Mzungu afukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau Waafrika!

Mdogo wangu Preta, kama wakumbuka hii skendo kwa kuwepo enzi hizo, basi kumbe nawe wa long time, umri wako zaidi ya Uhuru wa Tanganyika!!!!!

ni kweli mpendwa.....uhuru ukija mimi nilikuwa nauona....enzi hizo viongozi walikuwa wanawaheshimu wananchi na kuwatumikia.....
 
Kama Preta ulikuwepo enzi za marehemu Walwa akiwa RC huko kaskazini basi ni lazima sasa umekuwa kijeba!!Kumbuka hili ni gazeti la mwaka 1962. Tukifanya makisio kama unaweza kukumbuka skendo hii lazima ulikuwa umekwisha vunja ungo hivyo unaweza ukawa ulikuwa na miaka 18, sasa hivi kwa rehema za Mwenyzi mungu unadunda miaka 67!! Hongera sana kwani life expectancy ya Mtanzania imeshuka mpaka miaka 40 tu kwasababu ya viongozi mafisadi!!

asante sana....na bado nina afya njema nategemea kuishi miaka 25 zaidi.....
 
asante sana....na bado nina afya njema nategemea kuishi miaka 25 zaidi.....

Mungu ayasikie maombi yako ili utabili wako wa kuishi miaka mingine 25 utimie; hata hivyo tafadhali tuambie na sisi siri ya kuwa na maisha marefu yenye afya tele. Ningeshukuru kama utatuambia vitu ambavyo huvitumii katika maisha yako.
 
asante sana....na bado nina afya njema nategemea kuishi miaka 25 zaidi.....

Heshima kwako Preta na Mungu akuzidishie zaidi ya hyo miaka uloiongezea,sisi vijana tuna changamoto nyingi sana kwa hyo kufikia umri huo ni kuendelea kumuomba Mungu zaidi
 
Heshima kwako Preta na Mungu akuzidishie zaidi ya hyo miaka uloiongezea,sisi vijana tuna changamoto nyingi sana kwa hyo kufikia umri huo ni kuendelea kumuomba Mungu zaidi

vijana wa sasa mna mambo mengi sana....enzi zetu ukisikia mtu amekufa tena kijana au mtoto mkoa mzima na wa jirani wanashtuka....lakini leo hii ni kawaida.....
 
Mungu ayasikie maombi yako ili utabili wako wa kuishi miaka mingine 25 utimie; hata hivyo tafadhali tuambie na sisi siri ya kuwa na maisha marefu yenye afya tele. Ningeshukuru kama utatuambia vitu ambavyo huvitumii katika maisha yako.

watu wa siku hizi mna mabobish sana.....life style yenu wenyewe ndio inayowamaliza.....
 
dah...gazeti la long tym sana....nakumbuka hii skendo....wakati huo huyu bwana duka lake lilikuwa pale karibu na Tanganyika Arms....

asante,kumbe wewe Preta wa long time, nilidhani kasichana ka baada ya vita ya kagera. Hongera!
 
bora wazungu,kuna hawa wahindi wana dharau mno,wameiweka dola mfukoni,hawakamatwi,wanakwepa kodi,wananyanyasa wafanyakazi wa ndani,hawawalipi vibarua.yaani wahindi ni kero nyingine inayosumbua nchi.
 
vijana wa sasa mna mambo mengi sana....enzi zetu ukisikia mtu amekufa tena kijana au mtoto mkoa mzima na wa jirani wanashtuka....lakini leo hii ni kawaida.....

Mie nikuite mama mkubwa,sasa c ungetupa mbinu au njia zipi mlizokua mnatumia hata katika kula vyakula maana cku hizi utaona tunajinenepea hovyo,vyakula vipi mlikua/unakula labda?
 
kumbuka kuna Waziri wa awamu ya tatu alizuiwa kuingia hoteli fulani,naye [mzungu] hakujua kama yule ni Minister. Waziri alichemsha,jamaa aliendelea na biashara zake!sina hakika kama aliacha ubaguzi ama la..

Mnaongelea ya zamani hivyo?
Hivi miaka ya juzi kati - mwanzoni mwa miaka ya 2000,
Mzungu wa KADCO alimkatalia waziri kutumia VIP Lounge KIA!
LOL....JEURI WANAYO HAWA WATU

Angalizo: Tokeo hili lilichapishwa kwenye gazeti la Mwafrika 1962. Swali je hivi leo, ambapo viongozi wetu wanawakumbatia wawekezaji, kuna yeyote kati yao anayeweza kufikia maamuzi kama haya?

Mwafrika, Jumatatu Oktoba 29, 1962

MZUNGU mwingine ambae ni Meneja wa kampuni ya kuuza dawa, Arusha Bw. R. Bawley ameamriwa aihame Tanganyika, Mzungu huyo amepewa saa 48 tu kufanya hivyo.

Ripoti iliyopokelewa jana na gazeti hili ni kwamba Bwana Bawley alionekana akiondoka na matokaa kuelekea Kenya.

Sababu za kufukuzwa Mzungu huyo ni ufedhuli na kuwadharau Waafrika.

Mwandishi wetu akizungumza na na Regional Commissiner wa Jimbo la Kaskazini, Bwana P. Walwa jana alijulishwa kwamba jambo hilo alilihakikisha yeye mwenyewe alipofukuzwa na Meneja huyo.

Bwana Walwa alipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu ufedhuli wa meneja huyo. Watu wengine walisema kwamba huwafukuza watu dukani kwake au kuwatupia fedha wakinunua vitu.

Bwana Walwa alikwenda katika duka hilo ili ahakikishe mwenyewe kabla ya kuchukua hatua na kwenda kufika Bawley akamwambia 'nenda zako'.

Hapo Bwana Walwa alitoka na kutoa habari hizi kwa polisi.

Radhi yakataliwa:

Asubuhi yake Meneja huyo alikwenda kuomba radhi akisema hakujua kuwa yule aliyemfukuza alikuwa Regional Commssioner.

Bwana Walwa alikataa kumsamehe kwa sababu, alisema 'dharau ile ilifanyiwa Waafrika wote'.

Bwana Walwa alimwambia mwandishi wetu hiyo jana kwamba yeye alitembelea jimbo lote akiwaonya watu waheshimiane. Aliona si haki
wengine waachiwe kufanya dharau.

Bawley sasa ni Mzungu wa sita kuondolewa kwa visa kama hivyo tangu nchi hii ipate uhuru wake.

Nazitamani sana nyakati hizo,heshima yetu ililindwa ipasavyo.
 
Mie nikuite mama mkubwa,sasa c ungetupa mbinu au njia zipi mlizokua mnatumia hata katika kula vyakula maana cku hizi utaona tunajinenepea hovyo,vyakula vipi mlikua/unakula labda?

tulikuwa tunakula vyakula nachurale....sio hivi vyenu vyenye madawa lukuki.....sato walikuwa wanavuliwa na nyavu....sio hawa wenu mpaka wavuliwe na baruti...sijui sumu.....ukimkuta sato pale chakula barafu ni mkubwa anakulingana.......

Back
Top Bottom