salaam wanajamvi,
Leo nimeamua kuandika kuelezea umma namna udini na ukabila ulivyojengeka nchini, hususani katika mapenzi. Mimi ni mhandisi mhitimu wa chuo kikuu nina miaka 28. Mara ya kwanza kujihusisha na mahusiano ilikua mwaka 2006, wakati huo nikiwa form 6. Nakumbuka ilikua Dodoma, nilipokutana na mpenzi wangu huyo wa kwanza katika maisha yangu. Tulipendana sana, na tuliwekeana malengo na mipango mingi ambayo kwa asilimia kubwa tuliweza kkuitimiza.
Matatizo yalianza kuzuka mwaka 2007 huyu binti alipoenda chuo kusoma na mimi nikachagua kufanya kazi kwanza, kampuni flani hivi ya madini. Vikaanza visa kila kukicha , japo nilijaribu kumtimizia kila alichohitaji.....hatimaye aliamua nimwaga rasmi mwaka 2009
Nakumbuka nilimwaga machozi na kuchanganyikiwa. wakati huo nilikua nimejiunga na chuo , niko mwaka wa kwanza.... tulikua katika mitihani...nilifeli karibu nusu ya mitihani yote. ilinichukua miaka miwili kusahau kidogo kilichotokea.
Binafsi, sikuweza kuanzisha mahusiano na binti yoyote kwa kua katika nafsi yangu nilikua nampenda x wangu tu. wapo waliojaribu kunitega, relationships zingine zilivunjika ndani ya usiku mmoja.
Wakati nakaribia kumaliza mwaka wangu wa mwisho chuoni, mpenzi wangu wa zamani alirudisha mawasiliano na akanieleza sababu zilizosababisha aniache. akaniamabia ni kwa kua mimi ni mtu wa musoma , kwao sikubaliki. ati kuna dada yake aliwahi kupata mchumba mtu wa msoma akamsumbua sana, tangu siku hiyo ikawa nongwa kwao. sababu ingine akaniambia pia kwa kua mimi ni msabato.... ati kwao wasabato wanawachukulia kama walokole na wenye imani kali. akaniambia yuko tayari kurudiana na mimi iwapo tu nitaamua kubadili dini na kua mkatoliki kama yeye... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi kadhaa, nilikutana tena na binti wa kichaga... mwanachuo, mhandisi wa fani sawa na yangu. katika urafiki wetu uliodumu kama miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
uchungu niliopata siku hiyo siwezi simulia...nakumbuka nilienda slip way nikasimama na kushangaa bahari huku machozi yananitoka kwa zaidi ya masaa 6...
dini yangu, kabila langu imekua jinamizi kwangu.....nakereka zaidi na kauli kua nisubiri wangu anakuja.
nawashauri wote ambao mnabagua kwa udini na ukabila muache hizo mambo.. mnaumiza sana wengine. mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth: