Na Post

Na Post

sab

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
5,744
Reaction score
4,354
Nimeipost kama nilivyoipokea

"Mzee hiyo ni kweli wala sio utani. Kuna mzee mtu mzima sana aliniambia wanaume huwa hatujitambui.

Hela ya chakula unamkabidhi mama chumbani. Mama anatoka na kapu ananunua chakula anapika anawaambia watoto wanangu njooni mle nimewapikia chakula kitamu. watoto wanasema asante mama.

Hela ya nguo za sikukuu unamkabidhi mama chumbani. Kesho yake mama anatoka anaenda dukani kununua nguo.

Akirudi anawaambia watoto wanangu nimewaletea nguo za sikukuu njooni mjipime. Eee wanangu mmependeza sana. Si mnaona ninavyowapenda ee, ndio mama.

Ukifika wakati wa ada unamkabidhi mama ada chumbani. Asubuhi akiamka wanangu naenda kuwalipia ada zenu za shule.

Akirudi nimeshawalipia ada zenu ee, gari ya shule kesho itawapitia. Asante mama.

Mtoto akikosa mama yeye hatoi adhabu anawaambia watoto ngoja baba yenu aje.

Ukirudi unaelezwa unachukua bakora unaaaza kuchapa usijue ndio unazidi kuleta uhusiano mbaya na watoto.

Ukifika uzeeni sasa watoto hawana kumbu kumbu yeyote nzuri kwako. Tuwe makini .

mahitaji tukabidhi adharani. mama na watoto waone. Ushauri wa
bure."


*Wanawake Mungu anawaona jamani*
 
Sikuzote saa ya kula baba hayuko nyumbani, watoto wanaona baba anavyofunikiwa mapaja ya kuku wakati wao wanagawana vipapatio
 
  • Thanks
Reactions: sab
Pamoja na hilo, mama jenga mahusiano bora kwa familia
Nijenge mahusiano wakati mkiingia tu ndani mnasahau kuwa nyumba ina watoto. Matoy mnaona ni uchafu, mnawagombeza watoto waache kelele unaangalia mpira. Baba akirudi nyumba inakuwa jela
 
  • Thanks
Reactions: sab
Nijenge mahusiano wakati mkiingia tu ndani mnasahau kuwa nyumba ina watoto. Matoy mnaona ni uchafu, mnawagombeza watoto waache kelele unaangalia mpira. Baba akirudi nyumba inakuwa jela
Hayo ndio madhara yakutojenga mahusiano bora
 
Nimeipost kama nilivyoipokea

"Mzee hiyo ni kweli wala sio utani. Kuna mzee mtu mzima sana aliniambia wanaume huwa hatujitambui.

Hela ya chakula unamkabidhi mama chumbani. Mama anatoka na kapu ananunua chakula anapika anawaambia watoto wanangu njooni mle nimewapikia chakula kitamu. watoto wanasema asante mama.

Hela ya nguo za sikukuu unamkabidhi mama chumbani. Kesho yake mama anatoka anaenda dukani kununua nguo.

Akirudi anawaambia watoto wanangu nimewaletea nguo za sikukuu njooni mjipime. Eee wanangu mmependeza sana. Si mnaona ninavyowapenda ee, ndio mama.

Ukifika wakati wa ada unamkabidhi mama ada chumbani. Asubuhi akiamka wanangu naenda kuwalipia ada zenu za shule.

Akirudi nimeshawalipia ada zenu ee, gari ya shule kesho itawapitia. Asante mama.

Mtoto akikosa mama yeye hatoi adhabu anawaambia watoto ngoja baba yenu aje.

Ukirudi unaelezwa unachukua bakora unaaaza kuchapa usijue ndio unazidi kuleta uhusiano mbaya na watoto.

Ukifika uzeeni sasa watoto hawana kumbu kumbu yeyote nzuri kwako. Tuwe makini .

mahitaji tukabidhi adharani. mama na watoto waone. Ushauri wa
bure."


*Wanawake Mungu anawaona jamani*


AISEEE HIYO KITU NIKO NAYO MAKINI SANA. KUNA TYM NAMNUNULIA MWANANGU VITU NA KUMPELEKEA MWENYEWE. AMEKARIRI HADI NGUO NA VIATU NILIVYOMNUNULIA.

WANAUME TUWE MAKINI
 
  • Thanks
Reactions: sab
AISEEE HIYO KITU NIKO NAYO MAKINI SANA. KUNA TYM NAMNUNULIA MWANANGU VITU NA KUMPELEKEA MWENYEWE. AMEKARIRI HADI NGUO NA VIATU NILIVYOMNUNULIA.

WANAUME TUWE MAKINI
Big up mkuu kwenye chama la wana
 
Back
Top Bottom