Mzee wa upako atoa mpya!

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, amesema anaunga mkono viongozi wa dini kuwa matajiri. Amesema kuwa, hapingi viongozi wa dini kuwa na utajiri uliopindukia, kwa kuwa utajiri kwa wanadamu ndio mpango wa Mwenyezi Mungu.


Mzee wa Upako aliyasema hayo jana, Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Kiongozi wa dini kuwa tajiri siyo dhambi, bali hoja iliyopo ni kuhusu njia zilizotumika kupata utajiri huo.

“Mwenyezi Mungu hakuwaleta binadamu duniani waje kuwa masikini, kiongozi wa dini kuwa tajiri hakuna ubaya, suala hapa mali hizo amezipataje?.

“Hiyo ndiyo hoja kwangu, lakini utajiri unashida gani?, mimi nina gari sita zote kali na pia nina mpango wa kununua ndege kama ilivyo Marekani, ambako kuna mchungaji anamiliki ndege tatu na ni kiongozi wa dini anayeheshimika.

“Yupo mwingine wa huko huko Marekani, aliwahi kuja pale Kenya na ndege nane, ndege moja ikiwa imebeba maji tu, haya ndiyo maisha ambayo Mungu anataka tuishi,” alisema Mzee wa Upako.
 
Back
Top Bottom