Na imani wengi mmeboreka leo kama mimi..................

ntakuvunjia heshima biggy ujue, afu na nyumbani nisije kabisa na usinitafute........

Usiseme hivyo mamushka. Kichague chama chetu. Kipe nafasi.
Chagua CCM, chagua Kikwete!
 
Kwani kuna la kushangaza kwa huyu Bwana mipasho?? Yaani mikono ilikuwa inanyanyuliwa kama vile anasutana kule uswazi!!! Kuna aliyekwisha wahi ona wanawake wanasutana uswahilini? Nilishikwa na butwaa!!! Poleni TUCTA!
 
jamani hebu tuongelee ule ukweli kuhusu hizo hela

suppose wewe nikama mimi ninaechukua kima cha chizi sorry cha chini 104000 kumbuka no allowance ninaishi ubungo nina familia ya watu wanne kila mtu ale robo kilo

1. nauli kwenda na kurudi nyumbani 600@day 26days 15600/=
2. kula mchana kazini 1000@day 26days 26000/=
3. mchele mlo mmoja 1kg 1000@kg 30days 30000/=
4.chai na mkate asubuhi 1000@day 30days 30000/=
5.watoto 2 shule nauli 400@day 26days 10400/=
6.watoto 2 kula mchana shule 500@day 26days 13000/=
7. Umeme 10000 10000/=
8. maji 3000 3000/=
9.kodi vyumba 2 30000@month 30000/=
10. mkaa gunia moja 22000@mwezi 22000/=
11. mboga 1000@day 30days 30000/=
Jumla 220,000/=

hiyo ni experiancxe ya maisha ninayoishi na mke wangu na watoto wangu kima cha chini hakitoshi kabisa ndio maana wakati mwingine inabidi kutoroka kazini kwenda kufanya na biashara zako nyingine ili maisha yaende. ilitakiwa Kikwete atuombe samahani na kutumia lugha nzuri kwani tunateseka mno kumbuka hapo hakuna dharura FL1 akikutembelea inabidi asinywe soda kwani ataharibu bajeti. mtoto au wewe ukiumwa ukinunua dawa inabidi upige mahesebu ya kufidia hiyo ndiyo hali halisi ya maisha yetu bongo. Sijajua kwanini wale wazee walikuwa wanapiga makofi pale.
JK kapitiliza kuwa hataki kura zetu je kama wafanyakazi 350000 wakakataa kumchagua na kuwashawashi ndugu zaoi kama 10 hivi kwa kuwapa mifano kuwa maisha yanakuwa magumu kwa ajili yake baba kaka mjomba bibi babu na wengineo je ni wangapi wataacha kumpigia kura kwa kweli ile hutuba haikustahili kuwa na jeuri ile. muda umefika sasa wa kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani ni bora kujaribu upande mwingine kwani wamekuwa na jeuri sana na kufikiri hii nchi ni yao pekee. Hivi hela za uchaguzi bilioni tano kwa kila mgombea urais na tuna vyama kama 20 hivi wamezitoa wapi? hapo ni maraisi tu hujaongeza na wabunge na madiwani ndugu zangu tuache ushabiki wa kichama tuangalie hali halisi kama nilivyoorodhesha matumizi yangu kwa mwezi mmoja hapo juu. hapo sijaweka dhararura kama kuumwa kuna msiba au harusi ya rafiki yangu. Hivi hata hiyo kazi nitafanya kwa moyo kweli. kugoma tuache lakini haitoshi tuwatoe madarakani wababaishaji kuanzia wabunge wababaisha hata raisi na kubadili upepo. Leo hii mbunge anapewa kiinua mgogongo millioni 60/= baada ya miaka mitano mwakani anakuwa tena bungeni baada ya miaka 5 milioni 60 tena ndio si anastaafu kipindi kimeisha je ni kiasi gani kitapotea
nawasilisha hii kwa uchungu mno tena mno kutukanwa kwa viongozi wa Tucta ni kama tumetukanwa wafanyakazi wote

naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom