Naamini hapa ndio pa kuponea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naamini hapa ndio pa kuponea

Discussion in 'JF Doctor' started by elimumali, Dec 16, 2011.

 1. elimumali

  elimumali Senior Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapa jamvini napaamini sana ndipo pa kupata miongozo yote, ndipo pa kuponea.

  Nina ndugu yangu wa karibu sana, mjamzito ana upungufu wa damu (8.3) na yuko mwezi wa nane sasa, hivyo bado wiki nne tu ajifungue. Anatakiwa awe na 11.5 ndio salama.

  Wataalam wa madawa nifahamisheni:
  1. Atumie dawa gani/chakula gani ili damu yake iongezeke haraka (wiki 4)
  2. Hivi sasa dawa anazotumia ni HB Tone (vidonge), juice ya rozela na matembere. Kuna mtu kanishauri atumie Hemovit. Je, ipi nzuri zaidi kati ya HB Tone na Hemovit (ya maji?
  3. Vidonge na dawa ya maji ipi inafanya kazi haraka zaidi au nzuri zaidi?
  4. Hivi, ni kweli Beet root kwa mja mzito ina utata kutokana na reaction yake ya kutoa sumu mwilini?

  Natanguliza Shukrani.
   
 2. elimumali

  elimumali Senior Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jingine, Lozi (Almond) naweza kuipata wapi? Nasikia pia inasaidia. Mzizi Mkavu, please help.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Japo umepotea njia ila jitahidi sana na juisi ya rozela ona namna ya kutengeneza:
  JUISI YA KUONGEZA DAMU
  JINSI YA KUTENGENEZA
  1. CHEMSHA MAJI GLASS KUBWA 12 MPAKA YACHEMKE
  2. YATOE KWENYE MOTO WEKA CHINI
  3. WEKA MAJANI MEKUNDU KIGANJA KIMOJA NA NUSU
  4. KAA DAKIKA 20
  5. CHUJA
  6. WEKA KWENYE GLASS
  7.8. WEKA SUKARI KIJIKO CHA CHAI KIMOJA KAMA UNATUMIA SUKARI
  9. TAYARI KWA KUNYWA.

  nawakilisha.


   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  dawa ya kijani na kijanja ndio nini mamdenyi..
   
 5. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Juice ya rozela na matembere ndiyo suruhisho la haraka ILA KUMBUKA MATEMBELE ASILE TU KAMA MBOGA BALI CHUKUA MATEMBELE OSHA WEKA JIKONI NA MAJI KIDOGO SANA YAKICHEMKA MARA YA KWANZA TU TOA JIKONI NA KAMUA MCHUZI WAKE ANYWE.FANYA HIVYO ASUBUHI NA JIONI AU ZAIDI.Atumie Hemovit ya maji ni nzuri.Hilo tatizo lilisha mkuta my wife mwaka huu but God is good.Matembele ni faster damu kibao.
   
 6. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kijanja =Kiganja kuhusu dawa ya kijani naomba atoe maelezo mhusika.Kumbuka kuedit mada yako kitufe cha edit kipo kwa ajiri yako.
   
 7. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  You are right broda!!!!!!!!
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Pole sana,kwani hakupewa vidonge vya Iron?Mimi nakumbuka pia nilikuwa na damu 8 kwenye hiyo hiyo miezi,Nilipewa vidonge vya iron,nilikunywa marozera mpaka nafanyiwa C section nilikuwa na 11
   
 9. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Pia asitumie madawa bila ushauri wa Dr
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Caution, ili rozela i-retain minerals zake including iron inapaswa isiwekwe kwenye maji ya moto yaliyokwenye metalic vessel, metalic utensils kama bakuri au sufuria ya bati au chuma yana react na active metals zilizoko kwenye rozela solution hivyo kuifanya remaining juice kuwa makapi yasiyo na nutritional value
   
 11. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mpeleke Hospitali haraka sana. JF siyo hospitali
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  samahani, nilimaanisha mlonge, lakini nimeedit najua kupata mlonge mzuri siyo kazi ndogo.
  sorry for that.
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  JF doctor pls.
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  majani mekundu ndiyo Rosela au?
   
 15. The FaMa

  The FaMa Senior Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pole Mkuu, ukichukua ushauri uliopewa hapa na ukienda kuwaona madaktari bingwa wa akina mama utapata suluhisho kamili. Usimsahau na Mwenyezi Mungu pia.
   
 16. elimumali

  elimumali Senior Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Thanks Bakuza Nashukuru kwa maelekezo yako.
   
 17. elimumali

  elimumali Senior Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante sana, ni kweli Mungu ndio wa kwanza katika yote. Nimeamini kuwa matatizo huwaweka watu karibu na Mungu. Yaani hata kama ulimsahau, yakikukuta utakuwa naye kichwani kwako masaa yote. Thanks
   
 18. elimumali

  elimumali Senior Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asanteni sana wapendwa, Bakuza, Mamndenyi, Fe lady, The Fama, Ulimakafu, Baba Collings n.k. kwa mchango wenu. Ni kweli kabisa hapa JF panafaa sana kutafuta ushauri. Licha ya kupata ushauri wa kukusaidia pia unafarijika sana. Mwita25 amini hapa pia panaweza kuitwa hospitali, kwani idea unazopata hapa zinasaidia kutibu, na Doctors pia wamo humu humu. Nawashukuru sana, na naomba muendelee hivi hivi.
   
 19. elimumali

  elimumali Senior Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Very useful information. Asante sana mkuu, tutakuwa makini na vyombo vya chuma.
   
 20. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  anza kutumia dozi zilizoelekezwa na wadau hapo juu. JK
   
Loading...