata ajira hususani kwa vijana katika nchi ya Tanzania.

Wakati mwingi wengi wanaishia kuilaumu serikali na hata baadhi ya vijana kuilaumu serikali iliyo madarakani kwa kushindwa kuwasaidia kupata ajira ili kumudu gharama za maisha. Ukweli ni kwamba serikali inajitahidi kwa jinsi inavyoweza kulingana na miundombinu wezeshi lakini bado ni kwa kiwango kidogo sana. Badao kuna kazi kubwa ya kufanywa kuanzia ngazi ya serikali kuu mpaka kwa kijana binafsi ili kujinasua katika janga la ukosefu wa ajira ambalo kwa sasa ni changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea kama Tanzania.

Katika Makala hii nimelenga kuonyesha umuhimu wa somo la ujasiriamali katika elimu ya kijana wa Kitanzania ili mwisho wa elimu nchi isiwe na wahitimu ambao watakuwa ni mzigo kwa Taifa kwa kuwa tegemezi bali kila anayehitimu awe na uwezo wa kuona fursa zitakazompa kijana uwezo wa kujitegemea na kuondokana na utegemezi kwa familia au serikali kama chanzo pekee cha ajira.

Elimu ya kijana wa Kitanzania kwa asilimia kubwa imelenga kumpa kijana ujuzi fulani ili mwisho aweze kuajiriwa na mara chache kujiajiri. Kama elimu hiyo toka awali imejikita zaidi katika kuandaa mwajiriwa ni vigumu sana kijana kuhitimu na kutakiwa kujiajiri peke yake wakati msingi wake wote umebebwa na elimu inayomwandaa kuajiriwa.

Somo la ujasiriamali mashuleni tangu awali litawaandaa vijana kuwa na uwezo wa kiakili kufikiri na kubuni vyanzo binafsi vya kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.

UJASIRIAMALI NI NINI?
Ujasiriamali ni uwezo wa kiufahamu wa mtu kuona na kutambua fursa mbalimbali katika maisha ya watu, kuiwekea mikakati na mipango ya kuifanya kabla ya kuchukua hatua za kuthubutu kuiweka katika uhalisia.
Ujasiriamali ni ubunifu na uvumbuzi unaolenga kuanzisha miradi mbalimbali kwa kuthubutu kulingana na rasilimali wezeshi kutokana na uhitaji wa watu kwa lengo la kupata faida.

Kuna tofauti kubwa kati ya biashara na ujasiriamali kwani ujasiriamali hauhusiki na kutafuta mtaji na kujishughulisha na kuzalisha, kununua au kuuza vitu mbalimbali kwa kuiga wengine. Ujasiriamali unatokana na wazo la kiubunifu kutoka kwa mwanzilishi kwa kuyasoma mazingira kisha kuona changamoto na kuitafutia ufumbuzi. Wengi hujifunza kuhusu biashara mbalimbali na kuita ujasiriamali kitu ambacho sio sahihi. Unapojifunza kitu ambacho mwingine yuko sokoni anakifanya hiyo ni biashara tayari.

Mtu anayehusika na ujasiriamali huitwa MJASIRIAMALI. Ni mtu anayetumia rasilimali kama ardhi, mtaji na nguvu kazi kuibua wazo na kuthubutu kulifanyia kazi ili kuzalisha bidhaa itakayotatua uhitaji katika jamii.

Katika elimu ya Tanzania somo la ujasiriamali hufundishwa kama mada tu katika somo la biashara (Commerce) katika ngazi ya elimu ya sekondari. Katika elimu ya msingi wanafunzi wengi hawapati kujifunza kwa undani kuhusu ujasiriamali. Katika ngazi ya chuo wengi husoma kozi hii kwa mihula kadhaa ambayo bado haitoshi kuwapika wahitimu kuwa wajasiriamali wabobezi.

Katika taifa ambalo wahitimu wengi wanatarajiwa kujiajiri ni vema kuwa na msingi wa somo la ujasiriamali ili kuwawezesha wengi kutoka wakiwa na uwezo wa kubuni miradi mbalimbali na kuiendesha ili kujikwamua.

Katika ngazi ya sekondari haitoshi kuwa na mada tu ya ujasiriamali katika somo ambalo bado ni la uchaguzi kwa wanafunzi. Lazima lianzishwe somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa wanafunzi wote lengo likiwa ni kutengeneza wahitimu ambao hawatakuwa mzigo kwa taifa kesho kwani watakuwa na uwezo wa kujiajiri. Ni hatari na ni aibu kuwa na wahitimu wa vyuo vikuu ambao wakihitimu wanaanza upya kutafuta ujuzi mdogo katika nyanja kama ufugaji, kilimo, biashara na nyinginezo wakati wamekaa darasani miaka mingi.

Ni vizuri kila muhitimu atengenezewe uwezo wa kiufahamu wa kubuni miradi mbalimbali katika mazingira husika ila kujikwamua. Ni aibu kuwa na wasomi wanaohitimu na kuja kunakili biashara za wengine mitaani bila kuonyesha tofauti yoyote ili kuweza kupata soko zaidi. Si vibaya kuiga kwa wengine ila tatizo linakuja tunapokuwa na wasomi wengi katika eneo moja wakati fursa ni nyingi ila macho ya kuziona hayapo.
Somo la ujasiriamali likiwekewa misingi toka awali taifa litazalisha vijana wabunifu wenye uwezo wa kujikwamuwa kimaisha na kuiondolea jamii changamoto nyingi. Katika zama hizi za sayansi na teknolojia lazima kuzalisha wasomi wenye uwezo wa kuisoma dunia inataka nini na kuja na majibu.

DUNIA INA VIJANA WENGI WASIO NA AJIRA LAKINI WAKATI HUO HUO DUNIA IMEJAA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO ZIKITATULIWA NI AJIRA TOSHA.

FAIDA ZA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WAHITIMU WA TANZANIA

Vijana wa Kitanzania wanapohitimu wakiwa wabobezi katika somo la ujasiriamali ni faida kwao binafsi, jamii na taifa kwa ujumla kama ifuatavyo.

1. KUPATA WABUNIFU
Kutokana na elimu ya ujasiriamali inayojikita katika kuvumbua vitu vipya, wahitimu watasaidia kubuni na kuvumbua bidhaa na miradi mbalimbali ya kuwasaidia kujikimu na kutatua mahitaji katika jamii.

2. MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI
Kuna rasilimali zinalala kwa kukosa watu wenye uwezo wa kufikiri matumizi yake. Elimu ya ujasiriamali itaruhusu rasilimali mbalimbali kutumika kwa ufanisi.

3. KUZALISHA AJIRA
Elimu ya ujasiriamali ni tiba ya tatizo la ajira. Wahitimu wenye uwezo wa kubuni miradi mbalimbali watajikwamua na kuepukana na wimbi la ukosefu wa ajira.

4. KUKUZA KIWANGO CHA MAISHA
Elimu ya ujasiriamali itasaidia vijana wengi kukuza na kuboresha viwango vyao vya maisha kupitia vipato vyao binafsi vinavyotokana na miradi yao.

5. KUKUA KWA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Elimu ya ujasiriamali ni kichocheo cha kukua kwa sayansi na teknolojia kupitia uvumbuzi na ugunduzi unaofanywa na vijana wajasiriamali.

6. KUKUA KWA UCHUMI NA PATO LA TAIFA
Kupitia elimu ya ujasiriamali inayozalisha wajasiriamali, uchumi na pato la taifa linaweza kukuwa kwa kupata mapato katika miradi mbalimbali ya ujasiriamali.

HITIMISHO: Elimu ya ujasiriamali ni msingi wa vijana wengi kuweza kujiandaa kujiajiri. Kama serikali inataka kuepukana na changamoto ya ajira kwa vijana lazima uwekezaji uanzie kwenye kufundisha ujasiriamali kama somo kuanzia elimu ya chini ili kuandaa vijana wenye uwezo wa kubuni na kuendesha miradi yao binafsi itakayowakwamua wao na kulinufaisha taifa kimapato.

ELIATOSHA NYITI 0746 55 55 44
 
View attachment 2343682

ELIMU YA UJASIRIAMALI IKIFUNDISHWA KAMA SOMO MASHULENI ITAWASAIDIA VIJANA KUEPUKA ADHA YA KUKOSA AJIRA
 
Back
Top Bottom