Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Wana JF,
Nimeona ni muhimu kupost thread hii ya kusikitisha kuhusu mwanafunzi wa kigeni aliyevamiwa na kuchomwa visu UDSM juzi.
Kitendo hiki kimetokea katika taasisi nyeti ya elimu, mahali ambapo wanafunzi wengi wa kigeni hufika kila mwaka kwa vipindi tofauti kupitia exchange programme baina ya vyuo mbalimbali duniani kikiwemo UDSM.
Zaidi sana tukio hili limetokea mahali ambapo kuna kitengo maalumu cha ulinzi na usalama katika kampasi (auxilliary police) ambao wanawajibika kuwalinda wanafunzi na wafanyakazi.
Je, wahalifu hao wanapitapita je na kuwafikia wanachuo tena katika vyumba vyao?
Mzungu apigwa visu Jijini
2008-10-22 18:23:23
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Mzungu mmoja wa kike ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amejikuta akijeruhiwa mwilini baada ya kupigwa visu viwili na mtu aliyemvamia chumbani kwake kwa nia ya kumpora kompyuta yake ndogo `laptop`, pesa na vitu vyake vingine kadhaa vya thamani.
Tukio hilo la kusikitisha, linadaiwa kutokea mishale ya saa 6:00 mchana juzi, pale kwenye jengo la hosteli mojawapo ya kampasi ya Mlimani, lijulikanalo kama `Hall Three` almaarufu kama Extension Block, chumba namba 792.
Imedaiwa kuwa mdada huyo ni wa Kimarekani na anatoka LCCT Group na yuko chuoni hapo kupitia mpango wa ubadilishanaji wanafunzi (exchange programme).
Mashuhuda wamedai kuwa mtasha huyo amekutwa na masahibu hayo juzi wakati akiwa chumbani mwake.
Wanadai baadhi ya mashuhuda kuwa, katika mida hiyo ya mchana, binti huyo alistukia amevamiwa na jamaa mmoja aliyeshikilia bisu na kujaribu kumtisha ili ampatie fedha na vitu vingine alivyokuwa navyo.
Inadaiwa kuwa baada ya kuona hivyo, mdada huyo wa Kizungu akakataa kutii amri kabla ya kuanza kupambana na lijamaa hilo lililokuwa na bisu kubwa, akitumia ujuzi wa kareti na judo alioupata kwao kwa nia ya kujilinda na mashambulizi kama hayo.
``Palitokea purukushani kali... mwanadada alipambana vilivyo na kumfanya mporaji ashindwe kutimiza dhamira yake.
Hata hivyo, tayari mwanadada wa watu alishachomwa kisu sehemu za kichwani na mkononi kabla ya kuwahishwa katika zahanti ya chuo na kutibiwa,`` akasema mmoja wa watu waliodai kuwepo katika eneo la tukio.
Hata hivyo, imeelezwa zaidi kuwa cha kusikitisha, licha ya askari wa chuoni hapo almaarufu kama `auxillary police` kuwepo muda wote kwa ajili ya ulinzi, bado lijamaa hilo lenye kisu liliweza kutokomea kusikojulikana na kumuacha dada wa watu akiendelea kutaabika na majeraha aliyoyapata.
Mwandishi hakuweza kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuelezea tukio hilo baada ya asubuhi ya leo kushindwa kumpata kwenye simu yake ya mkononi.
Hata hivyo, jitihada za kupata maelezo zaidi toka kwa uongozi wa chuo hicho kuhusiana na usalama wa wanafunzi wake wakiwemo hao wa Kizungu na mali zao, zinaendelea kulindwa.
Aidha, imedaiwa na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo kuwa hivi sasa, matukio ya wanafunzi wa Kizungu kuvamiwa ndani ya vyumba vyao na kuporwa pesa na mali yamekuwa ya kawaida na kwamba cha kusikitisha, hakuna hatua zozote zinazoonekana kuchukuliwa.
``Hii si mara ya kwanza... wanafunzi hawa wa Kizungu ambao hulipa pesa nyingi za Kigeni, wamekuwa wakiandamwa mara kwa mara na vibaka.
Wezi huvamia vyumba vyao na kuiba mchana kweupe, tena nje ya jengo kukiwa na askari wa chuo walio na sare na silaha za moto... inasikitisha sana,`` akasema mmoja wa wanafunzi waliozungumza na mwandishi wa habari hii.
SOURCE: ALASIRI