Mzumbe Secondary Alumni ni umoja unaowaunganisha watu wote waliosoma shule ya secondari Mzumbe tangu ilipoanzishwa.
Lengo la thread hii ni kupost matukio mbalimbali yanayohusu shughuli za alumni hii.
Kuchangia shughuli za alumni tumia akaunti hii,
Account name: MZUMBE SECONDARY SCHOOL ALUMNI
Account number: 10100705678
BANK: Akiba Commercial Bank
SWIFT Code: AKCOTZTZ
NOTE: You can also transfer money to the bank account using MPESA/Tigo Pesa/Airtel Money.
Karibuni tuonyeshe uzalendo kwa vitendo...
Hongereni sana wakuu,
nitupieni kapicha kamoja ka hapo bwenini kwangu( mkwawa no.1) kijiji
Hongereni sana, huu ni mfano wa kuigwa.
Kutoka kuwa walalamikaji na kuwa waleta masuluhisho ya matatizo yaliyopo, hii ndio njia ya kwenda.
Nimehamasika, nami nitacopy na kupaste hiki mlichofanya kwenye shule ya kijijini kwangu bila kuwa na nia ya kupata kitu in return kama wanafiki wengi wanaofanya haya kwa show tu za kutafutia ubunge au udiwani.
Hongereni sana
View attachment 254218
Mwanachama wa alumni, Oscar Roman Chamlima, akikagua kazi za ujenzi zinazoendelea Mzumbe sekondari.
I miss my School.
Awali ya yote naomba nijikumbushe mambo machache.
Nimepamiss Mirambo3, njia ya kuelekea kwenye chapati.
Ha haaaa.
Nimemiss debe la M.Z.U.D.A.X.
Mzukila na Mzumoro mimi zilikuwa hazinifurahishi kabisa.
Mi nilikuwa mdau wa Mzudax. Kama kuna mtu alikuwa mdau wa Mzudax naomba nimjue.
teh teh teh...yule dada mwenye ulemavu wa mguu? mnankumbusha mbali sana
Well Done Mzumbe. Proud Alumni.
Daima Mbele, Nyuma Mwiko.