Mzizi Mkuu Wa Ufisadi

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Ndugu zangu watanzania,

Nchi yetu inakabiliwa na matatizo mengi kwa sasa kiasi kwamba inayumba sana na tusipoangalia itaanguka milele na haitapata kusimama tena.

Kama kuna mtu wa kuiokoa nchi yetu dhidi ya hatari hiyo,basi si mwingine bali sisi watanzania wenyewe. Huu ni wajibu mzito unaotukabili,ingekuwa heri basi tusiufanyie mzaha.

Miongoni mwa matatizo makubwa sana yanayotukabili ni hili la UFISADI.Yamkini tumekwisha anza kujaribu kupambana nalo lakini huenda silaha na mbinu tunazotumia kulikabili si muafaka kabisa.

Wataalam wa masuala ya kushughulikia matatizo,hususan matatizo ya kijamii wanapendekeza kwamba ili kuhakikisha kwamba tatizo linashughulikiwa ipasavyo hapana budi kutumia kile wanachokiita PROBLEM TREE ANALYSIS,yaani kulitambua na kulichambua tatizo kwa kuangalia matunda yake,majani yake,matawi yake,shina lake,mizizi yake mbali mbali na hasa mzizi wake mkuu-mzizi wa kati (TAPE ROOT),tena kwa kufika katika ncha ya mwisho kabisa ya huo mzizi mkuu. Naam,ukiisha kubainika huo mzizi mkuu,hakika siku utakapong'olewa,mti mzima utanyauka,si shina wala matawi wala majani yatakayobakia kijani kibichi.

Watanzania wenzangu,tumeujadili sana ufisadi(whatever this word means),yaani ubadhilifu,rushwa,ubinafsi na kujilimbikizia mali visivyo halali.Lakini je,tumekwisha kujiuliza na kutafuta u wapi mzizi mkuu wa dubwana hili,ili tuuchimbue tuondokane nalo?

Yamkini twaweza fikiri kwamba mzizi mkuu hapa ni CCM,well hoja hapo ikijengwa vizuri yawezekana ni kweli na hivyo dawa ya ufisadi ikawa ni kuing'oa CCM madarakani.Swali linalozuka tena hapo ni je, siku CCM iking'oka itakuwa kweli ndio mwisho wa ufisadi? Na kama jibu ni hapana...lets continue digging for the tape root.

Ndugu wananchi, kabla sijaja na nadharia yangu ya ninakodhani huko ndiko mzizi huo mkuu uliko, naomba mjadala...karibuni
 
Yamkini twaweza fikiri kwamba mzizi mkuu hapa ni CCM,well hoja hapo ikijengwa vizuri yawezekana ni kweli na hivyo dawa ya ufisadi ikawa ni kuing'oa CCM madarakani.

CCM yote sio mafisadi, isipokuwa kuna baadhi ya viongozi ambao ni mafisadi, sasa tunahitaji sheria kushika mkondo wake ili waondolewe, meaning kwamba ushahidi uwekwe wazi na tubadili baadhi ya sheria zetu za jamhuri, ambazo zinamkinga rais mstaafu kufikishwa kwenye sheria.

Huwezi kuingo'a CCM madarakani bila ya kuwa na alternative, na sababu nzito ya kuwapa wananchi wasiichague CCM, maana sababu zilizopo tayari zimeonekana kuwa hafifu na not enough kwa wananchi ku-respond on that line so far, dawa ni kubadili katiba ya jamhuri ni too weak na originally iliundwa kwa ajili ya utawala wa chama kimoja, sasa ni vigumu kapata haki ikiwa bado inatumika kwenye vyama vingi vya siasa.

Ahsante Mkuu.
 
Mkuu Field Marshal,
Na mafisadi sio viongozi peke yao ndugu yangu.Sheria tunazo,tena nyingine kali kama ncha ya upanga.Katiba yetu japo ni kweli inahitaji kuandikwa upya bado na yenyewe sio MZIZI MKUU wa UFISADI.Please search more until you find this tape root,this is my challenge to you JF members...
 
Kwa mtizamo wangu,Naona Mzizi mkuu wa ufisadi umejikita kwenye UKOSEFU WA MAADILI KATIKA UONGOZI.
Maadili yanapokosekana ktk uongozi kinachotokea ni kupora au kuvuruga maamuzi sahihi,kupuuza hoja za wananchi au kupindisha kwa maslahi ya kiongozi fulani.Tume nyingi zimeundwa tangu utawala wa BWM hadi leo tena na zikiwa na hoja lakini utekelezaji umekuwa wa kulindana sana kuliko utendaji halisi.

1.Viongozi tulio nao wamesahau/hawafuati kanuni za maadili ya uongozi aidha kwa kujua au kutojua.
2.Wanatafuta kujilimbikizia mali zaidi kuliko kutumikia wananchi.Wengi wakipata uongozi hapo ndo wakati muafaka ya kuendeleza biashara zao
3.Wengi wanatafuta kutumikiwa kuliko kutumika.Wanatafuta maslahi binafsi sana bila hata ya kujali hatima ya nchi na wananchi.
4.............
5............

Tunaweza kubadili hata Rais mwaka 2010 lakini bila kuhubiri haya maadili na kanuni za uongozi bora na kuwashikia mabango wanaokiuka,tutaishia kuwa na mabadiliko kama ya Kenya ambayo matunda yake yote yameishia shimo la giza.Walimbadili MOI wakaweka matumaini yao kwa Kibaki lakini walichopata kwa KIBAKI ni MAAFA YA WAKENYA ZAIDI YA 1500 NA MPAKA LEO HAWANA BARAZA KAMILI LA MAWAZIRI.

MAADILI HAYA YA UONGOZI MSIMAMIZI MKUU NI RAIS,NA AWE NA NIA YA DHATI KATIKA KUWAJIBIKA NA KUWAJIBISHA WALIO CHINI YAKE.

MAADUI WA MAADILI HAYA YA UONGOZI NI.
1.urafiki kuingizwa katika mambo yanayogusa maslahi ya Taifa yaani kulipana fadhila.Kwa kuwa nilikusaidia kupiga kampeni hata kama sina sifa ya kuongoza,naingizwa sehemu fulani ili nami nile fadhila.Huu ni mfumo wa kubebana.

2.Kulundikana ndugu wa damu au ukoo katika masuala ya uongozi/taasisi fulani(simaanishi kuwa ndugu hawawezi kuongoza kwa pamoja) ila huwa inatia woga kuchukua maaumuzi mazito dhidi yake.

3.WOGA(WENGI WANAHOFIA USALAMA WAO KAMA WATACHUKUA MAAMUZI MAZITO).Kuthubutu kutoa tamko zito mpaka uwe umehakikishiwa kuishi au una secure base.
4................
5..............

Huo ndo mtizamo wangu
 
CCM yote sio mafisadi, isipokuwa kuna baadhi ya viongozi ambao ni mafisadi, sasa tunahitaji sheria kushika mkondo wake ili waondolewe, meaning kwamba ushahidi uwekwe wazi na tubadili baadhi ya sheria zetu za jamhuri, ambazo zinamkinga rais mstaafu kufikishwa kwenye sheria.

Huwezi kuingo'a CCM madarakani bila ya kuwa na alternative, na sababu nzito ya kuwapa wananchi wasiichague CCM, maana sababu zilizopo tayari zimeonekana kuwa hafifu na not enough kwa wananchi ku-respond on that line so far, dawa ni kubadili katiba ya jamhuri ni too weak na originally iliundwa kwa ajili ya utawala wa chama kimoja, sasa ni vigumu kapata haki ikiwa bado inatumika kwenye vyama vingi vya siasa.

Ahsante Mkuu.

Thanks Mkuu.
Nani wa kuing'oa CCM? kwanza watakaoing'oa CCM ni wana CCM. so sis kama wananchi tunatakiwa kuanzisha chaos then CCM ikapanguka and that is only way.

CCM inatupeleka ziwani, its a matter of time tutakuwa drown wote tulio ndani ya MV Tanzania. What i like ni kwamba hata insiders wa CCM wako confidence kwamba CCM ndio mama na baba wa Tanzania, you either like it or you dont.

They will contiue sucking our bloods in new fasion that me and you know nothing about it. Welcome to my world,talk that walk but don't even think about walk that walk.
 
Single D, nadhani umeongea point moja muhimu sana kuhusu maadili. lakini naomba niongeze hoja kwamba siyo maadili ya uongozi ni maadili ya watanzania wote. Si CCM, wala CUF wala Chadema, si kiongozi , si watendaji si wafanyabiashara nk.
Naomba kuuliza wakati fedha za mafisadi inapelekwa CRDB na NBC mbona benki hizi binfasi zilipokea pesa bila kuuliza maswali hasa baada ya restrictions zinazotokana na Money laundering Act!? Kwa hiyo nadhani maadili kwa ujumla yamemomonyoka!
Also ni kwelikwamba kusema CCM yote ni ya mafisadi is too simple. Mi nadhani mfumo uliopo wa kuwachagua viongozi una hitlafu mkubwa sana. Ukiangalia mfumo uliopo CCM ulitegemea uongozi wa mtu moja mwenye busara (benevolent dictator) ambaye alikuwa Nyerere. Sasa kutokuwepo kwa Nyerere huleta hoja nani atasimamia utaratibu wa kuchagua uongozi bora ndani ya chama? Hata watu wengine wakijaribu bahati yao wanaambiwa system haiendi hivyo lazima ulipe takrima (hebu jaribu kufuatilia kampeni ya Salim Ahmed Salim na alivyokuwa anaombwa takrima na waandishi na wananchi wengine wakimwambia kwamba wenzake wanamtandao wanalipa vizuri!). Sasa kwa utaratibu huu unafikiri watachagua viongozi gani?
Also FMES amezungumzia a viable alternative, nadhani muda umefika kwa Chadema kujiimarisha na kuonyesha that they are viable alternative. Ni watu ambao wako kwa ajili ya taifa na siyo anti-CCM. Kuna tofauti kubwa.
Kama wangeweza kuwaconvince disillusioned CCM members kwamba si wanachama wote wa CCM ni mafisadi and there's room for them, wataweza kushinda vizuri tu. Tatizo imekuwa them vs. us. Na kwa hiyo haitawezekana kubadilisha uongozi ila kwa conflict kubwa.
Just adding my five cents...
 
Mtazungumza sana ,hata CCM ikiondoka au kuondolewa bado ukilitimba utaendelea tena kwa nguvu mpya na mbaya zaidi.
Kukata mzizi wa fitina ni kuundwa kwa katiba mpya ambayo itaangalia kila sehemu ya utawala na utawaliwa ,hakuna cha kujadiliana hapa zaidi ya kupeana matumaini yasiyotekelezeka nyimbo iwe ni Katiba mpya hili jamani halina mjadala CCM wanalijua hilo na ndilo jambo kubwa wanaloliogopa kuliko jengine lolote ,haya makelele ya kuwaumbua mafisadi hayana mshiko kabisa ni kasheshe ya bahari kuchafuka tu ila mkiwa na chombo imara basi mtavuka na ndipo walipo au walimo CCM ,kwa machafuko haya huwaga wanavuka tu japo wengine watadondoka lakini hawazami wataokolewa na ndivyo tunavyoona leo ,machafuko yote yanayotokea unaikuta CCM imesimama kidete ili kujiponya ,siku hizi kuna msemo wa eti kutoa kafara ,jamani si mnaona mambo yakizidi utaanza kusikia minong'ono ya kuna watu wanataka kutolewa kafara na ndio hapo wanapovukia Katiba haina kinga kwa kafara yao.
Kama kweli tunataka na tunahitaji mabadiliko basi ni lazima kama kufa KATIBA ibadilishwe ili iendane na wakati ama kwa kasi hizi alizokuja nazo Muungwana watamaliza kila kitu na hakuna jipya isipokuwa makafara yataongezeka tu ,au hamlioni hilo ?
 
Kwa mtizamo wangu,Naona Mzizi mkuu wa ufisadi umejikita kwenye UKOSEFU WA MAADILI KATIKA UONGOZI.
Maadili yanapokosekana ktk uongozi kinachotokea ni kupora au kuvuruga maamuzi sahihi,kupuuza hoja za wananchi au kupindisha kwa maslahi ya kiongozi fulani.

Mkuu Single D,
Naona umeanza kulenga penyewe,lakini chimba zaidi,kwa nini viongozi wanakosa maadili. Ama ilikuwaje kukaanza kuwepo ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi? Nakuhakikishia ukichimba zaidi utaipata ncha ya mzizi.
 
Thanks Mkuu.
Nani wa kuing'oa CCM? kwanza watakaoing'oa CCM ni wana CCM. so sis kama wananchi tunatakiwa kuanzisha chaos then CCM ikapanguka and that is only way.

CCM inatupeleka ziwani, its a matter of time tutakuwa drown wote tulio ndani ya MV Tanzania.

Mkuu Mtanganyika,
CCM sio mzizi wa ufisadi bali ni ngome ya mafisadi,field Marshall akwambie kwamba katika mapigano, ili kushinda vita lazima ngome zibomolewe. Bado nasisitiza,tafuta mzizi ndugu yangu,kuibomoa CCM au kuong'oa hakutatosha.Dig deeper
 
CCM yote ni wachafu na ni Mafisadi, lakini mimi nitaendelea kuombea siku moja amani itoweke

Hichi kimsemo cha wapenda amani ni kibovu sana na ndo kinatuaharibia nchi yetu

Watu tutaingia msituni na tukiibuka ni vita na matajiri walioiba pesa za wananchi, watakaopona wataanza mambo mapya kwa sheria mpya, ila totakoondoka tutaondoka kishujaa kwa kutetea utu na raslimali za nchi yetu

MMMM? hapa Baba H you got to think twice
 
Single D, nadhani umeongea point moja muhimu sana kuhusu maadili. lakini naomba niongeze hoja kwamba siyo maadili ya uongozi ni maadili ya watanzania wote. Si CCM, wala CUF wala Chadema, si kiongozi , si watendaji si wafanyabiashara nk.
Naomba kuuliza wakati fedha za mafisadi inapelekwa CRDB na NBC mbona benki hizi binfasi zilipokea pesa bila kuuliza maswali hasa baada ya restrictions zinazotokana na Money laundering Act!? Kwa hiyo nadhani maadili kwa ujumla yamemomonyoka!
...

Ndugu Susuviri,
Ni kweli ukosefu wa maadili ni tatizo la nchi nzima. Na hapo ndipo mbongo zifanye kazi,ilianzaanzaje maadili yakamomonyoka? Nini historia yake na ni nini kilisababisha hili?
 
Mtazungumza sana ,hata CCM ikiondoka au kuondolewa bado ukilitimba utaendelea tena kwa nguvu mpya na mbaya zaidi.
Kukata mzizi wa fitina ni kuundwa kwa katiba mpya ambayo itaangalia kila sehemu ya utawala na utawaliwa ,hakuna cha kujadiliana hapa zaidi ya kupeana matumaini yasiyotekelezeka nyimbo iwe ni Katiba mpya hili jamani halina mjadala kama kufa KATIBA ibadilishwe ili iendane na wakati ama kwa kasi hizi alizokuja nazo Muungwana watamaliza kila kitu na hakuna jipya isipokuwa makafara yataongezeka tu ,au hamlioni hilo ?

Ndugu Mwiba,
Wadhani katiba mpya itaondoa rushwa katika vyombo vya sheria,au itakomesha matrafiki kuwapiga madereva mabao, au itakomesha wizi wa kura,au itaondoa ubadhilifu na uchafu mwingine katika taasisi za umma na za binafsi na katika jamii kwa ujumla? Ebu utazame ufisadi kwa ujumla wake.
 
Mkuu Single D,
Naona umeanza kulenga penyewe,lakini chimba zaidi,kwa nini viongozi wanakosa maadili. Ama ilikuwaje kukaanza kuwepo ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi? Nakuhakikishia ukichimba zaidi utaipata ncha ya mzizi.

Dear Waridi,
Kwa mtizamo wangu ukosefu wa Maadili ya viongozi katika utumishi wa umma ulianza pale tu ilipobomolewa misingi ya Azimio la Arusha ule mwaka 1991 na kuanza lile la ZANZIBAR mwaka huo huo ambalo lilihimiza LAZIMA TWENDE NA WAKATI,KILA ZAMA NA MWONGOZO WAKE.
Tokea hapo ikawa fungulia mbwa kwa watawala,ndipo kukakithiri UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA KWA KASI KUBWA NA PIA RUSHWA IKAONGEZEKA miongoni mwa Viongozi.Pamoja na kutungwa sheria ikiwamo ya Mwaka 1995 KUHUSU maadili ya hawa viongozi lakini haijasimamiwa kutoa matunda halisi ingawa ipo na wizara maalum kabisa ya uongozi na utawala bora hapo OFISI YA MKUU WA NCHI.Kama ya 1995 imepitwa na wakati,basi tuone haja ya kuwepo sheria nyingine isaidie huu uozo.

1.Nisemapo Ubadhirifu wa mali ya umma umekithiri miongoni mwa viongozi namaanisha wanatumia hizi mali/raslimali za nchi aidha kwa matumizi binafsi kama ufuska(Leo hii magari ya serikali yanapaki maeneo si maalum kama vichochoro vya gizani kuopoa NYAPU)n.k.Wakati huo wanatoza kodi tena kwa fujo kweli hao wanaofanya magari hayo yatembee na hizo ofisi ziwepo.Mwisho wa mambo yote ya uozo wa serikali umefika.Jifunzeni kwa Generally msharafu,Kibaki,na comrade mgabe.SERIKALI ZA UOVU NA UOZO NI KIPINDI CHAKE KUANGUKA.

2.Rushwa imeelezwa zaidi kwenye ripoti ya TUME YA JAJI WARIOBA,Lakini haikusaidia.Hii rushwa kwa viongozi nionavyo mimi huanzia pale viongozi wanapokubali rushwa iliyotolewa kwa jina la zawadi,bakshishi au takrima ambayo hupambwa na sifa nyingi sana ili isionekane ni dhambi kwao.Kiongozi unalipwa pesa za walipa kodi,tena unataka zawadi kwao???Naililia Tanzania.

Katibu mkuu wa CCM mgosi Makamba alitoa kakitabu kake ka makatazo ya Rushwa kwa kunukuu maneno mengi ya vitabu vitakatifu(Quran na Biblia)lakini leo hapo alipo katibu mkuu wa CCM kwa nini asiwasomee ako ka kitabu maana viongozi wengi wananuka rushwa,wanapotosha sheria na hii inatokana na maslahi binafsi kwa viongozi wengi kujiingiza ktk mabizinesi na mabiashara?

Wengi wanaingia uongozi kutuibia,akiacha tu uongozi maana mirija ya wizi imefungwa,basi biashara inasambaratika na mwenyewe kushikwa na shinikizo kila wakati.TULIKUWA NA SCANDNAVIA,COMMUNITY AIR LINES N.K NA ZILITUSAIDIA SANA LEO ZIKO WAPI??(Asomaye na afahamu)
3......................
4...............
 
Kwa sasa Uongozi sio kuongoza tena, ila uongozi umekua aina nyingine ya biashara .... watu wanataka uongozi ili wapate heshima katika jamii then waweze kafanya biashara zao vizuri ama katika nafasi hiyo wapate utajiri. Tumeshuhudia wafanyabiashara wengi wakikimbilia kwenye siasa.

Pia ni kweli jamii nzima inakosa uadilifu. Wakati wa kampeni za uchaguzi ukienda kwa wananchi kuhubiri sera na ilani bila chochote hutasikizwa kirahisi... watakwambia mkono mtupu haulambwi........yaani hata ukiwaibia na kuwarudishia kidogo watakutukuza. Ndio maana wenye mitaji wanaingia kwenye siasa kirahisi sana.

Kisha kiongozi awapo mwadilifu, jamii huwa ya kwanza kumlaumu alivyochezea nafasi aliyopata hata akabaki na umasikini wake! Kwa maneno mengine jamii kwa ujumla wake haipendi uadilifu! Ukiwa mkurugenzi katika ofisi ya umma unategemewa uwe tajiri, tena haraka!

Watu kama mzee Apiyo wamekuwa ni mifano ya failure katika jamii yetu.....hatujivunii waadilifu wetu!
 
Tanzania sasa hivi ina matatizo mengi sana na solution yake ni ngumu kuipata, kila sector kuna matatizo hakuna sehemu unayoweza kusema kuwa ni pazuri hata kidogo.
Ni kweli kabisa ufisadi sasa ni moja ya rule za maisha yetu, maana watu wanajilimbikizia mali nying sana. mtu mshahara haufiki 500,000 lakini angalia mali alizonazo, anazipata wapi watanzania wengi ni mafisadi, hata CCM wakityoka madarakani bado ili tatizo litakuwepo. Tunaitaji maadili ya jamii kwa watanzania wote sio CCM pekee hata vyama vyote vya upinzani maana nao kila siku wanagombea ruzuku, hata wakipewa vinafasi kidogo waburunda mfano issue ya Dr. kaburu na Dr. Kitine
 
Mimi Nadhani Ili Kupata Root Cause Ya Ufisadi An Indepth Analysis Inabidi Ifanyike With Some Powerful Analyzing Tools, Kwa Sababu Hata Maadili Inaweza Kuwa Si Mzizi. Maana Mtuhazaliwi Akiwa Na Maadili. Maadili Hufundishwa From That Tender Age, Nyumbani, Shule, Mtaani, Kazini Etc. Practical Ndio Ishu.... Sasa Tusirahisishe Hii Mada Let's Think And Workout!!!!!!!!
 
Ahsanteni sana wanaJF kwa mchango mzuri sana tena sana. Sasa mjadala wa mada unapata mwelekeo mpevu.

Naomba tunapoendelea kutafakari na kuchangia ebu tupekue ujumbe wa ndani uliomo katika nukuu hizi
  • Rushwa ni wimbo wa sumu uliotapakaa katika ubongo wa KILA mwanataifa hili, tuondolee wimbo huu tafadhali- Mwimbaji Mpoto
  • TAMAA ikichukua mimba huzaa DHAMBI,DHAMBI ikiisha kukomaa huzaa mAUTI - Biblia
  • VIONGOZI ni zao la JAMII- hii sikumbuki alisema nani
  • Mdharau mwiba mguu huota tende- wahenga

Ni kweli ndugu zangu,kwamba ufisadi tulio nao leo chimbuko lake lina historia ndefu katika matukio ya kisiasa na matendo ya jamii kwa ujumla,jambo hili unaweza vile vile kulitazama hivi:

mtu mmoja akikosa maadili ni tatizo kwa familia
familia moja ikikosa maadili ni tatizo kwa kijiji
kijiji kimoja kikikosa maadili ni tatizo kwa kata
kata moja ikikosa maadili ni tatizo kwa tarafa
vivyo hivyo tarafa kengeufu huathiri wilaya
wilaya nayo huaribu mkoa
kutoka mkoani au majimboni taifa linadhurika

Nikweli pia kwamba joka linalotutesa sasa tumelilea wenyewe
Matharani,
Enzi zile(na hata sasa) watoto wetu na ndugu zetu walipopata ajira katika mashirika ya umma,tukawashinikiza watajirike na ambao hawakufanya hivyo tukawacheka, tulisababisha tamaa miongoni mwa watumishi wa umma wote. Hatimaye tamaa ikachukua mimba na ikazaa DHAMBI(mitiri ya joka)
Hili ni mojawapo ya maeneo tulipojikwaa na tulipoangukia tugagonga pua. Kilichotoka humo watoto wetu na ndugu zetu wakayaibia mashirika yakawa mufilisi, tukayauza.Tena kwa sababu tamaa ilikwisha kuzaa dhambi, yakauzwa hata ambayo yalikuwa yana nafuu.Mkosi nao ukaambatana na hilo,mengi tukawauzia ambao si wenzetu!!!

Aidha enzi zile,tulipofuata huduma maofisini, mfano mahakamani,hospitalini na kwingineko,watumishi wa umma chini ya shinikizo la jamii linalowatarajia watajirike,wakatuomba chai,wakachukua 10%,wakaleta misemo ya kuzunguka mbuyu, kula mlungula,shati la mikono mirefu na mingine nikumbusheni...
Laiti tungelijua ndio hivyo tulikuwa taratiiibutunamfuga nyoka mwenye sumu ya kufisha mithiri ya weapons of mass destruction.

Kwa upande mingine, hata mitazamo na matukio katika uwanja wa siasa yalichangia. Kila mtu alipopewa wadhifa(hata leo) utasikia akipongezwa kwa misemo ya kifisadi fisadi,mfano ..hongera sana ndugu UMEULA!! Ilikuwaje hatukutafakari tunamwambia ameula unini???
Twende mbele kidogo,(namkoma nyani hapa),
Yule mzee wa mkoa wa Rukwa aliyegombea ubunge dhidi ya Mzindakaya,akapigwa chini kura za maoni akakimbilia NCCR,akapachikwa unaibu katibu mkuu,akakuta NCCR hakuna mijihela aliyoizoea alikokuwa CCM,na juzi alivyoona mtu wa kwao kawa waziri mkuu,eti katangaza kurudi CCM (siasa za bongo bwana!).
Alipokuwa NCCR alilopoka hivi,
Sisi(yaani yeye na watu fulani ndani ya CCM) ndio tulishauri CCM iwakaribishe matajiri chamani,wakati vyama vingi vinakaribia kurejeshwa nchini.Tukasema,tukiendelea kushikilia eti CCM ni ya wakulima na wafanyakazi vyama vingine vitawachukua matajiri na kutuzidi nguvu
HUO ndio ulikuwa mwanzo wa mafisadi wengi kujikusanya ndani ya ngome moja,yaani CCM,lakini si kwamba hapo ndipo walipochimbuka,walichimbuka katika jamii kengeufu!!!

Kilichofuatia basi,ikawa ni kutimiza lile neno lililonenwa na nabii Yesu aliposema
KWA MAANA PALIPO NA MZOGA,NDIPO WAKUSANYIKAPO TAIHakika likatimia,matajiri wa hela chafu na wa hela safi(Matharani wale walioitikia wito wa mzee Sumaye kwamba anayetaka mambo yake ya kibiashara yamnyokee ajiunge CCM)wakaikimbilia ngome ya sisiemuuu,wenye tamaa nao wakaona,kumbe mambo ya fwedha ni CCM!! hao wakogombea udiwani,ujumbe wa shingo(NEC), ubunge,na hata urais. Au hamjui ni kwa nini CCM ina wanachama kibao, vijana wasomi wanakimbilia huko na maprofesa wanazitelekeza lecture rooms.Open your eyes and see this single reason amongst some others.

Kilichoambatana na hayo CCM ikajirundikia mafwedha kibao,eti ruzuku.Ikaendelea kuenjoy pia vitega uchumi ilivyovikusanya enzi za mfumo wa chama kimoja..Loo! tai wakazidi kumiminika katika bonde lenye mzoga.Ama kwa hakika katika vita yetu, lazima kuisambaratisha hii ngome.
Lakini tunarudi kule kule,tamaa ya tai wote hawa wamefugwa na kulelewa na jamii.Tena na tai wengine tunao, bado wako katika taasisi za umma,wengine kwenye vyama vya upinzani,kwenye NGOs ndo usiseme,hata private sector,ilimradi tu ni ka-nchi kananuka rushwa(Alisema Mwalimu,R.I.P)
Ngugu zangu,ni kwa dawa ipi tuiponye JAMII,tena tuiponye haraka kabla hatujaangamia sote.Je,tuanzie katika elimu ya malezi mashuleni na katika kaya,au tufanyeje????
 
