Mzungu aumbuka!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Nikiwa kazini katika kampuni ya ujenzi barabara hapa mjini iringa nilishuhudia kihoja hiki.Kampuni ya Interbeton baada ya kupata hasara kubwa kutokana na wizi wa mafuta,imeamua kuajiri wazungu ili kudhibiti wizi wa mafuta.

Basi bwana,tukiwa site alikatiza jamaa mmoja akiendesha baiskeli yake huku akiwa amepakia dumu kubwa taaratib akitokea Tanangozi kwenda Iringa mjini. Mzungu kuona lile dumu,akawasha hardbody yake na kumfukuzia yule bwana akidhani ni mwizi wa mafuta.

Alipomfikia,akafunga breki kali sana mbele ya mwenda kwa baiskeli, akashuka bila hata ya kuzima gari vizuri,akamvaa mnyalu wa watu na kufungua mfuniko wa lile dumu.

Looh! Kumbe lile lilikuwa limejaa ulanzi,na kwa sababu ulanzi wenyewe ulitembezwa juani muda mrefu,alipofungua tu,ulanzi wote ulifoka juu kama champagne na kumchafua mzungu wa watu sura yote na shati lake lote.

Sikufuatilia zaidi kama yule mzungu alimlipa yule mnyalu hasara ya ulanzi uliomwagika.
 
Unanikumbusha wizi wa mafuta uliokuwa unafanyika kwenye barabara ya Namanga-Arusha ulisababisha wachina wapige kung fu wezi wa mafuta na wizi ukapungua kidogo
 
Unanikumbusha wizi wa
mafuta uliokuwa unafanyika kwenye barabara ya Namanga-Arusha
ulisababisha wachina wapige kung fu wezi wa mafuta na wizi ukapungua
kidogo

shy kuna mchina alishtakiwa kwa kumburuta kibarua akiwa kamfunga nyuma ya pick up! kesu sijui iliishaje!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom