Puncler
JF-Expert Member
- Jul 17, 2017
- 1,388
- 1,884
Huu ujinga unaaminiwa tu na wajinga wasiokuwa na exposure.Hapa unatudanganya sana, kagame hawezi kuwa kama putin hapa EAC, kagame ni muasi kama waasi wengine waliojichukulia madaraka kibabe kwasababu walikuwa na dhamana katika jeshi la rwanda pia ukiangalia mfumo wa rwanda ni tofauti na kwetu Tanzania, wakati rwanda inajitafuta kujitawala Tanzania alishashiriki vita nyingi sana la ukombozi wa bara la afrika, wanyarwnda wengi wanakubali jitihada za JWTZ katika kutuliza vita nchini kwao na kagame kujitoa msituni kupewa nchi ktk makubaliano yaliofanyika arusha. Kagame analeta vijana wake hapa nyumbani kufunzwa ktk nyanja mbalimbali pia ukumbuke Tanzania ndio nchi pekee yenye intelijensia mama ukanda wa afrika mashariki. Tanzania inawqtu ambao imewahifadhi tayari ya violence ili amani ya nchi iendelee kuwepo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa ktk jumuiya ya madola kwenye ushiriki wa ulinzi wa dunia pia ukiongelea silaha kila taifa linanunua silaha pia kutokana na sababu za kiusalama nchi kama nchi haiwezi kuexpose kila aina ya silaha inayomiliki. Rwanda haiwezi na kamwe haina ubavu wa kujaribu kutumishiana misuli na mtanzania au hata mkenya au mganda mbaya zaidi huko burundi kuna vita ya ujasusi baina ya rwanda na burundi na warwanda wengi wanapoteza maisha yao ndani ya ardhi ya ndayishimiye. Paul kagame hawezi kumzonga evariste kama ilivyokuwa kwa nkurunzinza anamjua ni mtu wa aina gani. Hivyo kabla hujamfananisha muasi na jasusi uwe na evidence nzito za kutetea hoja yako
Weka facts and figures za nchi zote za EA community kuhusu intelijensia ili tulinganishe manake iseje ikawa hauna facts bali umekuwa brainwashed au una uzalendo uchwara wa kuogopa kukataa ukweli.
Ukienda kidunia(tumi Google au Wikipedia au reliable sources zozote) nchi zinalinganishwa kwa facts hata kwenye mambo ya intelijensia.