Mzee Yusuph amkataa mtoto aliyedai ni mwanae wa nje ya ndoa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa majina ya Ahmad Yusuph Mzee, amejitokeza hadharani katika studio za Wasafi Media akidai kwamba yeye ni mtoto wa mzee Yusuph wa damu kabisa ambapo anasema kwamba mama yake ambaye ni Marehemu kwa sasa alipewa ujauzito na Mzee Yusuph wakati alipokuwa akihudumu kama MC kwenye moja ya kumbi iliyokuwa huko Mbagala miaka ya 2002.

Ahmad anasema awali alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mume wa mama yake ambaye awali alikuwa anamtambua kama baba yake mzazi, lakini kabla mama yake hajafariki alimweleza ukweli kwamba hakua baba yake wa kumzaa bali baba yake ni Mzee Yusuph ambaye ndiye huyu muimba taarabu.

Ahmad amesema licha ya kwamba anatambua kama Mzee ana mali za kutosha na ni mtu maarufu, yeye kipaumbele chake anataka wakapime DNA ajiridhishe kama kweli Mzee Yusuph ni baba yake mzazi ili awe na faraja pamoja na amani ya kujihisi yupo salama duniani kwani kwa maisha anayoishi sasa ni kwamba hana baba wala mama, maisha ambayo ni hatari na siyo kwamba anamtafuta ili apate upenyo wa kurithi mali.

Kwa upande wa Mzee Yusuph licha ya kufanana na mtoto huyo kuanzia Mapua, Mdomo, Mashavu, kichwa mpaka rangi ya meno na ngozi. Bila aibu Mzee amesema hamtambui kijana huyo kama mtoto wake na hana kumbukumbu kama aliwahi kucheza michezo ya hasara huko Mbagala kiasi cha kumpatia mwanamke ujauzito.

Awali Mzee Yusuph alikataa kabisa kupima DNA lakini baadae baada ya kushinikizwa alikubali kwenda kupima DNA lakini kwa masharti mazito, ambapo amesema kijana huyo akitaka wakapime DNA pesa ya vipimo aitafute mwenyewe kijana na andapo atakuta siyo mtoto wake basi hatua kali za kisheria za uzalilishaji zitachukuliwa dhidi yake, aidha Yusuph ameongeza kuwa kama akikuta mtoto huyo ni damu yake atamfikilia kama aendelee kumlea au aachane naye kwani dini yake inasema mtoto wa nje ya ndoa siyo mtoto wake ni wa mwanamke.
Screenshots_2023-06-18-05-54-20.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
aidha Yusuph ameongeza kuwa kama akikuta mtoto huyo ni damu yake atamfikilia kama aendelee kumlea au aachane naye kwani dini yake inasema mtoto wa nje ya ndoa siyo mtoto wake ni wa mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini dogo si amesema tu anataka kujua km yeye ni baba yake au sio hayo masuala ya kumsaidia hajasema km anataka au nimesoma vibaya
 
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa majina ya Ahmad Yusuph Mzee, amejitokeza hadharani katika studio za Wasafi Media akidai kwamba yeye ni mtoto wa mzee Yusuph wa damu kabisa ambapo anasema kwamba mama yake ambaye ni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufanana huwa kunatokea hata kwa watu ambao hawahusiani.
Harmonize angekuwa na umri wa Mshana Jr halafu Hamorapa akajitokeza kudai Harmo ni baba yake, watu wangeamini sababu ya kufanana huko na Harmo hata angejitetea vipi bado asingeeleweka, ndiyo ninachokiona hapa.

Utetezi wa huyo mzee Yusuf nao ni wa kupuyanga, kumpa mimba mwanamke wa Mbagala siyo lazima ukutane naye Mbagala kipindi ukifanya kazi huko, labda anatumia hiyo hoja ya huyo dogo.

Upande wa dogo yeye ni wale akina akili matope. Story za baba na mama yake walikutania wapi ma wakapeania mimba wapi hazipaswi kuongelewa naye tena in public.
 
wakapime DNA ajiridhishe kama kweli Mzee Yusuph ni baba yake mzazi ili awe na faraja pamoja na amani ya kujihisi yupo salama duniani kwani kwa maisha anayoishi sasa ni kwamba hana baba wala mama, maisha ambayo ni hatari
.
View attachment 2660998

Sent using Jamii Forums mobile app

Dogo kafika miaka 20 ndo anashtuka kuishi bila mama na baba ni hatari!
Au anataka kukwepa jukumu la kujitafutia maisha yake so anatafuta shortcut kwa Yusufu?
 
Pombe bangi.....mbaya sana....
Mzee Yusuph amewazalisha wengi style hiyo akiwa star miaka hiyo yote anaujua ukweli .....kama alienda kuhiji na kusema uongo sielewi alienda kufanya nini huko .....kitu kidogo hicho ......angekubali yaishe kijana ajue ana baba akitaka kumsaidia sawa ama la basi....
 
Back
Top Bottom