Mzizi Mkuu Wa Ufisadi

Mkuu

Tatizo linalotukabili Tanzania ni tatizo la uongozi, Matatizo yote yaliyopo yana dawa yake. Ni kwamba hatuwezi kuendelea kwa kukumbatia sheria tulizo nazo. Kama ni ujanja ujanja wananchi wote wameisha kuwa wajanja.

Wanajua mianya yote ya UFISADI, pamoja na rushwa ndogo ndogo. Viongozi walio madarakani wanafaidika sana na mifumo hii, ndiyo maana wakisikia mtu yeyote anazungumzia suala la sheria wanakuja juu na kutaka kibadilishwe kifungu kimoja au kiwekewe kiraka.

Tukitaka tukate mzizi wa fitina Tanzania ni lazima tudai kwa nguvu zote kuandikwa upya katiba ya nchi, hili litaenda sambamba na mjadala wa kitaifa kuhusu lipi linatakiwa na lipi halitakiwi na lifanyikeje.

Hivyo ndivyo tutaweza kuwamaliza mafisadi bila kuleta matatizo. Lakini kwa hali halisi tuliyo nayo ni shida tu. Hakuta kuwa na nafuu yeyote katika suala zima la maendeleo labda maendeleo yatabaki kuwa kwa viongozi wachache wakishirikiana na wafadhiri wao tu.

Nimeikumbuka hii, kwamba kwa kuchoshwa na ufisadi, wanaJF tulianza kudai katika mpya miaka miwili (au zaidi) kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Je, katiba mpya ikipatikana, ufisadi utakuwa umepata dawa? lets resume the dig
 
Back
Top Bottom