Nabii Mwamposa akifikishwa Mahakamani " Atakuwa shahidi wa saba na sio mshitakiwa"

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,638
Baada ya kutokea vifo zaidi ya watu 15 katika mkanyagano wakati waamini wanaohisiwa ni wa dini ya kikristo wakigombea kwenda kukanyaga mafuta ya upako" huko moshi, mkoani kilimanyaro.

Kutokana na mashinikizo mbalimbali kutoka kwa Wakristo wasiokuwa na Imani kwa maji ya upako na mafuta ya upako, na hata kwa kebehi za dini zingine, kuna uwezekano wa Nabii Mwamposa kufikishwa mahakamani.

Kama atafikishwa mahakamani atakuwa shaihidi na sio mtuhumiwa. Atakuwa mtuhumiwa tu iwapo mafuta hayo yamewadhuru hao waliofariki au kujiruhiwa.

Kwa nini:

Tanzania inaruhusu wanachi wake kuamini kitu chocho ili mradi hawavunji sheria.
kwa hiyo kuamini kukanyaga mafuta sio kosa la walipata shida au sio kosa kwa Nabii Mwamposa.

Pili: Sio kosa la kidini kupaka mafuta.
Hapo kabla kwenye biblia watu na wafalme na manabii walipakwa mafuta ili kuwa na upako wa kufanya majukumu yao waliyopewa na munu pia yalitumika kwa ajili ya uponyaji. kama ninavyonukuu hapa chini.

Mafuta ya kutia, ambayo imetajwa mara 20 katika Maandiko, yalitumiwa katika Agano la Kale kwa kumwaga juu ya kichwa cha Kuhani Mkuu na uzao wake na kuinyunyiza hema na vyombo vyake vya ili kuzifanya kama takatifu na ambazo zimetengwa kwa Bwana (Kutoka 25 : 6; Mambo ya Walawi 8:30; Hesabu 4:16). Mara tatu imeitwa ", mafuta takatifu ya kutia" na Wayahudi walikatazwa kabisa kuitengeneza kwa matumizi binafsi (Kutoka 30: 32-33). Viungo vya mafuta ya kutia hupatikana katika Kutoka 30: 23-24 na vilikuwa na manemane, sinamoni na viungo vingine vya asili. Hakuna dalili kwamba mafuta au viungo hivi vina nguvu yoyote isiyo ya kawaida. Badala yake, ukali wa miongozo ya kuunda mafuta hayo ilikuwa mtihani wa utii wa Waisraeli na maonyesho ya utakatifu kabisa wa Mungu.

Hapo hakuna kosa la kidini/ Ukristo. kwa sababu pia yalitumika

Vifungu vinne tu vya Agano Jipya hurejelea mazoezi ya kupaka mafuta na hakuna hata mmoja wao anayoelezea matumizi yake. Tunaweza kutekeleza hitimisho letu kutoka kwa muktadha. Katika Marko 6:13, wanafunzi wanawapaka mafuta wagonjwa na kuwaponya. Katika Luka 7:46, Maria anatia mafuta miguu ya Yesu kama ibada. Katika Yakobo 5:14, wazee wa kanisa wanatia wagonjwa mafuta ya uponyaji. Katika Waebrania 1: 8-9, Mungu anasema kwa Kristo Anaporudi kwa ushindi mbinguni, "Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitakaa milele na milele ..." na Mungu anamtia mafuta Yesu "kwa mafuta ya furaha".

Haja ya kisheria.

lazima tujiulize nini chanzo cha vifo na majeruhi?
Chanzo ni umati wa watu kugombania kuwahi kukanyaga mafuta ya upako yaliyobarikiwa na nabii Mwamposa,
Ni kama kuwe na mkutano wa siasani na watu wakakanyagana au ni kama watu wakiwa kwenye mpira wa miguu halafu kwa sababu moja au nyingine wakakanyagana.

Sasa nani mwenye kosa?


Mkuu wa Polisi wa Mkoa, (kutokuwajibika ulinzi na usalama)
Mkuu wa polisi wa wilaya,(kutokuwajibika ulinzi na usalama)
Mkuu wa mkoa (awajibike kisiasa).

Nabii Mwamposa na waandaaji wake ni kama mashahidi ili kuthibitisha mashitaka ya hao hapo juu. (g vibali, mandalisi na mkusanyiko mkubwa.)

Viongozi hawa wanatakiwa kuchuliwa hatua za kindhamu na kisheria kwa kutokutimiza majuku yao vizuri.
Hawezi kuja mtu ambaye ni maarufu (Public figue) halafu wakakaa na kubweteka maofisini bila kuchukua taadhali ya mkusanyiko mkubwa wa watu. Hasa mashitaka yao yatanoga iwapo Nabii Mwampsa alikuwa na kibali cha Mkutano.

huu ndiyo ukweli kwa mtazamo wangu
 
halafu ukute mahakimu na mawakili watakao shughulikia shauri hilo baadhi yao walishashiriki ibada zake angalau kinafsi

na wale walokuwa wakitamani mwona siku zote kwa ukaribu walikosa nafasi sasa wanaeza mshika hata mkonoo

wimbo... paulo usije kucheza na sisi una mikono michaafuu....mwamposa usije karibu una mikono ya mafuta ya upakooooo 🤣 🤣 🤣 🤣
 
aje atueleze scientific proof/ spiritual proof ya hayo mafuta yake, asituletee majanga nchini kwetu.......kupoteza nafsi/uhai wa wenzetu inauma sana. Watu wakija uwasaidie usiwaue please!!!
 
aje atueleze scientific proof/ spiritual proof ya hayo mafuta yake, asituletee majanga nchini kwetu.......kupoteza nafsi/uhai wa wenzetu inauma sana. Watu wakija uwasaidie usiwaue please!!!
Kaka watu wanashida sana, ajira hakuna, pesa hakuna, uchumi mbovu, mabo hayaendi, watu wanasoma wanabaki wanastafu wakiwa nyumbani.

Wanatafuta njia mbadala kiroho (spiritual.)
 
Mwamposa ni tapeli tu, kama yalivyo matapeli mengine yanayotumia biblia kama njia ya kufanya utapeli wao.. Ashtakiwe hata kwa utapeli, wakimkosa huko wampe kesi ya kutolipa kodi kila anapowauzia waumini wake hayo maji.. Ikishindikana tutamuomba Pompeo amuweke na huyu kwenye listi ya bashite..

Mbona miaka ya 70, 80 na mpaka 90 hakukuwa na aina hii ya wachungaji na makanisa yao..?
 
Mtoa mada wacha kuhalalisha Makosa makubwa yaliyofanywa na mchungaji, katika makutano ya watu wengi cha kwanza kabisa kinachopaswa kuzingatiwa ni usalama, lazima kuwapo na safety plan, pamoja na watekelezaji wake, lazima ijulikane ni namna gani watu watakua controlled ili kuepusha majanga au kupunguza athari endapo janga litatokea, mahali kama pale walitakiwa wapite watu kwa mistari mitatu mitatu kuelekea nje, ni kosa kubwa sana lilifanyika japo polisi nao wanamaswali yakuulizwa ....
 
Kwanini wafe moshi wasife dar na kote wanakayaga mafuta kwanini aweke utaratibu wa mtego ilihali anajua watot wagonjwa wapo katika ilo kundi?,je hana uzoefu na ilo suala hana washauri?,hakupewa unabii na mungu ake,kwanini aliondoka kama ameacha kuku wakigombania mchele?, mpuuzi na mbwa kama wengine

Awe shahidi awe mtuhumiwa akiachiwa lazima alipe faini ya kila familia za wahanga angalau ml 50 kwa sababu amefanya kimakusudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka watu wanashida sana, ajira hakuna, pesa hakuna, uchumi mbovu, mabo hayaendi, watu wanasoma wanabaki wanastafu wakiwa nyumbani.

Wanatafuta njia mbadala kiroho (spiritual.)
na hiyo inasaidia kuwatuliza badala ya kuingia msituni hasira zao wanazimalizia kanisani kwa kukanyaga mafuta ya upako wanatulia na nchi inakuwa na amani
 
Nabii Mwampsa alikuwa na kibali cha Mkutano.

huu ndiyo ukweli kwa mtazamo wangu
Pamoja na kumsafisha sisi tunachoshangaa zaidi ni ile kukimbia kwa kificho,kuondoka usiku usiku na gari kutowasiliana na vyombo vya usalama na kuendesha ibada mpaka saa4.3 asubui. Ina maana aliwahi fweza. Alipoona ameitia kibindoni mpunga ndio akasema haya naenda moshi.
 
Mbona huleti maandiko yanayoonesha

Manabii, mitume na Yesu wakiuuzia watu mafuta ,chumvi na keki


Halafu unatumia maandiko ya agano la kale

Sihuwa mnasema limepitwa na wakati

Mnapotumia hayo maandiko mkumbuke , kuwa Agano la kale limekataza na kula nguruwe

Msilitumie tu kwenye kukusanyia sadaka na kutapelia watu
 
Kibali cha mkutano ilikiwa mwisho saa12 Jioni,akafanya mkutano na maigizo ya mafuta hadi usiku,kinyume na kibali,kosa juu la kumshitaki na kumfunga!;
 
aje atueleze scientific proof/ spiritual proof ya hayo mafuta yake, asituletee majanga nchini kwetu.......kupoteza nafsi/uhai wa wenzetu inauma sana. Watu wakija uwasaidie usiwaue please!!!
Mkuu kipindi kile watu wanapiga kikombe cha babu yale maji yalithibitishwa kisayansi au kiimani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom