Nabaguliwa kisa dini na kabila

Nabaguliwa kisa dini na kabila

Aisee umesahau wasabato ni marufuku kula kiti moto na pombe aisee,lakini pasaka wanafanya siku tofauti na wakristo wengine wanaita meza ya bwana ndo pasaka yao. kuhusu krismas hakuna maandiko kwenye Biblia yanayosema kuhusu krismas au ya kuwa krismas ni tarehe 25/Desemba,mimi nina rafiki msabato kinachonifurahisha wasabato ni kama wanazuoni wanabisha kwa kujenga hoja,kwa facts wanasoma Biblia vilivyo ukibisha unapewa kifungu.
 
..... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth:
Mkuu kuna rule of engagement inayosema, If you can't beat them, join them.
Hao wanawake wamekuwa fair sana kwako kwa kukueleza sababu zao katika mapenzi cha kushangaza wewe hujawa fair kwao kwa kutokuwaeleza kwa nini usifanye wanachotaka ukifanye badala yake unalalamika tu.
Hivi umeishajiuliza kwa nini kabila na dini yako inakuwa ni tatizo kwao. Inawezekana tatizo unalo wewe badala ya wao.
OPEN YOUR EYES na ujipime kwanza kama kweli unataka mapenzi na wao
 
Aisee umesahau wasabato ni marufuku kula kiti moto na pombe aisee,lakini pasaka wanafanya siku tofauti na wakristo wengine wanaita meza ya bwana ndo pasaka yao. kuhusu krismas hakuna maandiko kwenye Biblia yanayosema kuhusu krismas au ya kuwa krismas ni tarehe 25/Desemba,mimi nina rafiki msabato kinachonifurahisha wasabato ni kama wanazuoni wanabisha kwa kujenga hoja,kwa facts wanasoma Biblia vilivyo ukibisha unapewa kifungu.
 
salaam wanajamvi,
Leo nimeamua kuandika kuelezea umma namna udini na ukabila ulivyojengeka nchini, hususani katika mapenzi. Mimi ni mhandisi mhitimu wa chuo kikuu nina miaka 28. Mara ya kwanza kujihusisha na mahusiano ilikua mwaka 2006, wakati huo nikiwa form 6. Nakumbuka ilikua Dodoma, nilipokutana na mpenzi wangu huyo wa kwanza katika maisha yangu. Tulipendana sana, na tuliwekeana malengo na mipango mingi ambayo kwa asilimia kubwa tuliweza kkuitimiza.
Matatizo yalianza kuzuka mwaka 2007 huyu binti alipoenda chuo kusoma na mimi nikachagua kufanya kazi kwanza, kampuni flani hivi ya madini. Vikaanza visa kila kukicha , japo nilijaribu kumtimizia kila alichohitaji.....hatimaye aliamua nimwaga rasmi mwaka 2009
Nakumbuka nilimwaga machozi na kuchanganyikiwa. wakati huo nilikua nimejiunga na chuo , niko mwaka wa kwanza.... tulikua katika mitihani...nilifeli karibu nusu ya mitihani yote. ilinichukua miaka miwili kusahau kidogo kilichotokea.
Binafsi, sikuweza kuanzisha mahusiano na binti yoyote kwa kua katika nafsi yangu nilikua nampenda x wangu tu. wapo waliojaribu kunitega, relationships zingine zilivunjika ndani ya usiku mmoja.
Wakati nakaribia kumaliza mwaka wangu wa mwisho chuoni, mpenzi wangu wa zamani alirudisha mawasiliano na akanieleza sababu zilizosababisha aniache. akaniamabia ni kwa kua mimi ni mtu wa musoma , kwao sikubaliki. ati kuna dada yake aliwahi kupata mchumba mtu wa msoma akamsumbua sana, tangu siku hiyo ikawa nongwa kwao. sababu ingine akaniambia pia kwa kua mimi ni msabato.... ati kwao wasabato wanawachukulia kama walokole na wenye imani kali. akaniambia yuko tayari kurudiana na mimi iwapo tu nitaamua kubadili dini na kua mkatoliki kama yeye... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi kadhaa, nilikutana tena na binti wa kichaga... mwanachuo, mhandisi wa fani sawa na yangu. katika urafiki wetu uliodumu kama miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
uchungu niliopata siku hiyo siwezi simulia...nakumbuka nilienda slip way nikasimama na kushangaa bahari huku machozi yananitoka kwa zaidi ya masaa 6...
dini yangu, kabila langu imekua jinamizi kwangu.....nakereka zaidi na kauli kua nisubiri wangu anakuja.
nawashauri wote ambao mnabagua kwa udini na ukabila muache hizo mambo.. mnaumiza sana wengine. mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth:

hata wewe ni mdini pia, kwanini umlazimishe mwenzako kuwa sabato masalia angali wewe hutaki kuwa Mkatoliki? acha udini kama unataka kuoa binti wa kabila na imani nyingine kubalianeni lakini kila mtu abaki na imani yake kama wewe hutaki kubadili dini yako na yeye anataka kubaki na imani yake pia.
 
I think its a time for u-sabato kupitiwa upya..coz unaonekana kama ni dini au imani ya dunia nyingineeeee...enzi zile za zinjatrophus au kina homo-habilis sapiens. Kama dini/iman inakataza kunywa soda..nina waswasi na hizi blackberry, i-pads, i-phones etc...na sikuhizi zimekuja tena galaxy, mara nokia lumia....bado mi-face book, twirraaaaaa, whtsup etc.

Hii dini yako kaka ipo ki-kale sana kwa mwanamke wa 21st century kukubali kuolewa nawe....kama vip bora hata uwe mlokole wa kwa kakobe au ma arwakatare....coz mwisho wa siku ishu ni kwenda mbinguni kupitia njia ya yesu kristo.

Kuhusu suala la ukuryaaa a.k.a u-musoma, ni suala la kukubaliana na mpenzi wako na ikiwezekana anunue dol kubwaa linalofanana naye ili siku ukitaka kumtandika migumi unapiga hilo doll lake hasira zako zinatulia...and for curiosity...

Mbona ugomvi wenu wa huko tarime wa mapanga na mingumi mkija dar munauacha hukohuko?...sijawahi kusikia mkurya kumpiga mzaramo au hata msukuma.
 
Hata nami siwezi olewa na msabato; na ukizingatia mapenzi ya siku hizi unajifunza kumpenda mtu, so kigezo cha compatibility kwenye Imani ni muhimu. And for you guys huwa mnatuona wakatoliki ni waovu kuliko shetani mwenyewe; kiasi kwamba vita yenu na ukatoliki ingehamia kwa shetani, mbigu ingekuwa yenu.

Ushauri wangu, tafuta mchumba kanisani kwenu. Issue ya kupigwa hakuna mdada anavumilia hivyo jua the moment unalift Mkono kumpiga mtu ni sawa na kumpa talaka plus jela.
 
Daaa kuwa msabato gafla inabidi ujipange lolz!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
bora umekuwa muwazi.

Kwa freelanders ni ngumu kwa kweli.

Kusema ukweli Sabato ni Wakristo, lakini kidogo mna mambo magumu , na ndiyo maana mnahisi kubaguliwa.
Mambo kama yafuatayo ni ishu sana:
-Kutokula nyama
z
-Kutokunywa soda

-Kutokula baadhi ya samaki.

-kutokunywa chai na kahawa.

-kutopika wala kugusa chochote jumamoc.

-chakula cha jmosi kupikwa ijumaa.

-jua likizama ijumaa sabato ishaanza.

-mambo ya lesoni, pathfinderz, makambi etc

-hakuna sikukuu zozote za kikristo.

-hakuna vipindi maalum vya kanisa kama vile Majilio, Kwaresma, Ijumaa kuu na Jumatano ya majivu.

-masharti kama kutokutengeneza nywele kwa mwanamke, wakati mnajua MWANAMKE NYWELE.

-Kutumia na kuamini zaidi agano la kale kuliko jipya.

Kweli mdada anahitaji maamuzi magumu kabisa kuamua kuachana na mambo aliyozowea na kuwa msabato.
Dadaangu wa tumbo moja akiamua kuwa msabato nitamkubalia, lakn nitalia sana na machozi yataenda tumboni.
 
Aisee umesahau wasabato ni marufuku kula kiti moto na pombe aisee,lakini pasaka wanafanya siku tofauti na wakristo wengine wanaita meza ya bwana ndo pasaka yao. kuhusu krismas hakuna maandiko kwenye Biblia yanayosema kuhusu krismas au ya kuwa krismas ni tarehe 25/Desemba,mimi nina rafiki msabato kinachonifurahisha wasabato ni kama wanazuoni wanabisha kwa kujenga hoja,kwa facts wanasoma Biblia vilivyo ukibisha unapewa kifungu.

Na jamaa zangu 12 wanatokea wote Msoma na wote wa wasabato
 
Kusema ukweli Sabato ni Wakristo, lakini kidogo mna mambo magumu , na ndiyo maana mnahisi kubaguliwa.
Mambo kama yafuatayo ni ishu sana:
-Kutokula nyama
z
-Kutokunywa soda

-Kutokula baadhi ya samaki.

-kutokunywa chai na kahawa.

-kutopika wala kugusa chochote jumamoc.

-chakula cha jmosi kupikwa ijumaa.

-jua likizama ijumaa sabato ishaanza.

-mambo ya lesoni, pathfinderz, makambi etc

-hakuna sikukuu zozote za kikristo.

-hakuna vipindi maalum vya kanisa kama vile Majilio, Kwaresma, Ijumaa kuu na Jumatano ya majivu.

-masharti kama kutokutengeneza nywele kwa mwanamke, wakati mnajua MWANAMKE NYWELE.

-Kutumia na kuamini zaidi agano la kale kuliko jipya.

Kweli mdada anahitaji maamuzi magumu kabisa kuamua kuachana na mambo aliyozowea na kuwa msabato.
Dadaangu wa tumbo moja akiamua kuwa msabato nitamkubalia, lakn nitalia sana na machozi yataenda tumboni.

Mh. Mimi ni msabato ila nnachoweza kusema ni kwamba watu wanakuza na kupotosha mambo mengi.
.. wasabato wanakunywa soda aina zote, iwe cocacola, fanta au sprite/pespi.
.. kweli baadhi ya samaki watu hawali ila kama mmekutana na mtu, mnapendana, hiyo si issue kabisa.
.. most SDAs wanakunywa chai na kahawa sana tu, kuna mafundisho ynatolewa kuwa chai, kahawa, hizo soda zina side effect ila we are not forced to stop drinking, it's one's choice.
.. ni kweli kuanzia ijumaa tunapumzika na kupumzisha mwili na akili, for me hili ni jambo zuri as in, kama nimefanya kazi kweli for six days, i have the reason to relax, hata hivyo labda niseme kuwa kwa maisha ya mjini na ajira za sjku hizi, wasabato wengi wanashindwa, including myself, huko vijijijini kwetu kweli hayoyanafanyika.
.. mambo ya youth organisations yapo madhehebumengi, kwa hiyo pathfinders, adventist youth na mengineyo sidhani kama yanamfanya mtu asipende kuishi na msabato.
.. kutengeneza nywele, nakuomba angalau uje kanisani siku moja uone jinsi gani wanawake wanavyojiremba, it's natural that a woman must look pretty, and our women aren't exceptional. Wanajiremba, wanatengeneza nywele, japo hawatogi masikio.
 
Hata nami siwezi olewa na msabato; na ukizingatia mapenzi ya siku hizi unajifunza kumpenda mtu, so kigezo cha compatibility kwenye Imani ni muhimu. And for you guys huwa mnatuona wakatoliki ni waovu kuliko shetani mwenyewe; kiasi kwamba vita yenu na ukatoliki ingehamia kwa shetani, mbigu ingekuwa yenu.

Ushauri wangu, tafuta mchumba kanisani kwenu. Issue ya kupigwa hakuna mdada anavumilia hivyo jua the moment unalift Mkono kumpiga mtu ni sawa na kumpa talaka plus jela.

Dada Kaunga, wasabato hawana itikadi yoyote mbaya, ni imani tu iliyojengeka kwenu kwamba dini yetu ya kizamani, haiko compatible na madhehebu mengine, we see u catholics like any other, we respect u but differ in the way we understand bible, biblia ni very complicated kitabu, everyone has his own way of understanding it.

Jaribu msabato and u will never regret.
 
salaam wanajamvi,
Leo nimeamua kuandika kuelezea umma namna udini na ukabila ulivyojengeka nchini, hususani katika mapenzi. Mimi ni mhandisi mhitimu wa chuo kikuu nina miaka 28. Mara ya kwanza kujihusisha na mahusiano ilikua mwaka 2006, wakati huo nikiwa form 6. Nakumbuka ilikua Dodoma, nilipokutana na mpenzi wangu huyo wa kwanza katika maisha yangu. Tulipendana sana, na tuliwekeana malengo na mipango mingi ambayo kwa asilimia kubwa tuliweza kkuitimiza.
Matatizo yalianza kuzuka mwaka 2007 huyu binti alipoenda chuo kusoma na mimi nikachagua kufanya kazi kwanza, kampuni flani hivi ya madini. Vikaanza visa kila kukicha , japo nilijaribu kumtimizia kila alichohitaji.....hatimaye aliamua nimwaga rasmi mwaka 2009
Nakumbuka nilimwaga machozi na kuchanganyikiwa. wakati huo nilikua nimejiunga na chuo , niko mwaka wa kwanza.... tulikua katika mitihani...nilifeli karibu nusu ya mitihani yote. ilinichukua miaka miwili kusahau kidogo kilichotokea.
Binafsi, sikuweza kuanzisha mahusiano na binti yoyote kwa kua katika nafsi yangu nilikua nampenda x wangu tu. wapo waliojaribu kunitega, relationships zingine zilivunjika ndani ya usiku mmoja.
Wakati nakaribia kumaliza mwaka wangu wa mwisho chuoni, mpenzi wangu wa zamani alirudisha mawasiliano na akanieleza sababu zilizosababisha aniache. akaniamabia ni kwa kua mimi ni mtu wa musoma , kwao sikubaliki. ati kuna dada yake aliwahi kupata mchumba mtu wa msoma akamsumbua sana, tangu siku hiyo ikawa nongwa kwao. sababu ingine akaniambia pia kwa kua mimi ni msabato.... ati kwao wasabato wanawachukulia kama walokole na wenye imani kali. akaniambia yuko tayari kurudiana na mimi iwapo tu nitaamua kubadili dini na kua mkatoliki kama yeye... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi kadhaa, nilikutana tena na binti wa kichaga... mwanachuo, mhandisi wa fani sawa na yangu. katika urafiki wetu uliodumu kama miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
uchungu niliopata siku hiyo siwezi simulia...nakumbuka nilienda slip way nikasimama na kushangaa bahari huku machozi yananitoka kwa zaidi ya masaa 6...
dini yangu, kabila langu imekua jinamizi kwangu.....nakereka zaidi na kauli kua nisubiri wangu anakuja.
nawashauri wote ambao mnabagua kwa udini na ukabila muache hizo mambo.. mnaumiza sana wengine. mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth:

Kwanini wewe umekuwa mbaguzi kwa watu wa musoma na wasabato kiasi hicho?. Yaani mpaka unasema hutopenda tena kisa hao marafiki wa wili waliokukataa?. Wewe ndo mbaguzi mkubwa, tena mkubwa zaid ya hao mabinti!. Usiwatenge wasabato wenzio, sifa waliyopewa ni yao. Usiwatenge wa musoma wenzio.hukutaka kubadili dini basi tafta msabato. Umeambiwa watu wa musoma wababe basi uwe mnyenyekevu au pendekeza mu msoma mwenzio
 
sikitiko sikitiko penzi na dini hakika havipingani
bora kupishana elimu ila si imani ya dini
sishauri msababto kuoa msabato ila moyoni amani inaleta
 
Sijaona ubaya hao wapenzi wako kukwambia ukweli, kwanza wameelezea vikwazo vya penzi kati yako na wenyewe.

Ukweli ni uhuru.

Endelea kuwalaumu maana hata wewe hujaamua kuyapatia tiba matatizo yako,tafuta msabato pia mkurya yanini shida'
Kwani Wakurya wanatoka Musoma? wacha kuropoka.
 
Pole sana kaka yangu.
Ni changamoto ambazo wengi tunazipitia siku hata siku but kumbuka MKE MWEMA MTU HUPEWA NA MUNGU. Naamini unalifahamu hilo, so be patient kaka yangu.
 
salaam wanajamvi,
Leo nimeamua kuandika kuelezea umma namna udini na ukabila ulivyojengeka nchini, hususani katika mapenzi. Mimi ni mhandisi mhitimu wa chuo kikuu nina miaka 28. Mara ya kwanza kujihusisha na mahusiano ilikua mwaka 2006, wakati huo nikiwa form 6. Nakumbuka ilikua Dodoma, nilipokutana na mpenzi wangu huyo wa kwanza katika maisha yangu. Tulipendana sana, na tuliwekeana malengo na mipango mingi ambayo kwa asilimia kubwa tuliweza kkuitimiza.
Matatizo yalianza kuzuka mwaka 2007 huyu binti alipoenda chuo kusoma na mimi nikachagua kufanya kazi kwanza, kampuni flani hivi ya madini. Vikaanza visa kila kukicha , japo nilijaribu kumtimizia kila alichohitaji.....hatimaye aliamua nimwaga rasmi mwaka 2009
Nakumbuka nilimwaga machozi na kuchanganyikiwa. wakati huo nilikua nimejiunga na chuo , niko mwaka wa kwanza.... tulikua katika mitihani...nilifeli karibu nusu ya mitihani yote. ilinichukua miaka miwili kusahau kidogo kilichotokea.
Binafsi, sikuweza kuanzisha mahusiano na binti yoyote kwa kua katika nafsi yangu nilikua nampenda x wangu tu. wapo waliojaribu kunitega, relationships zingine zilivunjika ndani ya usiku mmoja.
Wakati nakaribia kumaliza mwaka wangu wa mwisho chuoni, mpenzi wangu wa zamani alirudisha mawasiliano na akanieleza sababu zilizosababisha aniache. akaniamabia ni kwa kua mimi ni mtu wa musoma , kwao sikubaliki. ati kuna dada yake aliwahi kupata mchumba mtu wa msoma akamsumbua sana, tangu siku hiyo ikawa nongwa kwao. sababu ingine akaniambia pia kwa kua mimi ni msabato.... ati kwao wasabato wanawachukulia kama walokole na wenye imani kali. akaniambia yuko tayari kurudiana na mimi iwapo tu nitaamua kubadili dini na kua mkatoliki kama yeye... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi kadhaa, nilikutana tena na binti wa kichaga... mwanachuo, mhandisi wa fani sawa na yangu. katika urafiki wetu uliodumu kama miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
uchungu niliopata siku hiyo siwezi simulia...nakumbuka nilienda slip way nikasimama na kushangaa bahari huku machozi yananitoka kwa zaidi ya masaa 6...
dini yangu, kabila langu imekua jinamizi kwangu.....nakereka zaidi na kauli kua nisubiri wangu anakuja.
nawashauri wote ambao mnabagua kwa udini na ukabila muache hizo mambo.. mnaumiza sana wengine. mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth:

Tatizo ninaloliona kwako ni kuwa bado hujakuwa na uzoefu wala ujuzi (experience) wa kutosha wa kuanzia kutongoza mpaka ya kudili na wanawake bado. Moja ya sifa za mwanaume mwenye uzoefu ni kuweza ku take control ya relationship yako.
Bahati mbaya zaidi ni kuwa aina ya wasichana unaokutana nao ni wasichana wajanja (au unaweza waita watoto wa mjini) ambao mara moja wanakuwa wamekusoma udhaifu wako. Wewe Kaa chini ujiulize kwa makini sana kumbe kabila lako na dini yako ni tatizo (vitu ambavyo naamini unawafahamisha mara tu baada ya kuanza mahusiano yenu na si mwisho🙂.
Sasa jiulize hivi; Wao huwa wanangoja na kufurahia nini na wewe siku zooote hizo mpaka pale inapofikia Mzee mzima unapomwaga ajenda ya kuchukua mzigo jumla jumla ndio wao wanakuwa wanaanza kupangua majeshi🙂. Hapa naweza kuamini tu kuwa labda kinachowaweka ni kuwa unahonga sana tu maana hizo ndio sifa za watu wa Musoma🙂. Hivyo kwa muktasari tu ni kwamba umekuwa zile aina ya relationship ambazo wamarekani wanaita FWB - yaani Friendship with Benefit (au ita mambo ya Fezwa🙂 huku wewe binafsi ukiamini kuwa ni "mapenzi". Na ndio maana pale unapotaka kuchange gia na wao wanachange gia kupitia sababu dhaifu kwa mtu ambaye tayari wanamjua ni dhaifu na kuishilia mbali.

Hivyo ni sawa mwanaume uko kwenye relationship na mwanamke anayekuhonga mahela au zawadi kedekedei au una enjoy tu sex yake (wanaume tunasema umepata mahala pa kuponea🙂 lakini ili hali moyoni mwako humpendi kabisa kuwa mpenzi wake wala kuwa mke wako hata kwa dakika tatu🙂. Halafu mwisho wa siku awe king'ang'anizi wa kudai ndoa na wewe si utamtemela mbali huko aishie🙂. kwa hiyo ndiyo kesi yako bwana.

Lakini bado kijana mdogo take your time kuwafahamu vema wasichana unaokutana nao. Uliza maswali magumu toka mwanzoni kabisa kuwa (What are they looking for in terms of relationship) naamini bado wapo wasichana waaminifu ambao wako tayari wala hawana vya kuchezeana akili na kutoa visingizio vya kuhuni.

Mwisho kwa taarifa yako tu ni kwamba mimi leo hata nikiingia mahala kama Zanzibar au Pemba bado ninaopoa mpenzi japo dini yangu wala kabila langu wala lafidhi yangu havifanani kabisa na watu wa pande za huko kabisa. Lakini ndio mwanaume lazima uwe mjanja na mwenye kujiamni na kuweza kutake a control of your relationship🙂
 
Back
Top Bottom