Naomba nielezee mambo makuu manne yanayoweza kusaidia uchambuzi kuelekea mzizi (Mizizi) ya rushwa na ufisadi.
1. Muundo (Uwe wa Serikali, au taasisi yoyote) Muundo unaweza kuwa chanzo kikubwa cha ufisadi.
Katika ngazi ya serikali miundo muhimu kama kuwepo kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa na nafasi yake katika muundo wa serikali. Kamati za kuzuia rushwa katika idara za serikali na taasisi nyingine(Kama zipo na zinawajibika kwa nani?) Je bunge letu linayo kamati ambayo inashughulikia utawala bora na maswala ya rushwa na iko chini ya nani na mipaka yake ni ipi na madaraka yake ni yepi?, Je kuna mahakama maalu zinazoshughulikia rushwa?. Maswala ya Muundo yakifanyiwa kazi yanaweza kuondoa mifumo ya serikali inayoacha mwanya wa ufisadi. Katika sekta binafsi na taasisi nyingine maswala ya kujiuliza ni kama taasisi inao muundo, je nani nanawajibika kwa nani nk. Uchambuzi wa awali usaidie kubaini changamoto za ufisadi zinazotokana na miundo ya serikali , idara zake, makampuni na asasi nyingine
2.Taratibu na Kanuni nyingine za kiutendaji. Uwajibikaji huanzia kwenye kufuata sheria, kanuni na taratibu za kushughulikia maswala mbalimbali ambayo yanaangukia katika majukumu ya makusudio ya kuanzishwa kwa taasisi yoyote. Hatua ya pili iende kwenye hizo taratibu, kanuni na sheria ili kubaini ni zipi ambazo ni kichocheo cha ufisadi. Kwa mfano, iwapo wafanyabiashara na walipa kodi wengine wasio waajiriwa hutakiwa kujaza marejesho ya mapato yao kila ifikapo mwisho wa mwezi machi ili kuainisha mapato yao kwa kipindi cha mwaka wa biashara uliopita, ni rahisi kwa kutumia taratibu hii kubaini mapato ya mfanyabiashara. Kwanini taratibu hii isitumike kwa watu wote?-- Matokeo ya uchambuzi wa taratibu na sheria unaweza ukasaidia kuweka taratibu zitakazoondoa mianya ya ufisadi.
3. Maswala ya kibinadamu (Human Factors). Pamoja na yote yanayoweza kufanyika kama ilivyoelezwa hapo juu, binadamu ndio wanaoendasha serikali, taasisi a kampuni.Wao ndio wenye kuweka miundo na mifumo, ndio wenye kuweka taratibu na ndio wenye kusimamia(au kutosimamia) hiyo mifumo na taratibu Ni muhimu, kwahiyo, kuwapima watendaji katika taasisi kwa vigezo vya uadilifu wao ili uweze kuwa na uhakika wa uadilifu wa taasisi.
4. Jamii. Jamii inalionaje swala la rushwa na ufisadi? Je wale wahalifu ndio wenye kupewa heshima na "viti vya mbele"? na wale waadilifu wanaonekana kama ni watu waliokosea kitu fulani katika utendaji? Mtazamo wa jamii kwenye maswala ya ufisadi inaweza kuwa kichocheo au silaha kubwa katika kupambana na ufisadi.
Sio nia yangu kutoa mada lakini niliona nishiriki katika mjadala huu uliouanzisha.
Kila la kheri
 
Mtaalam mmoja ameniambia hivi, kinachokosekana katika nchi yetu ni mifumo imara, na taasisi madhubuti za kuhakikisha kila jambo linaenda kiuadilifu na kamwe uovu wowote haupati fursa. hivyo licha ya kuchimbua mzizi kwa mikakati ya muda mrefu, sharti tuwe na mifumo na taasisi zenye meno ya chuma cha pua, vinginevyo mzimu wa ufisadi utaendelea kutuandama.
By the way, Uholanzi iliwahi kukaa miezi kadhaa bila serikali lakini kila jambo lilienda sawa kwani wanazo taasisi na mifumo isiyoteteleka.
 
Mkuu

Tatizo linalotukabili Tanzania ni tatizo la uongozi, Matatizo yote yaliyopo yana dawa yake. Ni kwamba hatuwezi kuendelea kwa kukumbatia sheria tulizo nazo. Kama ni ujanja ujanja wananchi wote wameisha kuwa wajanja.

Wanajua mianya yote ya UFISADI, pamoja na rushwa ndogo ndogo. Viongozi walio madarakani wanafaidika sana na mifumo hii, ndiyo maana wakisikia mtu yeyote anazungumzia suala la sheria wanakuja juu na kutaka kibadilishwe kifungu kimoja au kiwekewe kiraka.

Tukitaka tukate mzizi wa fitina Tanzania ni lazima tudai kwa nguvu zote kuandikwa upya katiba ya nchi, hili litaenda sambamba na mjadala wa kitaifa kuhusu lipi linatakiwa na lipi halitakiwi na lifanyikeje.

Hivyo ndivyo tutaweza kuwamaliza mafisadi bila kuleta matatizo. Lakini kwa hali halisi tuliyo nayo ni shida tu. Hakuta kuwa na nafuu yeyote katika suala zima la maendeleo labda maendeleo yatabaki kuwa kwa viongozi wachache wakishirikiana na wafadhiri wao tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom