Mzozo wa Congo, kwanini mchokozi asiwajibishwe?

Huo upumbavu wa Mchonga ulichangia kuitia nchi umasikini, leo hii wahanga wanaolaoamika umasiki wa nchi na hali duni za maisha moja ya sababu ni kushadadia mambo usiyo na faida nayo.

Tafiti zimeonyesha tuna vijana wa hovyo wasiokuwa na mchango wowote wa maana kwa taifa hili -- JPM.

Fnd9zI7WYAAJqG_.jpeg
 
Wa
hakuna wa kumwajibisha kagame, hata kama simkubali kwenye izo issue zake, lakini yeye anaenda kisomi zaidi. kwa kawaida, hakuna sababu yeyote ya msingi yenye ushahidi ya kumwadibisha kagame. yeye anasema, wale wanaopigana congo hata kama ni watutsi, sio wanyarwanda, ila ni wacongo wenye asili ya rwanda ambao wamekuwa neglected kwenye serikali ya congo hivyo ili congo kuwe na amani wakae kitako nao wajadiliane wao kwa wao, matatizo ya raia wa congo hata kama wana asili ya rwanda hayatakiwi kuifanya rwanda kuwa responsible. sasa hapo utakuja na sababu gani ya msingi.
Walipigwa hukimbilii kwa mbwana zao hao wanaowakana hadharani,na nyendo zao zinajulikana na kuwa documented

Hata wa kumfungia mipaka tu japo akajua yeye siyo almighty pia hakuna?
 
Katika mizozo yote, kila siku pana mchokozi na mhanga.

View attachment 2497295

Congo imekuwa ikiinyoshea kidole Rwanda siku zote kuwa ndiyo yenye lake jambo kwenye mzozo huu.

"Kulikoni kushindwa kumfunga Paka kengele? "

View attachment 2497475

Tanzania ya Nyerere haikuukubali katu upuuzi wa namna hii. Haikujali ulikuwa ukitokea Saharawi, Palestine, Iraq, Grenada, Mozambique au Vietnam. Tanzania haikuwahi kukaa kimya.

"Mchokozi asiyesikia hutiwa adabu kabla ya maisha kuendelea."

View attachment 2497307

Kulikoni mzozo wa Congo kuwa wa kudumu na kwa miongo zaidi ya miwili sasa, watu wasiokuwa na hatia wakiendelea kutaabika na hata kufa?

Kulikoni wanajeshi kwa maelfu kutoka nje walioko Congo kwa malengo ya kuuzima mgogoro huu kuendelea kuwapo bila ya mafanikio?

Kwanini mtuhumiwa huyu asisimamishwe uanachama EAC japo kwa kuanzia ili kujiridhisha na ikithibitika akafunzwa adabu vilivyo?
Iruhusiwe JWTZ kwenda kusafisha ili mradi wapewe misaada na vifaa zaidi na washirika wake wawe nyuma yake, uone watakavyosafisha na wakishindwa nakunya toka kariakoo mpaka mbagala
 
Rwanda inaongozwa na Paul Kagame. Huyu Paul Kagame ni Putin wa EAC, anaogopwa na kila kiongozi wa ukanda huu wa Afrika.

Nani atamgusa Kagame?

Huyu mama....kwa jeshi gani? Waliuaws na M23 enzi za JK kama kuku.

Ruto....kwa jeshi gani? Walipukutishwa na wasomali (Alshabab) miaka michache iliyopita

Museveni huyu ni swahiba wa Kagame. Lkn hata hivyo hafui dafu kwa Rwanda. Burundi na na vinchi vingine wala siviongelei
Hii sasa ngumu kumezaaa.
 
Mbna hawamgusi sasa?? Kelele za kwenye keyboard lol.

Vita sio kama ngumi za mtaani tuu, RDC wenyewe wameshindwa kuthibitisha hayo wasemayo….so hawawezi kukurupuka tuu kumgusa.. halafu vita ni solution ya mwisho sana katika nchi jirani.

Ila jua tuu tambo ni vitu vy kawaida kwa mtu kama Kagame ambaye in nature ni military pia, mbele ya Camera lazima ateme mikwara.
 
Anaogopwaaa, acha uongo wako hapaaa.
Tall anawapelekeshaaa kwata watu mweeeh.
 
Rwanda inaongozwa na Paul Kagame. Huyu Paul Kagame ni Putin wa EAC, anaogopwa na kila kiongozi wa ukanda huu wa Afrika.

Nani atamgusa Kagame?

Huyu mama....kwa jeshi gani? Waliuaws na M23 enzi za JK kama kuku.

Ruto....kwa jeshi gani? Walipukutishwa na wasomali (Alshabab) miaka michache iliyopita

Museveni huyu ni swahiba wa Kagame. Lkn hata hivyo hafui dafu kwa Rwanda. Burundi na na vinchi vingine wala siviongelei
Hapa unatudanganya sana, kagame hawezi kuwa kama putin hapa EAC, kagame ni muasi kama waasi wengine waliojichukulia madaraka kibabe kwasababu walikuwa na dhamana katika jeshi la rwanda pia ukiangalia mfumo wa rwanda ni tofauti na kwetu Tanzania, wakati rwanda inajitafuta kujitawala Tanzania alishashiriki vita nyingi sana la ukombozi wa bara la afrika, wanyarwnda wengi wanakubali jitihada za JWTZ katika kutuliza vita nchini kwao na kagame kujitoa msituni kupewa nchi ktk makubaliano yaliofanyika arusha. Kagame analeta vijana wake hapa nyumbani kufunzwa ktk nyanja mbalimbali pia ukumbuke Tanzania ndio nchi pekee yenye intelijensia mama ukanda wa afrika mashariki. Tanzania inawqtu ambao imewahifadhi tayari ya violence ili amani ya nchi iendelee kuwepo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa ktk jumuiya ya madola kwenye ushiriki wa ulinzi wa dunia pia ukiongelea silaha kila taifa linanunua silaha pia kutokana na sababu za kiusalama nchi kama nchi haiwezi kuexpose kila aina ya silaha inayomiliki. Rwanda haiwezi na kamwe haina ubavu wa kujaribu kutumishiana misuli na mtanzania au hata mkenya au mganda mbaya zaidi huko burundi kuna vita ya ujasusi baina ya rwanda na burundi na warwanda wengi wanapoteza maisha yao ndani ya ardhi ya ndayishimiye. Paul kagame hawezi kumzonga evariste kama ilivyokuwa kwa nkurunzinza anamjua ni mtu wa aina gani. Hivyo kabla hujamfananisha muasi na jasusi uwe na evidence nzito za kutetea hoja yako
 
Huku ni kulea pimbi na atakuja kuota mkia

Nani wa kumuwajibisha Rwanda mkuu, ukitoa Kenya kidogo, huku kwenye nchi nyingine hasa za Afrika mashariki, viongozi wako madarakani kwa wizi wa kura, na hilo Kagame analijua. Hivyo hawezi kumhofia kiongozi yoyote aliyeko madarakani kwa wizi wa kura.
 
hakuna wa kumwajibisha kagame, hata kama simkubali kwenye izo issue zake, lakini yeye anaenda kisomi zaidi. kwa kawaida, hakuna sababu yeyote ya msingi yenye ushahidi ya kumwadibisha kagame. yeye anasema, wale wanaopigana congo hata kama ni watutsi, sio wanyarwanda, ila ni wacongo wenye asili ya rwanda ambao wamekuwa neglected kwenye serikali ya congo hivyo ili congo kuwe na amani wakae kitako nao wajadiliane wao kwa wao, matatizo ya raia wa congo hata kama wana asili ya rwanda hayatakiwi kuifanya rwanda kuwa responsible. sasa hapo utakuja na sababu gani ya msingi.
Rwanda inawaneglegate hao M23 kwasababu mwanzo walikuwa waasi na kagame na kagame hawezi kuwarudisha nyumbani ilihali bado anataka mali zaidi kwa wacongo. Hizi nchi zilishakuwa na uhasama tangu na tangu huko nyuma, rwanda haipo powerful kama wengi wanavyodhani rwanda inajitahidi kujihami kwasababu nchi zinazomzunguka ni kubwa sana kuanzia kiardhi,manpower,resources majeshi hata silaha. Leo hujawai kusikia rwanda kapewa nishani ya ulinzi wa amani ya dunia lakini kila kukicha wanabuni njia mpya kujilinda. Rwanda inamajasusi wanaofanyia kazi sserikali ya kagame na sio usalama wa taifa lao kama ilivyo kwa mataifa mengine. Ukweli upo wazi ila ni swala la muda trust the process kuna vita inapikwa na wacongo na hao hao m23 watarudi kuipiga rwanda kwasababu kagame alishawahi kuwageuka na kutaka kuwakamatisha watu kama sultani makenga,role nkunda na wengine wengi ambao walikimbilia congo kuwa m23 na wakijificha sana kukwepa mkono wa ICC au kifo kutoka kwa RDF
 
Nani wa kumuwajibisha Rwanda mkuu, ukitoa Kenya kidogo, huku kwenye nchi nyingine hasa za Afrika mashariki, viongozi wako madarakani kwa wizi wa kura, na hilo Kagame analijua. Hivyo hawezi kumhofia kiongozi yoyote aliyeko madarakani kwa wizi wa kura.

Mkuu Kwa hakika umegusa penyewe. Ya huyu bwana hayavumiliki ila tu na wahalifu wenziwe.
 
Kunukuu maneno ya mtu aliyekuwa na mtindio wa ubongo na kuwa anawehukawehuka mara kwa mara kwa sababu ya damu za watu alizomwaga ni aina mojawapo ya ukichaa.

Hakuna mtu asiyekuwa na jema hata moja. Kudhani kuwa mtu anaweza kukosa jema kabisa ndiyo ukichaa wenyewe sasa.
 
Iruhusiwe JWTZ kwenda kusafisha ili mradi wapewe misaada na vifaa zaidi na washirika wake wawe nyuma yake, uone watakavyosafisha na wakishindwa nakunya toka kariakoo mpaka mbagala
Askari wa Kibongo huwa wanaaibisha sana, very poorly trained na hilo hujidhihirisha wanapokuwa kwenye operations za nje.
Mozambique kwa wale Al-Shabaab mpaka lilipoingia jeshi la Rwanda ndiyo likawamudu wakati jeshi letu lilishindwa na wanajeshi wetu kule DRC ni aibu hata kusema bora sasa wanajeshi wa Kikenya wanaonyesha professionalism na kwamba wako well trained.
Tulikuwa na jeshi imara enzi za mchonga kwa kuwa alizingatia sana nchi kuwa na jeshi lenye nguvu, inauma lakini ndiyo ukweli wenyewe.
 
Anaogopwaaa, acha uongo wako hapaaa.
Tall anawapelekeshaaa kwata watu mweeeh.

You're very right, wanamuogopa lakini hawawezi kuyanena hayo hadharani. Hako kanchi kadogo lakini matata.
Miaka kadhaa nyuma nikiwa Dubai tulikuwa tunapiga story na Waarabu wanasema 'hako ka Israel kadogo sijui kwanini tusikavamie tukakadhibiti kakaacha kuwaburuza Palestinians', it's the same shit I'm seeing our EA zone.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom