Naacha ualimu, nimechoka dharau

Mwalimu S

Member
Sep 20, 2015
41
33
Ndugu wadau: Najua humu ndani kuna watu tofauti wanachuo,watumishi na hata wanafunz...mm nizungumzie hii idara ya UALIMU licha ya kudharaulika kwa mishahara duni na mazingira mabovu ya kazi dharau imepitiliza mpaka walimu kupigwa makofi hadharani inaniuma sana si tu kwa ujinga wa huyu jamaa aliyepigwa Bali hata hii kada imekaa kudharaulika sijawahi kusika kama kuna Daktari kapigwa au Mhasibu lakin ni miaka ya juzi tu walimu walikula bakora hadharani na mkuu wa wilaya...kwa dharau hizi walimu wasitegemee kama kuna Siku watatekelezewa madai yao ...mmeyataka wenyewe bakini wenyewe kwenye kada yenu
 
Kuacha kaz sio ufumbuzi wa tatizo,tafuta ufumbuz kwann wawapige walimu na sio idara nyingine.
vipo vyombo vya sheria ambayo ni msaada mkubwa kwako.
 
Ndugu wadau: Najua humu ndani kuna watu tofauti wanachuo,watumishi na hata wanafunz...mm nizungumzie hii idara ya UALIMU licha ya kudharaulika kwa mishahara duni na mazingira mabovu ya kazi dharau imepitiliza mpaka walimu kupigwa makofi hadharani inaniuma sana si tu kwa ujinga wa huyu jamaa aliyepigwa Bali hata hii kada imekaa kudharaulika sijawahi kusika kama kuna Daktari kapigwa au Mhasibu lakin ni miaka ya juzi tu walimu walikula bakora hadharani na mkuu wa wilaya...kwa dharau hizi walimu wasitegemee kama kuna Siku watatekelezewa madai yao ...mmeyataka wenyewe bakini wenyewe kwenye kada yenu
Uliomba KAZI ukapata KAZI unaona KAZI kufanya KAZI sasa acha KAZI uone tabu ya kutokuwa na KAZI.
 
Tafadhali teacher!
Wanafunzi wanakuhitaji sana rudi darasani mkuu!
Hayo mengine ni ajali kazini tu
 
Punguza hasira na jazba Mkuu, hasira na jazba huwa zinatoa majibu yasiyo sahihi.
Kaa chini utulie kisha tathimini bila kutazama kilichotokea juu ya kupigwa kwa huyo mwalimu, Je hii kazi yako inalipa? Kama unaona hailipi tafuta nyingine.
Ila hata mimi naishangaa serikali kwa kutokuwajali walimu aiseee!!!
 
Ndugu wadau: Najua humu ndani kuna watu tofauti wanachuo,watumishi na hata wanafunz...mm nizungumzie hii idara ya UALIMU licha ya kudharaulika kwa mishahara duni na mazingira mabovu ya kazi dharau imepitiliza mpaka walimu kupigwa makofi hadharani inaniuma sana si tu kwa ujinga wa huyu jamaa aliyepigwa Bali hata hii kada imekaa kudharaulika sijawahi kusika kama kuna Daktari kapigwa au Mhasibu lakin ni miaka ya juzi tu walimu walikula bakora hadharani na mkuu wa wilaya...kwa dharau hizi walimu wasitegemee kama kuna Siku watatekelezewa madai yao ...mmeyataka wenyewe bakini wenyewe kwenye kada yenu
Hadhi ya mwalimu itapandishwa na mwalimu mwenyewe katika utekelezaji wa majukumu yake kitaaluma, ukikimbia wewe ni dhaifu... Ndio maana unadharaulika, washauri na wengine wenye mtazamo kama wako (mamluki) muondoke wote ili tubaki walimu halisi na tusiojua kulalamika ili tutatue kero kama hizo unazoziita dharau kwa kuzingatia nidhamu ya taaluma yetu
 
Hakuna nidhamu penye woga. Acha nidhamu ya woga. Kama mngekuwa na uwezo wa kutatua hizo kero si mngekuwa mshazimaliza. Acha kuishi kitumwa wewe eboo
 
Utumwa.. Nidhamu ya uoga, ndivyo hupelekea kukimbia nyumba yako, uliyoujenga mwenyewe kwa muda mrefu, acha fikra mgando, tafuta njia sahihi za kuitawala nyumba yako, akili ndogo hujenga hoja dhaifu kama hii yako
 
Ualimu ni kaz ambayo serikali imeifanya kua low profile job. Thats y inaonekana sio kaz nzuri (kaz ya dharau).

Otherwise sion tatizo na hiyo kazi mkuu we tafuta pa kwenda kabla ya kuacha ili ufanye job uipendayo
 
Kama ualimu utaendelea kuwa kimbilio la waliofeli basi ualimu utazidi kudharaulika labda serikali ichuje watu wenye sifa za kuwa walimu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom