Ahsanteni sana wanaJF kwa mchango mzuri sana tena sana. Sasa mjadala wa mada unapata mwelekeo mpevu.
Naomba tunapoendelea kutafakari na kuchangia ebu tupekue ujumbe wa ndani uliomo katika nukuu hizi
- Rushwa ni wimbo wa sumu uliotapakaa katika ubongo wa KILA mwanataifa hili, tuondolee wimbo huu tafadhali- Mwimbaji Mpoto
- TAMAA ikichukua mimba huzaa DHAMBI,DHAMBI ikiisha kukomaa huzaa mAUTI - Biblia
- VIONGOZI ni zao la JAMII- hii sikumbuki alisema nani
- Mdharau mwiba mguu huota tende- wahenga
Ni kweli ndugu zangu,kwamba ufisadi tulio nao leo chimbuko lake lina historia ndefu katika matukio ya kisiasa na matendo ya jamii kwa ujumla,jambo hili unaweza vile vile kulitazama hivi:
mtu mmoja akikosa maadili ni tatizo kwa familia
familia moja ikikosa maadili ni tatizo kwa kijiji
kijiji kimoja kikikosa maadili ni tatizo kwa kata
kata moja ikikosa maadili ni tatizo kwa tarafa
vivyo hivyo
tarafa kengeufu huathiri wilaya
wilaya nayo huaribu
mkoa
kutoka mkoani au
majimboni taifa linadhurika
Nikweli pia kwamba joka linalotutesa sasa tumelilea wenyewe
Matharani,
Enzi zile(na hata sasa) watoto wetu na ndugu zetu walipopata ajira katika mashirika ya umma,tukawashinikiza watajirike na ambao hawakufanya hivyo tukawacheka, tulisababisha tamaa miongoni mwa watumishi wa umma wote. Hatimaye tamaa ikachukua mimba na ikazaa DHAMBI(mitiri ya joka)
Hili ni mojawapo ya maeneo tulipojikwaa na tulipoangukia tugagonga pua. Kilichotoka humo watoto wetu na ndugu zetu wakayaibia mashirika yakawa mufilisi, tukayauza.Tena kwa sababu tamaa ilikwisha kuzaa dhambi, yakauzwa hata ambayo yalikuwa yana nafuu.Mkosi nao ukaambatana na hilo,mengi tukawauzia ambao si wenzetu!!!
Aidha enzi zile,tulipofuata huduma maofisini, mfano mahakamani,hospitalini na kwingineko,watumishi wa umma chini ya shinikizo la jamii linalowatarajia watajirike,wakatuomba chai,wakachukua 10%,wakaleta misemo ya kuzunguka mbuyu, kula mlungula,shati la mikono mirefu na mingine nikumbusheni...
Laiti tungelijua ndio hivyo tulikuwa taratiiibutunamfuga nyoka mwenye sumu ya kufisha mithiri ya weapons of mass destruction.
Kwa upande mingine, hata mitazamo na matukio katika uwanja wa siasa yalichangia. Kila mtu alipopewa wadhifa(hata leo) utasikia akipongezwa kwa misemo ya kifisadi fisadi,mfano ..
hongera sana ndugu UMEULA!! Ilikuwaje hatukutafakari tunamwambia ameula unini???
Twende mbele kidogo,(namkoma nyani hapa),
Yule mzee wa mkoa wa Rukwa aliyegombea ubunge dhidi ya Mzindakaya,akapigwa chini kura za maoni akakimbilia NCCR,akapachikwa unaibu katibu mkuu,akakuta NCCR hakuna mijihela aliyoizoea alikokuwa CCM,na juzi alivyoona mtu wa kwao kawa waziri mkuu,eti katangaza kurudi CCM (siasa za bongo bwana!).
Alipokuwa NCCR alilopoka hivi,
Sisi(yaani yeye na watu fulani ndani ya CCM)
ndio tulishauri CCM iwakaribishe matajiri chamani,wakati vyama vingi vinakaribia kurejeshwa nchini.Tukasema,tukiendelea kushikilia eti CCM ni ya wakulima na wafanyakazi vyama vingine vitawachukua matajiri na kutuzidi nguvu
HUO ndio ulikuwa mwanzo wa mafisadi wengi kujikusanya ndani ya ngome moja,yaani CCM,lakini si kwamba hapo ndipo walipochimbuka,walichimbuka katika jamii kengeufu!!!
Kilichofuatia basi,ikawa ni kutimiza lile neno lililonenwa na nabii Yesu aliposema
KWA MAANA PALIPO NA MZOGA,NDIPO WAKUSANYIKAPO TAIHakika likatimia,matajiri wa hela chafu na wa hela safi(Matharani wale walioitikia wito wa mzee
Sumaye kwamba anayetaka mambo yake ya kibiashara yamnyokee ajiunge CCM)wakaikimbilia ngome ya sisiemuuu,wenye tamaa nao wakaona,kumbe mambo ya fwedha ni CCM!! hao wakogombea udiwani,ujumbe wa shingo(NEC), ubunge,na hata urais. Au hamjui ni kwa nini CCM ina wanachama kibao, vijana wasomi wanakimbilia huko na maprofesa wanazitelekeza lecture rooms.Open your eyes and see this single reason amongst some others.
Kilichoambatana na hayo CCM ikajirundikia mafwedha kibao,eti ruzuku.Ikaendelea kuenjoy pia vitega uchumi ilivyovikusanya enzi za mfumo wa chama kimoja..Loo! tai wakazidi kumiminika katika bonde lenye mzoga.Ama kwa hakika katika vita yetu, lazima kuisambaratisha hii ngome.
Lakini tunarudi kule kule,tamaa ya tai wote hawa wamefugwa na kulelewa na jamii.Tena na tai wengine tunao, bado wako katika taasisi za umma,wengine kwenye vyama vya upinzani,kwenye NGOs ndo usiseme,hata private sector,ilimradi tu ni
ka-nchi kananuka rushwa(Alisema Mwalimu,R.I.P)
Ngugu zangu,ni kwa dawa ipi tuiponye JAMII,tena tuiponye haraka kabla hatujaangamia sote.Je,tuanzie katika elimu ya malezi mashuleni na katika kaya,au tufanyeje????