Naanza kuiona haja ya "semina elekezi"

Naanza kuiona haja ya "semina elekezi"

Badala ya watu kuwaza kutekeleza wajibu wao wanakuja kulialia humu jf ili waendelee kuchelewa kazini. Eti anavizia! Kwani mgonjwa anapoenda hospitali huwa anampigia simu Daktari? Kwa hiyo Dr, nae aseme wagonjwa wanamvizia maana wanaenda bila taarifa? Fanya kazi acha mazoea ya kuchekewachekewa bila sababu za msingi.
 
Sisi wengine yote hayo yanayoendelea solution yake tuliiona kupitia wizara ya ofisi ya raisi utawala bora (ambayo sasa imekuwa combined) na alitakiwa pale amuweke mtu anaelewa mambo ya management mbona kuna ripoti nyingi sana za wataalamu kutoka UDSM wakiongelea system za Tanzania ambazo shule tosha kwanini wasichaguliwe watu kama hao ambao ni technocrat wajue wanaanzia wapi kwanza kusafisha kuliko kumpa wizara Simbachawene kama alikuwa na umuhimu wa kuwa waziri basi wangeiacha utawala bora pekee kwanza ili kubadilisha mifumo swala ambalo ni muhimu.

Hakuna mtu asiyeoona taka zimejaa barabarani wakati manispaa inakusanya kodi luluki (sanasana kwenye business centres kama masokoni), hakuna mtu asiyejua hospitalini manesi wanabivuri au sehemu za kazi ni chafu, hakuna mtu asiyejua wafanyakazi wa serikari ni wavivu na sehemu zingine wanyanyasaji kwa raia wasio na uwezo kuanzia uwanja wa ndege mpaka polisi, hakuna mtu asiyejua sehemu nyingi perfomances zake ziko chini ya quality even with their limited budget, hakuna mtu ambaye akusikia vilio vya wakulima kucheweleweshewa malipo yao au kuzuiwa kuudha bidhaa zao sehemu wanazotaka, hakuna mtu ambaye ajasikia kodi za SUMATRA na halamashauri wanazojitungia na mengineo mengi.

Ukiyajumlisha yote haya kiini chake ni menejimenti either kuanzia wizarani au hizo sehemu wanazofanya kazi; hivi ungekuwa mshahara wa mfanyakazi umeugawa kwa masaa, ana clock in kabla ya kazi na analipwa kwa masaa ya kazi mwisho wa siku wangapi wangechelewa kazini kiolela, kungekuwa na government set of targets za sera ambazo zinataka mifumo ya management by objective ambapo mashirika yanafanya appraisals za strategy zao na wafanyakazi wao kama wanaweza kufanya kazi kwa malengo ya serikari wangapi wangekuwa washatimuliwa si ndio ingekuwa namna rahisi ya kujua uwezo wa viongozi wa ngazi zote kuanzia juu mpaka chini.

Sasa mara huyu anataka kwenda kukamua sijui majipu ya vyeti, huyu anataka watu wafanye hivi etcetera wakati kwa jicho la kitaaluma tatizo ni serikari, makatibu wakuu, managers mengine ni matokeo ya juu tu if anything ilitakiwa kulazimilisha wabadilike wao kwanza, watoe proposals wadai mifumo kutoka kwa managers at all levels kila kitu kita kaa sawa chenyewe kwakuwa wanaweza kukipima kwa merit za expectations zao.

Kwa sasa kinachoendelea ni yale yale yaliyomo ndani ya tatizo la management zetu ambalo ni uwezo mdogo wa kutafuta solution (Utoh kalisema sana hili kama tatizo kwenye taasisi za seriakri zinazppolekea kila aina ya ubadhirifu na poor performances hivi atujiulizi inawezekana vipi watu wakalipwa mishahara hewa na kuna wataalamu wa management ambao sehemu ya degree zao wamesomea maswala ya kuzuia ubadhirifu).
 
Mkuu kutafuta umaarufu kwa maslahi ya umma / kwa njia halali ni jambo zuri tu. Tambua kuwa shughuli zetu wanadamu za kila siku ni kutafuta umaarufu.Kwa mfano Ronaldo yule mchezaji mpira wa miguu wa timu ya Real Madrid anajitahidi kucheza vizuri na kufunga madoli ili apate umaarufu.Mwalimu anayeundisha vizuri darasani na kufaulisha wanafunzi wengi kwenye mitihani anatafuta umaarufu. Mfanya biashara anayejibidiisha ili apate faida kubwa na kuwa tajiri anatafuta umaarufu.Mwanajeshi anayepigana vita kwa uhodari na kuwezesha upande wake kushinda naye anatafuta umaarufu jeshini. Hii ni mifano michache tu. Kwahiyo kwangu mimi kila mtu anatakiwa atende jambo linalomhusu kwa weledi na bidii kubwa ili atafute na kupata umaarufu wenye faida kwenye jamii yake anayoishi ndipo tutakapoendelea.Tusiogope kutenda mambo mema na makubwa yenye faida kwa jamii yetu kwa kuhofu kuwa tutaambiwa tunatafuta umaarufu.
 
Mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamepanic, tena wamepanic vibaya, na matokeo ya kupanic huko wanafanya maamuzi ya kukurupuka na yanayovunja haki za bunadamu. Mara huyu kawatia ndani watendaji (Kinondoni), mara huyu kawalazimisha watu kufanya kazi bila likizo(Moshi), mara huyu kawalazimisha watendaji kukaa chini kwenye darasa lenye vumbi eti ili wajue watoto wakikaa inakuwaje (Lorya), kila kukicha ziara za kushtukiza ambazo mwisho wake hatuambiwi zime achieve nini (tena Dar peke yake)

Mara huyu kawafungia watumishi geti, Yaani ni fujo na sifa tu.

Kimsingi kauli ya Mh Rais kuwa wateuliwa wake watajielekeza wenyewe inaleta vurugu huku maofisini. Hawa waheshimiwa wameshindwa kuelewa maana ya 'HAPA KAZI TU' na kimsingi kila mtu ana tafsiri yake.

Bila semina elekezi tutayashuhudia mengi .
Kwakweli nimeanza kuona umuhimu wa Dkt. Magufuli kuwapa hawa wateuliwa wake semina elekezi, ili wajue ideology hii ya Mh Rais utekelezaji wake unaendaje

Nawasilisha

We ndiyo umegundua leo? Nilishaandika sana hapa. Magufuri alipaswa kupunguza gharama za semina elekezi na siyo kutokufanya kabisa. If you find "Education" expensive try ignorance. JPM is trying ignorance.
 
Naunga mkono mmoja hoja, upande wa pili kuna maeneo yametembelewa kwa mtindo huohuo na hakukua na matatizo na hakuna aliyewajibishwa.
Kama watu wanatimiza wajibu wao hao waviziaji wataonekana vituko, lakini hali halisi ikoje?
 
Kuna watu ni Kama shimo la kuzimu lilialo 'Nipe Nipe Nipe' nimesema hivi kutokana na watu kutwa kulalamika kwenye mitandao tena kwa kauli ambazo waliwahi kuzilalamikia. Nitatoa mifano kidogo ya kauli hizo:-

1. "TZ ILI ISONGE MBELE TUNAHITAJI RAIS DIKTETA..." Leo.."RAIS MAGUFULI NI DIKTETA ANAKIUKA HAKI ZA BINADAMU"

2. "KAZI YA URAIS AU UWAZIRI HAISOMEWI PESA ZA SEMINA ELEKEZI ZIKAHUDUMIE JAMII" Leo.. "BWANA MKUU NI KAMA KIRANJA MKUU HATAKI KUELEKEZA WENZIE"

3. "WATANZANIA NI WAVIVU SANA WANAHITAJI KIONGOZI MKALI" leo..."KIONGOZI FULANI AMEZIDI" nk

Hili ni tumbo la kuzimu lilialo nipe nipe nipe.... Kamwe haliwezi kutosheka..

Queen Esther

Mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamepanic, tena wamepanic vibaya, na matokeo ya kupanic huko wanafanya maamuzi ya kukurupuka na yanayovunja haki za bunadamu.

Mara huyu kawatia ndani watendaji (Kinondoni), mara huyu kawalazimisha watu kufanya kazi bila likizo(Moshi), mara huyu kawalazimisha watendaji kukaa chini kwenye darasa lenye vumbi eti ili wajue watoto wakikaa inakuwaje (Rorya), kila kukicha ziara za kushtukiza ambazo mwisho wake hatuambiwi zime achieve nini (tena Dar peke yake)

Mara huyu kawafungia watumishi geti, Yaani ni fujo na sifa tu.

Kimsingi kauli ya Mh Rais kuwa wateuliwa wake watajielekeza wenyewe inaleta vurugu huku maofisini. Hawa waheshimiwa wameshindwa kuelewa maana ya 'HAPA KAZI TU' na kimsingi kila mtu ana tafsiri yake.

Bila semina elekezi tutayashuhudia mengi.

Kwa kweli nimeanza kuona umuhimu wa Dkt. Magufuli kuwapa hawa wateuliwa wake semina elekezi, ili wajue ideology hii ya
Mh Rais utekelezaji wake unaendaje..

Nawasilisha..
 
NAUNGA MKONO HOJA maana huko tuendako serikali itapelekwa mahakamani kwa kuvunja haki za binadamu kwa misifa misifa REFERENCE SAMAKI WA MAGUFULI ZILIITIA HASARA SERIKALI ndivyo itakavyokuwa kwa sasa kwa hii tabia ya kukurupuka bila faida
 
Kweli waTanzania mapopoma! Sijui nani amewaloga? Sio nyie mnanalamika kuwa pesa ya serikali inaliwa kwa vitu visivo na tija!

Kweli leo mnataka semina elekezi za nini? Hakuna Haja, Ummy, Mahiga, Muhogo na wengine wote wameshapata mafunzo na experience ya kutosha wao wawafundishe wenzao!

Acheni kutafuta njia za kula pesa ya serikali!!!
 
Mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamepanic, tena wamepanic vibaya, na matokeo ya kupanic huko wanafanya maamuzi ya kukurupuka na yanayovunja haki za bunadamu.

Mara huyu kawatia ndani watendaji (Kinondoni), mara huyu kawalazimisha watu kufanya kazi bila likizo(Moshi), mara huyu kawalazimisha watendaji kukaa chini kwenye darasa lenye vumbi eti ili wajue watoto wakikaa inakuwaje (Rorya), kila kukicha ziara za kushtukiza ambazo mwisho wake hatuambiwi zime achieve nini (tena Dar peke yake)

Mara huyu kawafungia watumishi geti, Yaani ni fujo na sifa tu.

Kimsingi kauli ya Mh Rais kuwa wateuliwa wake watajielekeza wenyewe inaleta vurugu huku maofisini. Hawa waheshimiwa wameshindwa kuelewa maana ya 'HAPA KAZI TU' na kimsingi kila mtu ana tafsiri yake.

Bila semina elekezi tutayashuhudia mengi.

Kwa kweli nimeanza kuona umuhimu wa Dkt. Magufuli kuwapa hawa wateuliwa wake semina elekezi, ili wajue ideology hii ya
Mh Rais utekelezaji wake unaendaje..

Nawasilisha..

hivi semina elekezi unaelekezwa nini usicho kijua haswa? Kama ni waziri wa Maji au nishati na madini au afya n.k hawajuimatatizo yanayo wakabili wananchi? Hivi kweli kila waziri hajui mipaka ya majukumu yake? Hawana sera?? . Kama kuna waziri yeyote atakaye fanya upuuzi au kuharibu kwa kisingizio cha kutopewa Semina Elekezi basi huyo anafaa kuwajibishwa na atakuwa ameshindwa kazi.
 
Mwanzo mgumu ila tutazoea, maana tulibweteka Sana. Sasa mnapatashida kwenda na hii kasi
 
siku hizi kila mtu mtaalamu wa kila kitu.............................
 
Mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamepanic, tena wamepanic vibaya, na matokeo ya kupanic huko wanafanya maamuzi ya kukurupuka na yanayovunja haki za bunadamu.

Mara huyu kawatia ndani watendaji (Kinondoni), mara huyu kawalazimisha watu kufanya kazi bila likizo(Moshi), mara huyu kawalazimisha watendaji kukaa chini kwenye darasa lenye vumbi eti ili wajue watoto wakikaa inakuwaje (Rorya), kila kukicha ziara za kushtukiza ambazo mwisho wake hatuambiwi zime achieve nini (tena Dar peke yake)

Mara huyu kawafungia watumishi geti, Yaani ni fujo na sifa tu.

Kimsingi kauli ya Mh Rais kuwa wateuliwa wake watajielekeza wenyewe inaleta vurugu huku maofisini. Hawa waheshimiwa wameshindwa kuelewa maana ya 'HAPA KAZI TU' na kimsingi kila mtu ana tafsiri yake.

Bila semina elekezi tutayashuhudia mengi.

Kwa kweli nimeanza kuona umuhimu wa Dkt. Magufuli kuwapa hawa wateuliwa wake semina elekezi, ili wajue ideology hii ya
Mh Rais utekelezaji wake unaendaje..

Nawasilisha..

Ni management by and with crisis.
lakini usisahau hao wakuu wa wiwili ni waalimu ambao wanadhani namna ya kiutendaji ni wa shule tena zile shule tulizosoma mwalimu na viboka na black book etc
Maadam una ametures ni muhimu kuwapa some kind of orientation. mkulu asiwe mbanifu sana alegeze pale kwenye manufaa.
 
mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamepanic, tena wamepanic vibaya, na matokeo ya kupanic huko wanafanya maamuzi ya kukurupuka na yanayovunja haki za bunadamu.

mara huyu kawatia ndani watendaji (kinondoni), mara huyu kawalazimisha watu kufanya kazi bila likizo(moshi), mara huyu kawalazimisha watendaji kukaa chini kwenye darasa lenye vumbi eti ili wajue watoto wakikaa inakuwaje (rorya), kila kukicha ziara za kushtukiza ambazo mwisho wake hatuambiwi zime achieve nini (tena dar peke yake)

mara huyu kawafungia watumishi geti, yaani ni fujo na sifa tu.

kimsingi kauli ya mh rais kuwa wateuliwa wake watajielekeza wenyewe inaleta vurugu huku maofisini. Hawa waheshimiwa wameshindwa kuelewa maana ya 'hapa kazi tu' na kimsingi kila mtu ana tafsiri yake.

Bila semina elekezi tutayashuhudia mengi.

kwa kweli nimeanza kuona umuhimu wa dkt. Magufuli kuwapa hawa wateuliwa wake semina elekezi, ili wajue ideology hii ya
mh rais utekelezaji wake unaendaje..

nawasilisha..

elimu elimu elimu elimu elimu elimu elimu

Nilipiga kampeni ya magufuli mpaka kaingia ikulu lakini tangu akanyage ardhi ya magogoni najutaaaaa!
 
Mwanzo mgumu ila tutazoea, maana tulibweteka Sana. Sasa mnapatashida kwenda na hii kasi

Serikali ya Magu itapewa Semina elekezi itakapofikishwa Mahakamani kwa kuvunja Haki za Binadamu na hata kuvunja Katiba! Hizo 1.3trilion zitaishia kulipa fidia wahanga!
 
Back
Top Bottom