Naamini naweza kuikosoa Serikali bila hofu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Pamoja na malalamiko mengi, bado tafiti zinaonesha kuwa katika kila watu 10 hapa nchini, 6 wanaamini wanaweza kuikosoa Serikali liyopo madarakani bila hofu kuliko serikali iliyopita.

Ajabu lakini ni kweli! Unaweza kudhani ukosoaji unaminywa lakini bado si kwa kiwango cha kutisha..

Utafiti unaonesha asilimia 60% ya Watanzania bado wanaamini wanaweza kuikosoa serikali inapofanya makosa bila hiyana.

Unasemaje?!

1.JPG
 
hujatekwa bado... subiri yakukute uone kama utakuja na hoja yako tena..!!!!
endelea kuamini ila usithubutu kufanya hayo unayoamini...
 
Huu ni utafiti uliofanywa kabla ya September 2016 au ni mimi sijaelewa?
 
Huu ni utafiti uliofanywa kabla ya September 2016 au ni mimi sijaelewa?
Naam, sijaona utafiti mpya. Nasubiri kusikia utasemaje japo naamini hautakuwa na tofauti kubwa na huu!
 
Siamini ukikosoa kiheshima bila matusi utapata matatizo. Wengi wanakosoa kwa mihemko ambayo kiubinadamu si sahihi. Utafiti upo sahihi
Kuna watu wanadhani matusi na kukosa heshima ndio ukosoaji sahihi. Hata mimi unipe ushauri kwa kunisimanga na kunidharau siuchukui!
 
Kuna watu wanaamini matusi na kukosa heshima ndio ukosoaji sahihi. Hata mimi unipe ushauri kwa kunisimanga na kunidharau siuchukui!
Natamani anionyeshe matusi ya Askofu Niwemugizi (?) na yule Askofu mwingine. Natamani mtu anionyeshe matusi ya Ben Saanane.
 
Naam, sijaona utafiti mpya. Nasubiri kusikia utasemaje japo naamini hautakuwa na tofauti kubwa na huu!
Kama hicho kijarida kimetolewa sep 2016 na mpaka March 2018 hakuna kingine kipya ina maanisha utafiti unaweza kuwa ulianza kabla hata ya Oct 2015.

Kumbuka kipindi hicho vurugu mechi zilikuwa hazijaanza na yule mtakatifu sana alikuwa bado anasoma mchezo na wakati huo akiandaa wasaidizi wake watakaoweza kumsujudu kwa kila atakachokisema
 
kukosoa inaruhusiwa iwapo tu utakua na faini milioni 15 kama ITV,
 
Kama hicho kijarida kimetolewa sep 2016 na mpaka March 2018 hakuna kingine kipya ina maanisha utafiti unaweza kuwa ulianza kabla hata ya Oct 2015.

Kumbuka kipindi hicho vurugu mechi zilikuwa hazijaanza na yule mtakatifu sana alikuwa bado anasoma mchezo na wakati huo akiandaa wasaidizi wake watakaoweza kumsujudu kwa kila atakachokisema
Kosoa kwa adabu!
 
Pamoja na malalamiko mengi, bado tafiti zinaonesha kuwa katika kila watu 10 hapa nchini, 6 wanaamini wanaweza kuikosoa Serikali liyopo madarakani bila hofu kuliko serikali iliyopita.

Ajabu lakini ni kweli! Unaweza kudhani ukosoaji unaminywa lakini bado si kwa kiwango cha kutisha..

Utafiti unaonesha asilimia 60% ya Watanzania bado wanaamini wanaweza kuikosoa serikali inapofanya makosa bila hiyana.

Unasemaje?!

View attachment 725472
Wewe punguani kweli kweli. Unatuletea takwimu za miaka 2 iliyopita kuaminisha watu kuwa uhuru wa kukosoa upo? Watu kama Tundu Lissu majeraha hayajapona wewe unaleta porojo. Pika zingine uzilete. Na mzungu mbelgiji ameshawakana na taarifa zenu za kipuuzi za kughushi.
 
Back
Top Bottom