Naam, Makonda tena anachallenge status Quo!

Naam, Makonda tena anachallenge status Quo!

foleni
maji
hospital/madawa
umeme
barabara za ndani
mipango miji
ufisadi
majitaka
uchafu
taa za barabarani
sehemu za wazi kupumzika na kubadilisha hewa ya jiji
barabara kuu za jiji
sharia za barabarabi
ajira
watoto/wazee mitaani
madawa ya kulevya
.........
.....
ongezea zako
Huyu rc haja tatua hata moja ktk list hii uliyoiweka
 
Baada ya kubadilisha mfumo wa PF3 sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar amekuja na nyingine nayo ni kuhakikisha kila Mtaa wa Dar yetu unakuwa na majina rasmi pmj na namba za nyumba, amesema anawaagiza Wakuu wa Serikali za Mitaa wote kulifanyia kazi hilo swala ili Barua ziwe zinaltwa majumbani mwetu na Posta badala ya kwenda kufwata mwenyewe Kijitonyama au Posta!

Big Up Makonda only sky is the limit man!!!
Endelea kujiuliza maswali kuna mambo mengi sana tunafanya kwa mazoea tu lkn siyo ya lazima na tunaweza kuyabadilisha!

DSCF2294%2B-%2BCopy.jpg
Manzese sijui kama itawezekana
 
foleni
maji
hospital/madawa
umeme
barabara za ndani
mipango miji
ufisadi
majitaka
uchafu
taa za barabarani
sehemu za wazi kupumzika na kubadilisha hewa ya jiji
barabara kuu za jiji
sharia za barabarabi
ajira
watoto/wazee mitaani
madawa ya kulevya
.........
.....
ongezea zako
Hayo yote hana uwezo nayo
 
Hii project posta waliianza siku nyingi tangu 2010 siyo makonda ni posta wenyewe msitafute sifa IPO arusha pia Na itaendelea Tanzania mzima
Makonda anatafuta kick kwenye miradi ya watu
 
Hakuna aliyesema kwamba Mkuu wa Mkoa ndiyo ameanzisha bali amepokea kijiti kama yalivyo mambo mengi kama siyo yote hata Raisi Magufuli hakuna aliloanzisha bali anaendeleza yale ambayo watangulizi wake waliyaanzisha na ndiyo maana wanasema kupokezana kijiti ndiyo maana yake, hivyo Mkuu wa Mkoa Makonda kwa upande wake amesema ili kulifanikisha hilo atasimamia Mitaa yote iwe na Majina na namba za nyumba!
Hivi ile project yake ya kuwashonea walimu uniform iliishia wapi?
1459909771423.jpg
 
Apokee kijiti makonda ni mkuu Wa posta acheni sifa sifa wanatakiwa wapewe shirika la posta wenyewe siyo makonda dar Na arusha project inakaribia kumalizika itaendelea tanga morogoro mtwara lindi Na mwanza kwa mujibu Wa posta sifa hizi ni za shirika la posta kwa kuleta huu mfumo mzuri Na wanataka kuweka mpaka map kama Google map kwa akili ya kuwafikia wateja wao kiurahisi
Asante sana mkuu kwa kutupatia ukweli maana hao jamaa wana tabia ya kuvuna wasicho panda
 
Usiwe mgumu kuelewa namna hiyo, siyo kazi ya Posta kutoa majina ya mitaa na namba za nyumba bali ni kazi ya Serikali za Mitaa pamoja na Jiji la Dar na ndiyo maana Posta wenyewe ndiyo waliomulika Mkuu wa Dar!
Hapo makonda hana anapo husika,mwambie amalizie project ya kuwasafirisha walimu bure
 
Kwa hiyo makonda ndio atatoa Namba za nyumba Tanzania mzima wewe ungewapongeza shirika la posta kwenye hili siyo makonda haya mashirika pia yanahitaji kupongezwa yakifanya vitu vizuri pia yanaendeshwa Na watanzania wenzetu nao wanahitaji motisha
Salute mkuu
 
Hivi huwa huna kazi ya kufanya masaa yote nikuandika utumbo wako humu si uende kambini ili server za jf zipumue
Huyu jamaa tangu jk awaombee zile nafasi 46 kutoka kwa magu,basi yeye ila siku ni kupost kusifu watumishi wa ccm tu
 
foleni
maji
hospital/madawa
umeme
barabara za ndani
mipango miji
ufisadi
majitaka
uchafu
taa za barabarani
sehemu za wazi kupumzika na kubadilisha hewa ya jiji
barabara kuu za jiji
sharia za barabarabi
ajira
watoto/wazee mitaani
madawa ya kulevya
.........
.....
ongezea zako
Anaanza na alichikiona yeye kwanza wewe unayako maybe ukipata nafasi unaweza anza na lolote
 
Halafu huyu jamaa anawadanganya watu wasio jielewa tu kiufupi ni kwamba ili barua ziwe zinawafikia watu nyumbani badala ya kutumia sanduku LA barua inabidi serikali ianzishe mfumo wa area codes ambao unaitaji nyumba zote kusajiliwa kuyagawa maeneo ktk mfumo huo,ni suala linalohusu wizara inayohusika na mipango miji si la mkuu wa mkoa na jambo ilo sio geni nimepata kulisikia kipindi cha mama anna tibaijuka alipata kulizungimzia kwamba lilikuwa kwenye mchakato kabla hajangolewa na kashfa ya escrow
Mkuu mtu aliyezoea kubebwa siku zote lazima alazimishe kubebwa tu
 
Tatizo kubwa walilonalo wanasiasa hasa wetu ni kwamba hawazijui nambari, wanazipenda tu na hasa kusomesha wananachi wao hizo nambari. Na ndio maana moja kati ya msemo wanaoupenda ni, "wataisoma namba"

Kibiashara, hilo haliwezekani ndani ya Tanzania yetu hii ya sasa hivi, sijui huko mbele tunakokwenda. Hatuna mila ya kutumiana parcels kwa kutumia postal service au courier, hii imechangiwa zaidi kutokana na tabia ya wizi kwa baadhi ya watumishi wa taasisi zetu huko siku za nyuma. Sasa ikiwa kuna batua tano zinazokwenda Mbagala zinazolipiwa Tsh 2,000 kila moja kwa jumla ya Tsh 10,000, huyu mfanyakazi unamlipa kiasi gani, mafuta ya piki piki kiasi gani, na gharama nyengine ni kiasi gani? Ziko kampuni ndogo ndogo zinafanya kazi hii siku hizi lakini kwa kutegemea zaidi wafanya biashara na ikumbukwe hixi kampuni binafsi wana uwezo mkubwa wa kudhibiti gharama za matumizi na ufanisi na idadi ya wafanyakazi, sii taasisi za serikali yetu ambazo tunasikia zinalipia pango kwa Bilioni 600 kwa mwaka.

Ushauri wangu kwa wahusika ni kuwa wangewapatia sanduku za posta serikali za mtaa ili wananchi wawe wanatumia hiyo sanduku ya posta na serikali ya mtaa iwe inachukuwa hizo barua/kifurushi kutoka posta na kuvisambaza kila siku, kwa mafao ambayo watakubaliana na shirika la posta.
 
Back
Top Bottom