Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Nadhani kwa picha hii nitaeleweka kuhusu ubinafsi ambao nimekuwa nikionglea mara kwa mara na umuhimu wa umoja katika malengo.
Weka taswira kwamba boti hilo kubwa ni Nchi. Imewabeba raia ambao wana mwelekeo fulani na sehemu fulani wanapaswa kufika. Lakini kutokana na uchu na ubinafsi wanaanza kubomoa meli na kuigawanya ili kila mtu awe na kiboti chake kidogo. Hawapendi kuishi katika boti kubwa kila mtu anataka kuwa na lake. Wanatoa mbao kwenye meli ili kila awe na boti lake kutoka kwenye lile boti kubwa.
Hawajui kwamba dhuruba la baharini linahitaji uwepo wa boti kubwa na sio viboti vidogo ambayo haviwezi kuhimiri mawimbi makubwa ya baharini na upepo.
Ni dhahiri kwamba wana hatarisha maisha yao sababu ya ubinafsi.
Picha hii ni kielelezo. Cha umuhimu wa umoja katika malengo na madhara ya ubinafsi. Katika nchi na katika jamii. Kwamba kama jamii tukiendekeza ubinafsi na kila mtu kujiangalia yeye hatutafika.