Mzungu afukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau Waafrika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzungu afukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau Waafrika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Askari Kanzu, Dec 26, 2011.

 1. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Angalizo: Tokeo hili lilichapishwa kwenye gazeti la Mwafrika 1962. Swali je hivi leo, ambapo viongozi wetu wanawakumbatia wawekezaji, kuna yeyote kati yao anayeweza kufikia maamuzi kama haya?

  Mwafrika, Jumatatu Oktoba 29, 1962


  MZUNGU mwingine ambae ni Meneja wa kampuni ya kuuza dawa, Arusha Bw. R. Bawley ameamriwa aihame Tanganyika, Mzungu huyo amepewa saa 48 tu kufanya hivyo.

  Ripoti iliyopokelewa jana na gazeti hili ni kwamba Bwana Bawley alionekana akiondoka na matokaa kuelekea Kenya.

  Sababu za kufukuzwa Mzungu huyo ni ufedhuli na kuwadharau Waafrika.

  Mwandishi wetu akizungumza na na Regional Commissiner wa Jimbo la Kaskazini, Bwana P. Walwa jana alijulishwa kwamba jambo hilo alilihakikisha yeye mwenyewe alipofukuzwa na Meneja huyo.

  Bwana Walwa alipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu ufedhuli wa meneja huyo. Watu wengine walisema kwamba huwafukuza watu dukani kwake au kuwatupia fedha wakinunua vitu.

  Bwana Walwa alikwenda katika duka hilo ili ahakikishe mwenyewe kabla ya kuchukua hatua na kwenda kufika Bawley akamwambia 'nenda zako'.

  Hapo Bwana Walwa alitoka na kutoa habari hizi kwa polisi.

  Radhi yakataliwa:

  Asubuhi yake Meneja huyo alikwenda kuomba radhi akisema hakujua kuwa yule aliyemfukuza alikuwa Regional Commssioner.

  Bwana Walwa alikataa kumsamehe kwa sababu, alisema 'dharau ile ilifanyiwa Waafrika wote'.

  Bwana Walwa alimwambia mwandishi wetu hiyo jana kwamba yeye alitembelea jimbo lote akiwaonya watu waheshimiane. Aliona si haki
  wengine waachiwe kufanya dharau.

  Bawley sasa ni Mzungu wa sita kuondolewa kwa visa kama hivyo tangu nchi hii ipate uhuru wake.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  dah...gazeti la long tym sana....nakumbuka hii skendo....wakati huo huyu bwana duka lake lilikuwa pale karibu na Tanganyika Arms....
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nikisimuliwa nchi hii ilivyokua zamani na ilivyo sasa, ni masikitiko makubwa.
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Tunachangia wenyewe hali hii kwa kuwaona mafisadi kama wajanja, tunataka maendeleo ya harakaharaka yasiyofanana na vipato.Inapelekea kufanya maamuzi mabaya yenye kujala ubinafsi. Wengi wetu tunawajua ndugu,marafiki wanaofanya mf. TRA na kujenga makasri kwa njia zisizo halali lakini tunawasifia. Vita dhidi ya ufisadi inabidi vianzie kwenye ngazi ya familia.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama na weusi nao wangekuwa wanafukuzwa hivi Ulaya si tungelia ubaguzi
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Waafrika wengi tu wanafukuzwa kila kukicha, japo si kwa ufedhuli.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,424
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  kwani huyu mzungu kwa nini kafukuzwa? fanya ujinga huko ulaya ukione cha moto
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,424
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  natamani huu uongozi ungekuwepo kipindi hiki uende ukasafisa wazungu wanaotuonea kila kukicha huko migodini..
  sema sasa hivi huu uongozi wa JK legelege kina FF ndio washauri wa raisi
   
 9. Mlamoto

  Mlamoto JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kuwa mfuatiliaji mzuri! Weusi wanafukuzwa mno! Mwishoni mwa miaka ya tisini weusi kwa mamia waliokuwa Ufaransa walikimbilia kanisani walipotaka kufukuzwa, bado wakafukuzwa kwa nguvu na kwa ukatili, na ikazua vurugu kubwa mno! Siyo Ufaransa tu, Urusi na Ujerumani weusi wanaishi kwa uoga wa kuuwawa kila sekunde, na nchi nyingi za wenzetu sisi ni garbage tu mbele zao. Go back to your history.
   
 10. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  iko poa sana
   
 11. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mdogo wangu Preta, kama wakumbuka hii skendo kwa kuwepo enzi hizo, basi kumbe nawe wa long time, umri wako zaidi ya Uhuru wa Tanganyika!!!!!
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mh! Unakumbuka au umesimuliwa?
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Siku hizi hakuna kiongozi anayeweza kuthubutu kumfukuza mzungu hata afanye ufedhuli wa aina gani.
   
 14. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hapo tu,ndiyo nilipokuwa namkubali Nyerere
   
 15. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kumbuka kuna Waziri wa awamu ya tatu alizuiwa kuingia hoteli fulani,naye [mzungu] hakujua kama yule ni Minister. Waziri alichemsha,jamaa aliendelea na biashara zake!sina hakika kama aliacha ubaguzi ama la..
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu hayo yalifanyika baada ya Tanganyika kuwa imepata uhuru! Tumekaa na uhuru kwa muda lakini sasa ukoloni kwa nchi zetu za Afrika umerudi yena kwa njia nyingine. Tunaenda kuwaomba warudi kama wawekezaji sasa fukuza muwekezaji ukione cha moto! Wawekezaji (wakoloni wapya) wana jeuri kuliko wale wakoloni wa zamani. Viongozi wetu hawaruhusiwi kuingia kwenye migodi wanafukuzwa kama fisi. afadhali huyo alimwambia tu nenda zako.
   
 17. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wako wazungu wana roho chafu.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama wakifukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau weupe, sidhani kama itakuwa vibaya
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama Preta ulikuwepo enzi za marehemu Walwa akiwa RC huko kaskazini basi ni lazima sasa umekuwa kijeba!!Kumbuka hili ni gazeti la mwaka 1962. Tukifanya makisio kama unaweza kukumbuka skendo hii lazima ulikuwa umekwisha vunja ungo hivyo unaweza ukawa ulikuwa na miaka 18, sasa hivi kwa rehema za Mwenyzi mungu unadunda miaka 67!! Hongera sana kwani life expectancy ya Mtanzania imeshuka mpaka miaka 40 tu kwasababu ya viongozi mafisadi!!
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  RC Walwa alikuwa na jeuri ya kumfukuza mzungu kwakuwa kiongozi mkuu wa nchi alikuwa na msimamo usioyumba katika masuala ya maslahi ya wananchi wake.
  Jeshi la polisi lilikuwa na jeuri ya kutekeleza wajibu wao bila kusita kwakuwa lilikuwa linatambua wajibu wake na dhamana yake kwa wananchi. Jeshi la polisi lilikuwa halijachakachuliwa na kuwa vibaraka.

  Sasahivi mkuu wa nchi kila siku kiguu na njia kutembeza bakuli kwa hao wazungu, hawezi kuthubutu hata kuwakemea achilia mbali kuwafukuza.

  Wazungu wanalindwa na polisi wetu wenyewe na kuwatumia kuwanyanyasa wananchi na hata kufikia hatua ya kuua.

  Wazungu wanabaka dada zetu kwenye balozi, migodini, mahotelini na kwingineko lakini viongozi wa serikali, si raisi, mkuu wa jeshi la polisi, RC ama DC anayethubutu kuchukua hatua.

  Swali la kujiuliza hapa, kama enzi za mwalimu yeye na viongozi wenzake waliweza, hawa wa sasa wamepungukiwa na nini hadi wazungu wanatamba watakavyo?
   
Loading...