Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kukaa mwezi mzima bila ya Baraza la Mawaziri na alipotokea kutangaza baraza lenyewe akaacha Wizara nne bila ya Mawaziri ila aliweza kuwapata Manaibu wake. Siku moja baada ya kuapishwa kwake Rais Magufuli akaenda Wizara ya fedha na kukagua Mahudhurio ya wafanyakazi. Tangu hapo serikali yetu kwa sasa imekuwa ni ya kuviziana!
Alipokwenda Muhimbili wengine tulihoji mantiki ya kwenda kule, Maana matatizo ya Muhimbili kama ikifikia yatatuliwe na Rais maana yake Serikali nzima chini yake imeshindwa kufanya hivyo. Lakini yale matatizo yameendelea kuwepo na yataendelea kuwepo kwa kuwa chanzo au kiini cha matatizo yenye hakijashughulikiwa!
Lakini watanzania walikuwa wamechoshwa sana na hali ya ulegevu wa serikali iliyopita, kiasi kwamba kauli mbiu ya "Hapa Kazi" iliwavutia hasa pale walipoona mtoa kauli mwenyewe anapiga "Push Ups" majukwaani. Lakini matatizo yetu haya tuliyonayo hayatatatuliwa kwa mitulinga bali kwa kutumia akili. Hizi "Ziara za Ghafla" "Kufunga mageti" au "kuvamia" ni maonesha ya nguvu walizonazo watawala wetu, lakini si njia mujarabu za kuelekea kwenye lengo la kuwa na serikali Imara na taifa linalojitegemea!!
Kwa mfano tatizo la wagonjwa kulala chini Muhimbili halikuwa ni la vitanda bali aina ya huduma zinazotolewa huko wanakotoka hao wagonjwa wanaolala chini. Kama wagonjwa wote wanaokwenda kwenye Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, za Mikoa na Hospitali za Rufaa za Kanda madaktari wanawaandikia wagonjwa waende Muhimbili kupimwa kwa kuwa huko tuu ndiko kwenye CT Scan na MRI basi bila shaka kulala chini kutaendelea mpaka pale vifaa hivyo vitakapokuwa kwenye ngazi za wilaya na Mkoa!!
Huu ni mfano mmoja tu ambao unaonesha kwamba hii staili ya kuviziana ambayo
Ben Saanane ameiita "Slack Management" haina tija hata kidogo, ni staili ya kutaka wengine waumbuke na wengine waonekane ni wachapa kazi, itatuvuruga tu wala haitatutoa hapa tulipo. Kama tunataka kuendelea nayo Muasisi wake bado yupo, tumpe kazi na ataifanya kwa ufanisi sana. Augustine Lyatonga Mrema!![
Huna jipya
/QUOTE]