Mzozo wa Congo, kwanini mchokozi asiwajibishwe?

Rwanda inaongozwa na Paul Kagame. Huyu Paul Kagame ni Putin wa EAC, anaogopwa na kila kiongozi wa ukanda huu wa Afrika.

Nani atamgusa Kagame?

Huyu mama....kwa jeshi gani? Waliuaws na M23 enzi za JK kama kuku.

Ruto....kwa jeshi gani? Walipukutishwa na wasomali (Alshabab) miaka michache iliyopita

Museveni huyu ni swahiba wa Kagame. Lkn hata hivyo hafui dafu kwa Rwanda. Burundi na na vinchi vingine wala siviongelei
Kwa jeshi gani alilonalo huyo Kagame na wahuni hao wa M23? acha ushabiki wa kijinga
 
Rwanda inaongozwa na Paul Kagame. Huyu Paul Kagame ni Putin wa EAC, anaogopwa na kila kiongozi wa ukanda huu wa Afrika.

Nani atamgusa Kagame?

Huyu mama....kwa jeshi gani? Waliuaws na M23 enzi za JK kama kuku.

Ruto....kwa jeshi gani? Walipukutishwa na wasomali (Alshabab) miaka michache iliyopita

Museveni huyu ni swahiba wa Kagame. Lkn hata hivyo hafui dafu kwa Rwanda. Burundi na na vinchi vingine wala siviongelei
Kushabikia jeshi la nchi nyingine ni kosa.
 
Kumbuka Tigrayans na Abiy Ahmed haikuwa hadi alipo kasimu u waziri mkuu akatupia kombati na kuingia uwanjani. Vinginevyo Tigrayans walikuwa kwenye viunga vya Addis Ababa.
Sasa si ndio uongozi huo na Zelensky si unamuona frontline anafanya hamasa. Kinachotakiwa ni courage na kuwa serious na matamko ya kisiasa yaendane na vitendo. Congo vita wanapigia mdomoni zaidi
 
hakuna wa kumwajibisha kagame, hata kama simkubali kwenye izo issue zake, lakini yeye anaenda kisomi zaidi. kwa kawaida, hakuna sababu yeyote ya msingi yenye ushahidi ya kumwadibisha kagame. yeye anasema, wale wanaopigana congo hata kama ni watutsi, sio wanyarwanda, ila ni wacongo wenye asili ya rwanda ambao wamekuwa neglected kwenye serikali ya congo hivyo ili congo kuwe na amani wakae kitako nao wajadiliane wao kwa wao, matatizo ya raia wa congo hata kama wana asili ya rwanda hayatakiwi kuifanya rwanda kuwa responsible. sasa hapo utakuja na sababu gani ya msingi.
 
Kawaida sera zetu nje huwa hatufungamani na upande wowote, ukiitazama vizuri hii sera ni sawa na sera ya kulea tatizo, naamini kuna wakati huwa tunaona kabisa chanzo cha tatizo kilipo, lakini tunaamua tu kuwa wapole bila sababu, huu wakati mwingine ni sawa na ujinga tu.

Kagame anaonekana mchokozi, sasa ni kama anaogopwa, aliwafukuza wale mabalozi wa Ufaransa, Ubelgiji, lakini mpaka leo kimya, wazungu hawajafanya chochote, inawezekana wako kwenye majadiliano ya chini chini Rwanda ifungue ofisi zao za ubalozi, huu nao ni sawa na uoga mwingine kwa Kagame.
 
Huyu mbona hata kwa Congo hawezi kufurukuta? Ni land locked country. Huyu mbona hata bila kufyatua kitu (kama yule mwamba wa Commorro) anatepeta asubuhi tu?
Sasa kwann anasumbua hivi halafu anatazamwa tu? Na kuna kipindi alimtisha Kikwete kwa kumwambia "I will hit you"
 
Sasa si ndio uongozi huo na Zelensky si unamuona frontline anafanya hamasa. Kinachotakiwa ni courage na kuwa serious na matamko ya kisiasa yaendane na vitendo. Congo vita wanapigia mdomoni zaidi
Hata Nyerere alifika Mtukula ndani ya kombati za kijeshi.
 
Sasa kwann anasumbua hivi halafu anatazamwa tu? Na kuna kipindi alimtisha Kikwete kwa kumwambia "I will hit you"
Kutisha, mkwara mbuzi au kujimwambafy nani asiyeweza? Kwani Saddam ilikuwaje? Kim naye je? Kwani tangu lini maneno matupu yakavunja mfupa?
 
Kawaida sera zetu nje huwa hatufungamani na upande wowote, ukiitazama vizuri hii sera ni sawa na sera ya kulea tatizo, naamini kuna wakati huwa tunaona kabisa chanzo cha tatizo kilipo, lakini tunaamua tu kuwa wapole bila sababu, huu wakati mwingine ni sawa na ujinga tu.

Kagame anaonekana mchokozi, sasa ni kama anaogopwa, aliwafukuza wale mabalozi wa Ufaransa, Ubelgiji, lakini mpaka leo kimya, wazungu hawajafanya chochote, inawezekana wako kwenye majadiliano ya chini chini Rwanda ifungue ofisi zao za ubalozi, huu nao ni sawa na uoga mwingine kwa Kagame.

Bila kumung'unya maneno huu ni unafiki. Nyerere hakuwa na unafiki huu.

Ninakazia:

https://www.jamiiforums.com/threads/lililokuwa-taifa-la-kupigiwa-mfano-halipo-tena.2031851/

Serikali ya watu haiwezi kuwa ya kinafiki.
 
Katika mizozo yote, kila siku pana mchokozi na mhanga.

View attachment 2497295

Congo imekuwa ikiinyoshea kidole Rwanda siku zote kuwa ndiyo yenye lake jambo kwenye mzozo huu.

"Kulikoni kushindwa kumfunga Paka kengele? "

View attachment 2497475

Tanzania ya Nyerere haikuukubali katu upuuzi wa namna hii. Haikujali ulikuwa ukitokea Saharawi, Palestine, Iraq, Grenada, Mozambique au Vietnam. Tanzania haikuwahi kukaa kimya.

"Mchokozi asiyesikia hutiwa adabu kabla ya maisha kuendelea."

View attachment 2497307

Kulikoni mzozo wa Congo kuwa wa kudumu na kwa miongo zaidi ya miwili sasa, watu wasiokuwa na hatia wakiendelea kutaabika na hata kufa?

Kulikoni wanajeshi kwa maelfu kutoka nje walioko Congo kwa malengo ya kuuzima mgogoro huu kuendelea kuwapo bila ya mafanikio?

Kwanini mtuhumiwa huyu asisimamishwe uanachama EAC japo kwa kuanzia ili kujiridhisha na ikithibitika akafunzwa adabu vilivyo?
Huo upumbavu wa Mchonga ulichangia kuitia nchi umasikini, leo hii wahanga wanaolaoamika umasiki wa nchi na hali duni za maisha moja ya sababu ni kushadadia mambo usiyo na faida nayo.
 
Congo ni nchi yenye jeshi matako kabisa linakera na halistahili kuwa na hata one star General mmoja. Ukiwaona wanavyopigana wanadai mapigano makali ila ukifuatilia ni kwamba M-23 wakifanya movement hao FARDC wanaondoka eneo hilo bila heavy resistance.
Kazi ya M-23 ni kutangaza tunaenda kuvamia eneo hili, wakishajitokeza na kufyatua risasi mbili tatu FARDC kazi yao ni kuretreat. Jeshi gani linapigana kwa retreat kuliko advancement.

Na serikali ya DRC ni walaini. Muda ambao Felix kawa Rais unamtosha kabisa kuwa ameshika madaraka ipasavyo na akiamua jambo political will inaenda kwa moyo mmoja. Sababu za deko wanazotoa Congo kushindwa ni upuuzi tu.

Abiy Ahmed pale Ethiopia alikaa miaka michache tu akawasoma kwanza kisha ghafla akaondoka mamluki, Tigrayans walivyojifanya wanaleta armed resistance aliwanyoosha mara moja. Hapo kaingia hamna silaha za kutosha ila kafanya procurement ya haraka sana. Uturuki, UAE, China wamempa drones tofauti, kanunua artillery na silaha ndogondogo hata za Iran. Ile vita aliyopigana ni heavy na Tigrayans wanajua vita ya kisasa sio hawa M-23. Wamekufa watu maelfu na mamilioni wamehamishwa makazi ila uamue moja nchi isambaratike kwa kuendekeza upuuzi au ulazimishe serikali iheshimiwe na nchi ibaki na utengamano.

Congo haihitaji silaha za hata $1 billion kuanzisha operation ya maana. Ground attack jets zenyewe wanazo tatu tu Su-25, drones hawana, artillery za maana hawana. Sijui priority yao hao lala lala ni nini.

Kwani Mali Republic ina hela gani kushinda DRC, mbona inafanya procurement ya maana na training ya nguvu na waasi inawatandika ipasavyo. Congo sio nchi ya kushindwa na mamluki wa Uganda na Rwanda kwa pamoja, ni uwendawazimu wao tu jeshi la kukata mauno bora hata mgambo wetu.

Vita inayoshindikana kwa kupambana inajulikana, na inayoshindikana kwa uzembe inajulikana.
Papaa, nikufege juu ya nini. Mie ni myuzisiee tangu mpaka vile.
Hii mambo ya magonvi ni mambo ya bantu ba burebure, vremaa papaa.
 
klm.co.tz

Tanzania na Kenya - Machafuko ya kiraia

Kutokana na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini Tanzania na Kenya kuanzia Ijumaa tarehe 27 Januari hadi na kujumuisha Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, baadhi ya safari zetu za ndege kwenda, kutoka au kupitia Dar- es- Salaam (DAR), Kilimanjaro (JRO), Zanzibar (ZNZ), na Huenda Nairobi (NBO) ikatatizwa. Tunafanya tuwezavyo ili kukusaidia ukiwa njiani tena.

Kuweka nafasi tena na kuomba kurejeshewa pesa

Ikiwa umehifadhi nafasi ya safari ya ndege kwenda, kutoka au kupitia maeneo yaliyoorodheshwa hapa chini Ijumaa tarehe 27 Januari hadi na ikijumuisha Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, unaweza kuona hapa chini ni chaguo gani za kuhifadhi na kurejesha pesa tunazoweza kukupa. Chaguo hizi ni halali tu ikiwa una tikiti iliyotolewa hapo awali mnamo au kabla ya Ijumaa 27 Januari 2023.

Dar- es- Salaam, Tanzania (DAR)

Kilimanjaro, Tanzania (JRO)

• Zanzibar, Tanzania (ZNZ)

• Nairobi, Kenya (NBO)

Je, ndege yako halisi itaondoka Ijumaa tarehe 27

Januari hadi na ikijumuisha Jumatatu 30 Januari

2023 hadi, kutoka au kupitia yoyote ya waliotajwa hapo juu

marudio. Kisha tarehe yako mpya ya kuondoka inapaswa

iwe kabla au Jumatatu tarehe 6 Februari 2023. Unaweza

weka nafasi upya ya safari yako ya ndege hivi punde siku ya Jumatano 1

Februari 2023. Tafadhali tazama hapa chini chaguo na..
 
Huo upumbavu wa Mchonga ulichangia kuitia nchi umasikini, leo hii wahanga wanaolaoamika umasiki wa nchi na hali duni za maisha moja ya sababu ni kushadadia mambo usiyo na faida nayo.
Umaskini umetukumba lini tena sisi?

EI18xZUWoAAEgTP.jpeg
 
Kumaliza mgogoro wa DRC huhitaji hata kupigana vita, ujinga na ukabila wa mwafrica ndio chanzo kikubwa cha hii vita, jiulize hao M23 wanataka nini then ukishajua utagundua Congo hakuna tatizo kabisa zaidi ya upumbavu mtupu
 
klm.co.tz

Tanzania na Kenya - Machafuko ya kiraia

Kutokana na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini Tanzania na Kenya kuanzia Ijumaa tarehe 27 Januari hadi na kujumuisha Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, baadhi ya safari zetu za ndege kwenda, kutoka au kupitia Dar- es- Salaam (DAR), Kilimanjaro (JRO), Zanzibar (ZNZ), na Huenda Nairobi (NBO) ikatatizwa. Tunafanya tuwezavyo ili kukusaidia ukiwa njiani tena.

Kuweka nafasi tena na kuomba kurejeshewa pesa

Ikiwa umehifadhi nafasi ya safari ya ndege kwenda, kutoka au kupitia maeneo yaliyoorodheshwa hapa chini Ijumaa tarehe 27 Januari hadi na ikijumuisha Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, unaweza kuona hapa chini ni chaguo gani za kuhifadhi na kurejesha pesa tunazoweza kukupa. Chaguo hizi ni halali tu ikiwa una tikiti iliyotolewa hapo awali mnamo au kabla ya Ijumaa 27 Januari 2023.

Dar- es- Salaam, Tanzania (DAR)

Kilimanjaro, Tanzania (JRO)

• Zanzibar, Tanzania (ZNZ)

• Nairobi, Kenya (NBO)

Je, ndege yako halisi itaondoka Ijumaa tarehe 27

Januari hadi na ikijumuisha Jumatatu 30 Januari

2023 hadi, kutoka au kupitia yoyote ya waliotajwa hapo juu

marudio. Kisha tarehe yako mpya ya kuondoka inapaswa

iwe kabla au Jumatatu tarehe 6 Februari 2023. Unaweza

weka nafasi upya ya safari yako ya ndege hivi punde siku ya Jumatano 1

Februari 2023. Tafadhali tazama hapa chini chaguo na..

Kama namwona beberu na security alert yake
 
Wa
hakuna wa kumwajibisha kagame, hata kama simkubali kwenye izo issue zake, lakini yeye anaenda kisomi zaidi. kwa kawaida, hakuna sababu yeyote ya msingi yenye ushahidi ya kumwadibisha kagame. yeye anasema, wale wanaopigana congo hata kama ni watutsi, sio wanyarwanda, ila ni wacongo wenye asili ya rwanda ambao wamekuwa neglected kwenye serikali ya congo hivyo ili congo kuwe na amani wakae kitako nao wajadiliane wao kwa wao, matatizo ya raia wa congo hata kama wana asili ya rwanda hayatakiwi kuifanya rwanda kuwa responsible. sasa hapo utakuja na sababu gani ya msingi.
Walipigwa hukimbilii kwa mbwana zao hao wanaowakana hadharani,na nyendo zao zinajulikana na kuwa documented
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom