Naanzisha maombi binafsi kwa ajili ya Simba,Nawashauri Simba hivi

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,663
2,000
Mimi Ni Mtanzania,Mimi Ni mpenzi au shabiki wa Simba tokea nimezaliwa ila Ni mshabiki muoga,huwa naumwa Sana Simba ikicheza mechi nzito.

Kuanzia leo naanzisha maombi maalum kuiombea Simba ishinde mechi zake zote zikizobaki,maana yake ichukue kombe.

Kwa sisi waombaji na kwenye ulimwengu wa roho hakuna kinachoshindikana mbele za Mungu.

Mungu aliwahi kufanya Yale ambayo kwa macho ya binadamu hayawezekani kwa Mungu yaliwezekana.

Naanza Leo kuiombea Simba ivuke vikwazo vyote kabla ya mechi zake zote zikizobaki,kwa sababu usione kimya Kuna hila nyingi zinafanywa ili Simba itoke mapema kabisa ili timu zenye hofu na Simba zipate nafuu.
Kuna fitina nje ya uwanja ambapo Kuna kila namna haramu hasa kwa hizi timu zenye uzoefu na fainali, nyingi zaidi hizi za kaskazini, na Mambo mengine Kama hayo,ntaomba Simba ivuke yote.

Pia ntaomba Simba icheze vizuri kwa kupata ushindi kila mechi dhidi ya wapinzani wake,na Simba iibuke mshindi Hadi ichukue Kombe,ntaomba.

Ushauri,
Kuhusu ushauri Sina Shaka najua Simba ina wabobevu,lakini kuonesha mchango wangu hata mdogo tune kama punje ya vumbi,Nawashauri Hivi kwa Sasa Simba ichukulieni kila mechi Kama fainali.

Isifikiriwe kuwa mnakutana na mshindi wa pili basi ni kibonde, hapana.
Al Ahly Ni mshindi wa pili je Ni kibonde?

Kila timu iliyofuzu robo fainali iko na uzito sawa .
Mfano Al Ahly tulimfunga kwetu nae akajatufunga kwao.
Hivyo mshindi wa pili yoyote baada ya kuingia robo fainali lazima atacheza kufa na kupona,na wengine confidence zimepanda baada ya kuingia robo fainali.

Simba Sasa klabu bingwa ndio imeanza Ni ama zao ama zetu.

Simba itakua imeogopwa Sana hivyo kila timu itakayokutana nayo itapigana Hadi tone la mwisho ya damu.
Kwa hiyo mkae mkijua mmepaniwa Sana au kila timu inaiangalia Simba kwa tahadhari ya Hali ya juu.wengi hawatamani kukutana na Simba mapema,lakini wakikutana kila hila kila mbinu itatumika.

Hivyo Omni langu kwenu ichukulieni kila mechi kwenu Ni fainali.

Haya Ni maoni ya Mshabiki wenu,ninaimani na benchi la ufundi najua mnajua zaidi yangu,lakini Dua haikataliwi.

Sasa naingia kwenye maombi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom