Mzee wa Upako ahoji mantiki ya CCM kujifananisha na nyoka katika ngonjera ya CCM kujivua gamba

Unaweza kutafsiri kwa namna unayojua lakini tafsiri sahihi ya kujivua Gamba kwa CCM wanayo wanaCCM wenyewe.
 
Wakati wa agano la kale mungu aliandaa nyoka wa shaba ambaye kila aliye mtanzama alipona.

Hosptali zote zina nembo ya nyoka!!!

Pesa ya tsh 500 ina nembo ya shaba.

Mungu anatusisitiza kuwa wajanja kama nyoka sasa nadhani mzee wa upako kashindwa kuelewa bible



mbaya sana mzee wa upako ndiye aliyeshauli jk kumufukuza rostam aziz lakini sasa anakwepa na kutumika na mafisadi
 
Namshangaa Mzee wa Upako kushindwa kuelewa CCM kujifananisha na NYOKA. Names have spirits. Kama mtu akiitwa NYOKA kweli atakuwa na TABIA ya Nyoka. Na mara nyingi MTU ANAPOONGEA anajaribu ku-express/reveal kile kilicho ndani ya NAFSI yake!!!Kwa hiyo KIWETE aliposema kuwa WANATAKA KUJIVUA GAMBA KAMA NYOKA he was correct by 100 pc. Nani asiyejua kuwa CCM NI NYOKA?


I believe Mzee wa upako anajua characteristics za nyoka:
  1. Sumu kali ya kuua palepale anapokugonga.
  2. Mate yake ni sumu kali akikutemea.
  3. Uongo au udanganyifu(Biblical serpent).
  4. Kujivua gamba kila baada ya muda ili kujirudisha upya.
  5. Kutambaa kwa tumbo au kuruka
  6. n.k
CCM wana hizo tabia kwa ujumla wake. Kama ni sumu walishawatemea Wa-tz wote,kama ni mate walishatutemea sana,kama ni UONGO CCM wamelidanganya taifa hili for almost 50 years(tangu enzi za TANU). Sasa ndo wanajivua gamba ili WAPATE KASI ZAIDI YA KUNG'ATA ZAIDI NA SUMU YAO KALI YA UFISADI,wapate kasi zaidi ya KUWADANGANYA Wadanganyika.

Tangu enzi za Biblia Nyoka ni adui wa bin-Adamu. Mungu alimwagiza mwana-Adamu popote atakapomwona NYOKA AMPONDE KICHWA. Sumu ya nyoka siku zote iko kwenye KICHWA CHA NYOKA. Ukishapiponda KICHWA cha nyoka umeshammaliza.

Watanzania tunatakiwa kujua KICHWA CHA NYOKA CCM ni kipi ili TUPAPIGE HAPO HAPO ILI KUMMALIZA asije akaendelea kutugonga!!!!

Namimi mjori wa Bwana sitatenda kinyume na mapenzi yake,
Nitatenda kama ulivyoniagiza Mungu wangu nitalenga kichwani tu na sio kwenye GAMBA.
 
kuvua gamba ni lugha ya picha inayomaanisha kuanza upya kwa jambo na wala haihitaji uwe mchungaji au msomi uliebobea kuelewa nini chamaanishwa labda kama mtu anataka kupotosha makusudi.
Kama unaona kujivua gamba ni lugha ya picha basi tafsiri nyingine ni kuwa tumuogope sumu yake ni kali mno!
 
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.

Japo naafikiana na huyu mbabaishaji,lakini kinachonishangaza ni ukweli kuwa juzi juzi tu alikuwa mstari wa mbele kujikomba kwa JK akidai asilaumiwe kwa kila kitu.Sasa hiyo CCM anayoilaumu kwa kauli-mbiu ya kujivua magamba inaongozwa na Obote?Au aliyeanzisha kaulimbiu hiyo ni Edwin Mtei?

Honestly,I strongly doubt credentials za huyu "Mzee wa Upako".Watumishi halisi wa Bwana hawawezi kuwa watumwa wa publicity.
 
Jamani CCM imewakosea nini? yaani nyie kila kitu kwa CCM ni kibaya? mbona watu wa JF hamna shukurani? Au ndio ule msemo wa tenda wema nenda zako wala usingoje shukurani unatimia?
Uongo wao uko wapi?si wanatoa ytafsiri ya kujivua gamba kwa nyoka na maana halisi ya tabia za nyoka?
 
mzee upako hana jipya, alitegemea sana sadaka na zaka kutoka kwa waumini wake lakini sasa tangu waumini waende kwa babu loliondo hawarudi tena kwenye maombi yake! kanisa limebaki tupu! sadaka atapata wapi? kwa mafisadi!!!
 
RA, EL na Chenge watacheza sana na watu /Viongozi wenye kuwa na mvuto na watu wengi

kuna hatari kubwa ya Misikiti, Makanisa na hata Vyama vya siasa kusambaratika maraa baaya ya siku 90 za CCM kwisha
 
Sasa kama kujivua gamba ni mfano mbaya je operation sangara ni mfano gani.????

Sangara ni samaki anaye kula watu . Baada ya ajali ya mv bukoba watu waliacha kula sangara.

Hata hivyo huu ni mtazamo watu tofauti.
Yesu anaitwa nyoka wa shaba katika agano la kale nyoka wa shaba alitundikwa na kila aliyemtazama alipona.

Hii ndiyo chazo cha hospitali kuwekewa alama ya nyoka.

Mbona hata tshs 500 ambayo babu wa loliondo anataka ina alama ya nyoka??

Mzee wa upako ana upeo mdogo wa maandiko??
 
Mantiki iliyopo ni mafisadi kutumia watu ilikujilinda wasifukuzwe.

Gazeti la mtanzania lipo ukingoni kwa sababu ccm imekiri kuwa ni la mafisadi!!!

Ndiyo maana hata wakati wa uchaguzi mafisadi walitumia rai kumushambulia slaa

mtanzania ni mafisadi
rai ni mafisadi pia
 
kuvua gamba ni lugha ya picha inayomaanisha kuanza upya kwa jambo na wala haihitaji uwe mchungaji au msomi uliebobea kuelewa nini chamaanishwa labda kama mtu anataka kupotosha makusudi.

Binadamu ana gamba? Wewe wa wapi?
 
Jamani CCM imewakosea nini? yaani nyie kila kitu kwa CCM ni kibaya? mbona watu wa JF hamna shukurani? Au ndio ule msemo wa tenda wema nenda zako wala usingoje shukurani unatimia?

Akili yako sawa na chimpanzee.
 
Mzee wa upako ni tatizo kwa jamii kwa sababu kwanza hajui philosophia ya ndumila kuwili kuwa ni lazima sana ukumbuke mambo uliyofanya jana, kitu ulichosema na watu uliowambia na kwa nini ilikuwa lzima ufanye au kutenda vile ulivyotenda. Yeye sasa inaonekana ni mzee wa tumbo sio upako na sasa kazi yake ya upako imemalizwa na babu anatafuta turufu nyingine ya kumudu maisha yake na inawezekana anatafuta upenya wa kuingia siasa lakini naona hana nafasi. Katika imani unaweza kufanikisha kuwadanganya waumini saa zote, muda wote na kwa mambo yote lakini sii hivyo kwenye siasa hatapata hata wa kumsikiliza aluta contnua tuwakatae opportunist kama mzee wa upako kwanini anapewa fursa kwenye jukwaa hili kwa upupu wake
 
Back
Top Bottom